Ngida1
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 586
- 206
Ndugu Wana_Forum,
Hapo nyuma kuna mwana-Forum mmoja ambae alisema kuwa anataka kuihama nchi kutokana na kero za siasa zetu za CCM zisizo na mipango ambazo zinamdhalilisha mwananchi kuwa maskini kila siku. Mimi kwa mchezo nilikuwa wa mwanzo kumcheka kwenye hio thread yake. Leo, nami ninataka kuihama sio nchi bali hii Forum kwasabau naona afya yangu itaathrika kutokana na siasa mbovu za hii nchi yetu chini ya CCM.
Leo kwa mara ya mwanzo niliona ile picha ya wanafunzi wa Mbagala wakisoma shule nje kwenye mchanga bila ya madeski na machozi yalinioka - yalinitoka machozi nikukumba 540,000 Sterling Pounds alizokutwa nazo Chenge na mabilioni ambayo akina Rostam wanazo. Baada ya kuiona hii picha nikaona bora nitoke kwenye hii Forum, kwani kila siku naona habari ninazozipata zinanitia uchungu kiasi ambacho afya yangu inaathirika, kutokana na pressure yangu bure bure kupanda. Kwahivyo, nimeamua bora kutoka kwenye hii Forum kabla sijapata heart attack kutokana na stress ninyoipata kutokana na news ninazozisoma hapa kwenye hii Forum. Sitaki tena kusoma habari zozote zile za hii nchi yangu kwani kila mara ninaposoma naona maisha yangu yanakuwa hatarini.
Kwahivyo, kwa wale marafiki zangu wa hapa kwenye hii Forum na wale watani wangu akina Lampart na wengine ninawaeleze kuwa mimi hawatoniona tena na yule ambae atataka kuniona basi awasiliane na mimi kwenye hii private email address yangu:
<ngida1@hotmail.com>
Nimeona bora nitokane na hii Forum kwasababu kila siku presssure yangu inapanda. Kwa yoyote atakaewasiliana na mimi kwenye private address yangu basi tafadhali asinieleze chochote kuhusu maendeleo ya siasa ya hii nchi. Labda mtu ataweza kunielezea bei mpya ya bia, massage parlours mpya zilizofunguliwa, etc etc etc
Kuhusu siasa sitaki kusikia chochote kutoka mtu yoyote yule. Sitaki kusikia kabisa habari kama vile watu wametembelea shamba la mifugo la Raisi huko Bagamoyo, kwasababu sifahamu kwanini Rais atakuwa kwenye Miradi kama hio. Kama 5 million kwa mwezi hazimtoshi basi ni kusema mtu na State itamuengezea. Kila mtu anafahamu kuwa ukiwa mwenye Miradi basi ni lazima upoteze 60% ya time yako huko kwenye Miradi yako japokuwa unao wafanyakazi 1000. Sijui kama Raisi mwenye Miradi anapata wakati wa kushughulikia kero za wananchi. Labada pengine hata hajui kama wanafunzi kule Mbagala wanakaa chini bila ya madeski!
Anyway, wale niliowakera hapa kwenye hii Forum kama akina ndugu yangu Mzee Bubu Ataka Kusema na akina Nd. Lampart ninawaomba samahani sana na wale tutakaoendelea kuwasilian basi wajue kuwa there will be no politics in our discussions. Sitaki kupata heart attack at this young age.
Kila la kheri / Ngida1