Mhh jamani hivi kila mtu kama angekimbia nani angetuletea uhuru katika bara hili la Africa??!!!. Hakuna mtu yoyote kutoka dunia nyingine atakuja kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania, bali sisi wenyewe. Watanzania kwa pamoja tukiendelea kuelimishana, kupinga mabaya, kusifia yaliyo mazuri, kufanya kazi kwa bidii na kujituma na mengine mengi, mimi naamini kabisa iko siku tutafika tuuuu.
Of course njia ya mkato ya kufika mapema ni kumpata kiongozi aliye msafiiii, atakayekubali na mwenye ubavu wa kuwaface hawa mafisadi. Ukikutwa na hatia za wizi kama hizi basi WAPIGWE RISASI WAFE, WANYONGWE KAMA VILE INAVYOFANYIKA HUKO CHINA. Wakipigwa risasi watu kama 100 hivi nawaambieni viongozi watashika ADABU, hakutakuwa na wizi mbaya kama tulio nao sasa. Viongozi lazima wajuwe kuwa wanapochukuwa form za uongozi wanaipenda nchi yao na wanataka kuitumikia, ni sawa na kuwa padre, au sister kanisani (RC).
Kama mtu hawezi kuwatumikia watanzania kwa hicho kipato kidogo anacholipwa aache asiende huko, akatafute kazi kwenye makampuni ya SIMU, MATANGAZO, BIA, SIGARA, nakadhalika. Aiache na atuache watanzania salama salimini. Viongozi wasiingie kwenye kazi za siasa wakitegemea kutengeneza PESA KWA NJIA ZA WIZI wa aina mbalimbali.
Ndugu Ngida1 karibu tena ulingoni, kukimbia matatizo siyo kutatuwa matatizo. Ukiyakimbia matatizo ya nchi yako, unategemea nani ayatatuwe??? haya ni ya kwetu wote mimi na wewe, sisi na wewe, tusichoke mpaka kieleweke.
Aluta kontinua mapambano yanaendelea. Pamoja tutaweza.