Halo dadangu
Dinazarde. Hujambo? Ninayoandika hapa yalistahili yawekwe kwenye PM
lakini wewe hukuchagua hivyo; ulikuwa na sababu nilizozielewa!
Napenda kukupongeza kwa kuwa mdau mzuri sana kwenye jukwaa hili kwa michango moto moto ya jokes
unayotoa hapa kuanzia 2/4 mpaka sasa na hasa siku ya 7/5/2014. Jokes zako zilinifurahisha sana mimi na hata wadau wengine kulingana na ma-likes mengi uliyorushiwa. Moja ya jokes zako niliyoipenda sana ni ile ya: "Mambo ya Uswazi".Pamoja na kuipenda sana hii joke, nililalamika kwamba ulipunguza ladha yake kwa kuweka conclusion kwenye joke yenye maneno: "Baba Kidawa hooii" Maneno haya yanamnyima msoma joke kufikiria anachokitaka.
Kwa mawazo yangu, joke haitakiwi kuwa na conclusion au ufafanuzi wa aina yoyote. Joke nzuri ni ile inayomwacha msomaji huru ku-imagine hatma ya matukio kwenye joke. Tazama jokes hizi za wenzetu
KUHUSU WATOTO. Ni maelezo tu hakuna conclusion au summary yoyote yet jokes ni powerful sana.
Maoni yangu mengine kuhusu joke ni kwamba joke hitakiwi kukejeli au kuzungumzia maumbile ya watu. Joke ya namna hiyo inawafanya watu kuudhika. Hapa jukwaani kwa mfano zimetokea jokes kuhusu sura za Mh. Mizengo Peter Pinda na Stephen Wassira. Sikuona likes zikitolewa kwenye jokes za aina hii. Kwa hiyo tuache kutoa jokes zinazokebehi sura au maumbile ya watu!
Kwa hiyo dada Dinazarde naomba niishie hapo kwa leo. Kama utakuwa na lolote weka kwenye comment ya thread hii.
Nakutakia kazi njema.
shieka.