Kwakheri Rafiki yangu kipenzi.

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Nakuandikia haya kukupa mkono wa kwakheri Rafiki yangu, nimeishi nawe kwa muda mwingi sana.
Siku ya kwanza ulipo kuja kwenye maisha yangu nilijua nimepata Rafiki bora kabisa, lakini kumbe nilijidanganya japo pia nitakushuru kwa yale mema machache ulio yafanya kwaajili yangu ambayo kwa kiasi fulani yamenipa mafanikio.

Moyoni nina malalamiko mengi kwako japo sikuombei mabaya huko uendako. Ila nikiyakumbuka haya machache naumia sana.

1; ni kwa sababu yako nimepoteza ndugu zangu niwapendao kwa kushindwa kugharamia matibabu yao. Wengine walikufa kwa dhiki masikini.

2; kwasababu yako ukanifanya nikashindwa kujiamini hata kile kidogo nilicho kipata nilikitumia vibaya

3; ukanifanya hadi leo niishi mwenyewe bila mwenza japo natamani sana lakini wewe ulinifanya nisijiami

4; Nina mengi ya kusema lakini kwa kifupi tu kwamba maisha yangu hayakuwa na furaha kwa kipindi chote ulichokuwa nami,
Sesimi kuwa ulileta laana hapana ila mikosi ilizidi kuwa mingi.

Mwisho niseme tu nenda salama nami nafungua ukurasa mpya wa maisha yangu
Nitazikumbuka nyakati chache nilizofurahi nikiwa nawe.

KWAKHERI RAFIKI YANGU 2019
NA SASA NAKUKARIBISHA 2020.
Si Mimi tu ila na wana JF wote tunakupa mkono wa kwakheri.

Happy New year JF Mungu ajaalie tufike salama.

Yale machungu na mateso ya 2019 tuyaache yaende, tuwe na mwanzo mpya kile ulichodhani hakiwezekani hebu nenda ujaribu kukifanya.
Lakini usisahau kusamehe wale walio kuumiza ili ukaanze upya bila mzigo moyoni mwako.
Bahati na iwe upande wako.
 
Nzuri mno! Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom