Kwako Jaji Mutungi, Kampeni za Uchaguzi wa Urais 2025 zimeruhusiwa Rasmi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,175
22,697
Amesikika Katibu mkuu UWT Ndugu Jokate Mwegelo akimuombea kura ya Urais mmoja wa "wanaosemekana" kutaka kugombea Urais 2025, kada huyo amesema hayo akiwa Mbinga Ruvuma, ingawa haijathibitika ametumwa aseme, au amejituma mwenyewe!

Tupe majibu stahiki ndugu mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi!!

Na ikiwa jambo hili halijaruhusiwa, jitutumue Uipe ONYO au karipio Kali CCM!!

Ni hayo tu.

Chanzo: Ayo Tv.
 
Maisha ya kila siku ni siasa, kwa hiyo kila siku unapoishi, ni kampeni, ukisifia Barbara, maji, au ukikosoa, tayari ni kampeni
 
Maisha ya kila siku ni siasa, kwa hiyo kila siku unapoishi, ni kampeni, ukisifia Barbara, maji, au ukikosoa, tayari ni kampeni
Ndo kumuombea kura mapema hivi?

Unawezaje kumuombea kura mtu ambaye chama chake hakijampitisha na Tume ya Uchaguzi haijapuliza kipenga?
 
Amesikika Ndugu Jokate Mwegelo akimuombea mmoja wa wanaosemekana kutaka kugombea Urais 2025,

Tupe majibu stahiki ndugu mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi!!

Na ikiwa jambo hili halijaruhusiwa, jitutumue Uipe ONYO au karipio CCM!!

Ni hayo tu.
Wala usijali huyo Jokate yupo Kwa kazi maalum!

We hujui mgombea anapopiga kampeni mapema nachuja mapema!!?

Bora mtaka kiti angefanya 50/50 ingemsaidia lakini kuwaaminisha wtu mapema hivi ni kujiumiza na kujimaliza kisiasa!!

Wapiga domo Wote wa urais wa huyu mama ni Anti-samiah wote !

Source-trust me Brooo!
 
Ndio shida ya CCM wao siku zote wanawaza CHAGUZI ila MATATiZO ya wananchi kama
1.Mgao mkali wa UMEME
2.Ukosefu wa Maji licha ya kuwa na vyanzo lukuki vya MAJI
3.Huduma duni kabisa za Usafiri jijini Dar
4.Migogoro ya kila siku kati ya Wakulima na Wafugaji ,..HAYAWAHUSU ila kutwa ni kuwaza KUPORA chaguzi..
Hawa watu pasipo watz kuamka,TUMEKWISHA
 
Ndo kumuombea kura mapema hivi?

Unawezaje kumuombea kura mtu ambaye chama chake hakijampitisha na Tume ya Uchaguzi haijapuliza kipenga?
Sasa hakuna uchaguzi, chama chako na mgombea wako wameathirika?
 
Back
Top Bottom