Kwako Balozi Dkt. Wilbroad Peter Slaa

Haya yote Magufuli anayashughulikia.
Ufisadi wa Magofuli hata wahi kulingana na ufisadi wa Lowasa.

Na ndiyo maana alisema nafuu huyu kuliko yule.
Mchawi mpe mtoto amlee,bado aliyoyasema ya naishi na kufanyiwa kazi...
Katika nafasi yake leo...na Amini anafanya mambo mengi...yeye si muamuzi....
Hivyo kijana tulia uone mambo yakishughulikiwa
 
Badala wahangaike na hali ya sasa ya chama wanaanza kumchokonoa mzee wa watu. Akijibu mtapoteana muanze kulalamika tena. Endeleeni kumchokonoa .....
 
Alikua padri akaacha,akaoa mke akaacha akaoa tena. Alikua CCM akatoka,akaenda CHADEMA akatoka. Aliwapinga mafisadi sasa anawakumbatia. Hauhitaji akili nyingi kujua huyu ni mtu wa aina gani.

Yes,huyu ni mtu mwenye msimamo.ambaye wakati wote hujitenga na wenye mizaha.Bravo
 
Mwacheni mzee wa watu ale kuku kwa siku hizi za mwisho?

Wa TZ hambebeki mzee alihangaika sana kwenye maandamano alikuwa anasimama front! Mkewe aliwahi kupigwa hadi damu!!!
Hambebeki juzi mlitakiwa kundamana mkajifungia vyumbani na wake zenu!!

Pambaneni na hali zenu! Ndio kaamua hivyo DR Slaa. Hivi karibuni jiwe anataka hapa ndani hata jina lako ulitaje wazi....siyo maha.. nini sijui!!
 
Kama kuna kauli ilinishangaza kutoka kwa daktali slaa basi nikuutangazia uma eti alikua akishindia mihogo,huku kwa mwezi alikua akitia m7 kibindoni.
 
Kwako; Balozi Dr; Wilbroad Peter Slaa,
Natambua "URAIS" ndio msingi mkuu wa mgogoro wako na Lowassa/CHADEMA na sio 'tanabahi' nyingine ..

Mzee wangu Dr Wilbroad Peter Slaa, ninatumia haki yangu ya kimsingi ya kikatiba inayopatikana kwenye Katiba yetu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Article 18(a) "every person has a freedom of opinion and expression of his ideas". And now, Dr Slaa, Let Chip Fall Where They May. To allow events to unfold naturally; to accept what occurs without prejudice, worry, or regret regardless of the consequences and no matter what happens. I'm going to tell you the truth; Tujadili hili.

MWEMBEYANGA; Tuanze hapa, September 15, 2007 Mwembeyanga, ORODHA YA MAFISADI (LIST OF SHAME) wakati wewe (Dr, Wilbroad Peter Slaa) ukiwaongoza wanasiasa wenzako wa upinzani kuisoma orodha ya Mafisadi. Kanuni na vigezo ambavyo waraka ule ulitumika kutaja ni sambamba na (a) USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI na (b) USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI.

Katika orodha ya mwaka 2007, Dk. Slaa uliwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), ambaye sasa ni marehemu, Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM) na Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM). Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, kada wa CCM, Nazir Karamagi, Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM), Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na Rais Jakaya Kikwete..

Dr Slaa, unakumbuka katika mkutano wako wa Tabora April 2011 uliongeza majina mengine na kusema "tuongeze kwenye orodha ya Mafisadi".. Unakumbuka? Nafikiri umesahau, nikusaidie kukumbuka; Kwa mujibu wa magazeti ya Tanzania Daima na Mtanzania, waliotajwa katika orodha hiyo mpya ni: Waziri wa Ujenzi wakati huo, Dk. John Magufuli na John Samwel Malecela, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Philip Mangula.. Umesahau?

Sasa kama katika orodha yako ya 2007 baada ya miaka 4 ukatuongezea na "MAGUFULI" kwenye orodha yako, halafu leo unafanya nae kazi hadharani, tena ukimuita "mheshimiwa Rais" kwanini uone hatari wengine kufanya kazi na wengine ambao wewe uliwataja kwenye orodha yako ya 2007? Kwamba wewe ndie pekee ambae unaamua nani ni "SAFI" na yupi anapaswa kupuuzwa kwa sababu ni mchafu?

Aliyeondoka CCM kwenda upinzani kati yao hao ambao walitajwa katika orodha hiyo ya 2007 ni Edward Lowassa pekee, wengine wote (ukimuondoa Daudi Balali) bado CCM na umeamua kujiunga nao. Tena ukiwa sehemu ya watu ambao ni marafiki zako. Watu ambao ulituaminisha miaka 11 iliyopita kwamba ni "MAFISADI" leo wewe unaishi nao nyumba moja.. Kwanini tusikufikirie tofauti na mtazamo wako katika hili?

Unakumbuka kauli ya aliyekuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM wakati huo, Nape Nnauye April 2011 akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Zanzibar alisema, “...yaliyosemwa Tabora na Dk. Slaa, ni hila za hao hao wenye shutuma za ufisadi lakini sisi tumejipanga vizuri wasijidanganye kuwa tutarudi nyuma, tutahakikisha chama kinakuwa safi na wenye shutuma wakafanye shughuli nyingine.” UNAKUMBUKA? Au utakuwa umesahau maana ni miaka takribani saba sasa tangu umtaje "MAGUFULI" kwenye orodha ya pili ya 'Mafisadi'

Narejea maneno yangu ya January 18, 2016 saa 7:42pm "Tunapozungumzia utendaji wa kichama na management Dr Wilbroad Peter Slaa atabaki kuwa imara. Tunapozungumzia mgombea urais kulingana na hali ya kisiasa ya 2015, Edward Lowassa alikuwa mtu sahihi kwa CHADEMA. Kama CHADEMA ingekwenda kwenye uchaguzi ikiwa na Dr slaa ingelikuwa uchochoro kwa Magufuli. Magufuli alikuwa mgombea mgumu sana kupambana nae. Lowassa alikuwa mgombea sahihi na mpinzani wa dhahiri wa Dr Magufuli.."

Dr. Slaa, unakumbuka 15.07.2014 ukiwa makao makuu ya chama, Ufipa ukiwa na nyaraka za siri (confidential) ukisema kwamba "Nina barua ya AG wakati wa kuhamisha Hela.Barua inasema "This letter is instructive). Barua nyingi zimeandikwa na pia IPTL imeandika tarehe 5.9.2013 kuwa hela zisitolewe bado kuna utata".. Dr, Slaa unakumbuka hili? Sasa kwanini hadi sasa haujamuuliza Magufuli ni kwa sababu gani hadi sasa 'Attorney General' aliyetajwa hapo hajatiwa nguvuni? Kwanini umeungana na wao ambao uliwapa tuhuma awali na 'umepiga kimya' na umepoa kabisa na kuwa mpiga makofi wa Magufuli?

Dr, Slaa unakumbuka wakati ule unatueleza mbele ya waandishi wa habari kuhusu mamlaka ya watu kuporwa na Rais? Ibara ya 8 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inayoweka wazi kuwa wananchi ndio msingi wa mamlaka yote (Sovereignty of People) imefutwa na nani? Rais anajiweka juu ya mamlaka yote ya wananchi? Haujui hilo? Sasa Rais ni 'mfalme'. Ndie anaamua hata mengine nje ya matakwa ya bunge. Lakini 'umepiga kimya' kabisa Daktari wangu, umesahau hayo?

Dr, Slaa unakumbuka Julai 2014 wakati ukitueleza kwamba "Tumeingia gharama na ukweli umewekwa hadharani. Sasa tupo tayari kupigwa risasi kwa kuuusema ukweli."... Leo upo kimya wakati watanzania wakiuwawa kwenye mikono ya polisi, wanasiasa wakipigwa risasi mchana kweupee, na upo kimya, haukemei, na hauoni kama ni shida, hayo ndio ulikuwa ukihubiri Nyakati zile? Kwamba tukae kimya tuliona unyanyasaji kwa raia? Hata kuondoa uhai wao?

Dr, Slaa Sitaki kuongelea madai yako ya maaskofu kuhongwa; maana baraza la maaskofu lilikanusha na kukutaka wewe (Slaa) uoneshe na kupeleka ushahidi TEC, ushahidi na kuwataja wahusika hao ili wachukuliwe hatua za kinidhamu na haujafanya hivyo.. Unataka niendelee kuamini 'utumishi' wako? Tuhuma umetoa 2015 na leo 2018 haujawahi kuthibitisha popote.. Wewe ni Padre, kumbuka.

Dr, Slaa wanachama wa CHADEMA na wafuasi wa UKAWA wanatambua 'chanzo cha mbio zako', suala la msingi ni urais! Mazungumzo ya awali ni wewe kutaka CHADEMA na UKAWA wakusimamishe kuwa mgombea wao, swali linakuja, nani kati ya SLAA na LOWASSA anaweza kupambana na CCM na mgombea wao, John Pombe Magufuli? Wakachagua LOWASSA walio wengi. Wewe ukitaka kumtumia Lowassa kukuombea kura jukwaani, endapo ungepitishwa kuwa mgombea.

Dr, Slaa unahoji kuhusu 'uzalendo ndani ya CHADEMA' nafikiri hapa kuna kila sababu ya kwanini usijitazame mara mbili, unakumbuka kiwango cha mshahara wako wakati ukiwa 'katibu mkuu wa CHADEMA'? sio chini ya milioni saba za kitanzania, bila Makato. Pesa zikitoka kwenye mapato ya chama na Makato ya mishahara ya wabunge na wakurugenzi ili ulipwe wewe. Madai yako, usingeliombwa kugombea urais 2010 ungelishinda ubunge Karatu. Uzalendo wako tunaupima kwa tafsiri ipi hapa?

Dr, Slaa mwaka 2008 ulikuwa bungeni kama mbunge wa Karatu (CDM) na ulijadili taarifa ya kamati tuele ya bunge kuhusu RICHMOND. UNAKIRI kwamba 'Ufisadi ilikuwa ajenda iliyowapa umaarufu CHADEMA, leo wamewachukua.' sasa tujiulize, kwanini umeamua kuunganisha nguvu na wengi ambao ni sehemu ya RICHMOND ukimuondoa LOWASSA pekee am car yupo CHADEMA? tuamini sasa una matatizo binafsi na Lowassa lakini sio CCM na ufisadi wa RICHMOND?

Dr, Slaa ukiwa Serena Hotel ulitueleza kwamba "uliamua kuachana na siasa, tarehe 28 Julai 2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona yanayofanyika ndani ya chama chako hayamridhishi" sawa, kwanini unafikiri yalikuwa hayaridhishi wakati umeshiriki hatua zote za kumleta Edward Lowassa kwenye vikao vya kamati kuu, ukiwa wewe ndie katibu mkuu wa chama? Nini kilisukuma kung'atuka? Wivu? Maslahi? Au kugeuzwa chapati?

Dr, Slaa nakumbuka moja kati ya kauli yako kutoka pale Serena ulisema "Ni afadhali sifa yake iharibike kuliko kusema uongo. Ni heri kupotea kwenye siasa za dunia kuliko kusimamia uongo!" sasa kwanini sasa unashindwa kuishi ukweli kuhusu hali ya nchi yetu kisiasa ilivyo? Hausemi lolote kuhusu kusiginwa kwa sheria ya vyama vya siasa (1992)na kanuni zake za Maadili (2007). Ukweli gani ulituaminisha unaupigania? Ikiwa wanasiasa wanazuiwa kufanya siasa wakati wanapokea ruzuku, tena vyama vyao vina usajili wa kudumu?

Dr, Slaa tangu umeamua kuachana na siasa za majukwaani, na kuamua kuwa 'mfuasi mahiri' wa Magufuli na serikali yake (kabla ya kuteuliwa kuwa balozi) ni lini umewahi kusema lolote kuhusu UFISADI wowote ndani ya nchi hii? Hata ufisadi wa zamani ambao unapaswa kufanyiwa kazi na serikali hii. Kuna upotevu wa zaidi ya trilioni moja na nusu, kwenye bajeti ya 2016/17, Dr, Slaa umesema lolote kuhusu hilo, popote, au taarifa ya CAG haijakufikia? Au umeamua kuwa upande wa 'DOLA' na kusahau maneno yako kwamba wewe ni 'mzalendo'?

Dr, Slaa unasema na kutuaminisha watanzania kwamba LOWASSA hapaswi kuaminiwa kwa sababu tu ya hisia zako, na hata tuhuma za RICHMOND ambazo hadi sasa mahakamani hazipo.. Kwanini watanzania wasiamini kwamba, wewe unaendeshwa na chuki zako dhidi ya Lowassa katika "urais" na sio vinginevyo? Kama ni tuhuma, kwanini haukutaka watu wamkatae aliyekuwa Mgombea wa CCM? Ambae alikuwa na tuhuma kadhaa ikiwepo ya kututia hasara kwenye 'ukamataji meli ya samaki ya TAWALIQ 1, achilia mbali mkataba wa KONOIKE.

Dr, Slaa ulishindwa kutueleza kwa 'kina' endapo LOWASSA angelikuja na hao wabunge 50 na wenyeviti aliowataka yeye basi SLAA ungeendelea kuwa ndani ya CHADEMA kwa kuwa tu LOWASSA katimiza vigezo alivyovitaka yeye? ambavyo anasema ni sehemu ya masharti yako?

Suala la aidha LOWASSA ni mzigo (liability) au mtaji (asset) halikujibiwa hadi siku ya mkutano tajwa (kwa mujibu wako). Maana ulitaka kufahamu anapokuja (Lowassa) anakuja na akina nani, ni wafuasi wa aina gani; vijana wa bodaboda, vijana wasio na ajira au watu waliosombwa tu, au wanakuja kwenye mapambano?

Jibu ambalo Slaa anadai alipewa lilikuwa ni kuwa "tungepata wabunge 50 na wenyeviti wa CCM mkoa wasiopungua 22, wenyeviti wa CCM wilaya 88." Na Dr, Slaa ulisema na kukiri kuwa "kama ni hivyo kutakuwa na tetemeko (la kisiasa)." sasa kwanini nisiulize hili swali; kumbe tatizo sio uchafu wa Lowassa? Tatizo ni anakuja na watu gani kukupigania wewe katika "urais"?

Je, LOWASSA angeingia CDM na kutopewa (asiteuliwe) nafasi ya kugombea Urais na Slaa (kama unavyoamini wewe ni bora kuliko Lowassa) ukapewa nafasi hiyo ya kugombea urais, ungeyasema yale uliyoyasema pale Serena?? Au shida ni "urais" kama alivyojisemea Tundu Lissu?? Na sio tuhuma zingine ambazo ulijaribu kumtupia Lowassa alipokubaliwa kujiunga CHADEMA na kuwa mgombea wao?

Dr Slaa, unasema kwamba wewe mwenyewe kuwa uliandika barua ya kujiuzulu (katibu mkuu-CDM) tangu mwezi Julai mwaka (2015) lakini kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu ni kwamba Dr Slaa ulipokea mshahara wa mwezi wa 7 na 8 na pia kuendelea kutumia nyumba na gari za chama. Kww wakati huo. Nani mkweli hapo?

Dr, Slaa hadi sasa, haujatueleza gharama za kuendesha mkutano wako Serena Hotel na kurusha matangazo yako kwa Radio na Tv kwa saa 3 mfululizo ambazo ni zaidi ya shilingi halali za kitanzania milioni 225 ulitoa wapi, nani alikuwa nyuma ya ufadhili wako, ikiwa ulitueleza kwamba "Nyumbani kwako unashindia MIHOGO".. tueleze hayo hata leo..

Dr, Slaa haujatueleza ni hatua ipi ulichukua baada ya kuikataa ile rushwaa ya milioni 400 (ambayo ulitueleza Serena Hotel) mwaka 2008 na pia hatua ipi uliichukua na kuifuata baada ya kupewa saa 5 [ukimtaja Rostam] za kutubu dhambi zako kabla haujauwawa... Yote ni matukio ya 'kusadikika' ikiwa hadi sasa haujatuonesha nanma sahihi ulivyoshugulika nayo..

Dr, Slaa alisema pale Serena "uchungu kuona chama alichokijenga (CHADEMA), kikifikia hatua ya kusomba watu kwa mabasi na malori kisha mkasema mafuriko hayazuiliki! Hayuko tayari,... Anakataa kuwa ZEZETA!" LAKINI Dr, Slaa umejiunga na CCM ambayo katika uchaguzi mdogo Kinondoni, watu wamesombwa kutoka maeneo kadhaa, kujaza mikutano ya hadhara ya kampeni, umekubali kuwa "ZEZETA" huko ulipo sasa?

Dr Slaa, ulisema wewe sio muumini wa mifumo kandamizi ya rushwa na hongo. Madiwani wananunuliwa 'upo kimya' tena kwa rushwa za wazi na dhahiri. Ushahidi unapatikana wa video, TAKUKURU wanasema 'sio ushahidi' Bali ni 'taarifa', wewe muumini wa haki umetulia kimya? Wananchi wanaporwa haki yao na kurejeshwa kwenye chaguzi za lazima. Mnyeti anakiri na kusema wazi kwamba 'hata mbunge wa Arumeru Mashariki akipenda, anafikishiwa bei', umetulia kimya.. Kama hauoni.

Dr, Slaa unasema wewe ni muumini wa haki za binadamu, utawala bora wa sheria. Kwanini kama ndivyo hadi sasa haukuwahi kuwakemea askari ambao waliondoa maisha ya Akwilina Akwilini akiwa kwenye safari zake? Muuaji hayupo na jalada limefungwa. Ben Saanane hayupo (mwaka wa pili sasa), Mkuu wa Mkoa wa DSM anavamia kituo cha TV na bunduki (kushinikiza masuala yake yafanyike) na haujawahi kukemea kwa maneno au mdomo popote.

Dr Slaa unasema 'waliopokelewa na CHADEMA 2015 ni MAKAPI'.. Sawa, ni vyema na wewe ukaitwa "MAKAPI" kutokana na kukataliwa na chama chako mwaka 1995? au 2015 (wakati CHADEMA wakiamua kumpa nafasi ya kugombea 'urais' Lowassa na sio wewe?) Au MAKAPI ni kutoka CCM kwenda CHADEMA pekee? Kama wewe ulipokelewa CHADEMA 1995, kwanini ushangae wengine kupokelewa 2015? Au tatizo ni lile-lile, "urais"?

Dr Slaa, ulisema "una ushahidi wenye vielelezo kuhusu ushiriki wa Lowassa kwenye RICHMOND, tofauti na na maneno ya Scotland yard" Sasa kwanini hadi sasa tangu 2008 hadi sasa 2018 (miaka 10 baadae) sijaona ukaifungua kesi kumshtaki Lowassa? Kuna mashtaka yenye kuendeshwa na mtu binafsi 'private prosecution' ambayo unaweza idhini kwa DPP.. unasubiri nini Dr Slaa?

Dr Slaa, ulisema "Hatuwezi kujenga maadili tukiwa na watu wachafu," kumbe uchafu kwako ni "LOWASSA" na sio wale wengine wenye kuhusishwa na EPA, ESCROW, KAGODA, MEREMETA? Kwako tafsiri ya uchafu ni 'LOWASSA' lakini sio mwingine yoyote ambae anatajwa kwenye shughuli za ufisadi katika nchi hii? Umeungana nao leo. Hapo ndio nakuona una 'chuki' ya dhahiri.

[HASHTAG]#MMM[/HASHTAG], Martin Maranja Masese
Mwacheni Dr Slaa atuwakilishe huko Sweden!
 
Jamani kumtunza Josephine ni shughuli ya gharama kubwa
Huyu mzee afanyeje zaidi ya kunywa matapishi yake

Kazi mnayo....Ngoja amtunze vizuri baby wake...lingine?
 

Attachments

  • 20180308_095845.jpg
    20180308_095845.jpg
    148.9 KB · Views: 23
Mh Balozi ni vema ukajitokeza kujibu maswali haya ili wanaCCM wenzio wakuamini .
 
Tangu mchakato wa KATIBA MPYA uliposhindwa ndio nikatambua kama nchi hatutaweza kufanikisha jambo lolote la maana hadi pale kizazi cha uhuru kitakapofutika kwenye uso wa dunia.

Kwenye mkwamo kama huu ni wanafunzi wa vyuo vikuu ndiyo wanakuwa "conscience of the nation". Ndivyo ilivyokuwa Kenya wakati wakijadili vipengele muhimu vya katiba yao mpya. Sasa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania sijui wamekengeukaje? Do they only live for themselves? But that would be contrary to their youthful nature!
 
Mbona mnahangaika sana na Dr. Slaa nyie mlishaamua kumbeba huyo mtu wenu na Dr alishaamua kuwaachia chama chenu mmemuita kila jina, yeye ameendelea na utaratibu wake wa maisha kabla ya kumlaumu tuelezeni sisi kwanini mtu mliyemtangaza fisadi ndiye mlimpa nafasi ya kugombea urais?
 
Povu loote kumtetea Lowasa na kushinikiza Slaa aonekane anamakosa, cdm bwana wanasiasa za matope!
 
Back
Top Bottom