Dear Ndugu: Ganesh, Lampart, Kichuguu, Mndundu, Gudboy, Bubu Ataka Kusema, Mzee Mwanakijiji, Buchanan, Firstlady1, Nguli, Ziondaughter, Bluray, MTM, Josh Michael, Mtoto, Chrispin, Geoff, eRRy84, Omumura, Kweli, Ngambo Ngali, Kobe, Son of Alaska, Kidatu, MzeePunch, Ndahani, Tripo9, Nicko, Mchili, ChaMtuMavi, Maane, kelly01, Dark City, Sugar wa Ukweli, BabaJ, Sonara, Sipo, Mchukia Fisadi, Richard pamoja na wote mlioniletea PMs,
Samahanini sana kwa kimya changu, kwani nilikuwa ninazitilia maanani zile advices mlizonipa kwenye comments zenu. Nimesoma kila comment zaidi ya mara 3.
Nimefarajika sana na msgs zenu. Nimeshindwa kumjibu kila mmoja wenu kwasababu msgs zilikuwa ni nyingi. Nimepokea comments 44 pamoja na private emails 67. Kwa kweli sikutegemea hata kidogo kama mtakuwa-touched na ule ujumbe wangu kama mlivyoonesha. Pia, ule ujumbe wangu ulisomwa na wana_Forum zaidi ya 818 mpaka wakati huu ninapokuandikieni huu ujumbe.
Ninakushukuruni nyote sana sana for your comments and advices, kuanzia Bubu Ataka Kusema ambae ilibidi sio atake kusema tu bali safari hii alisema kabisa na nyote wengine..
Nd. eRRY84, beats zako zilikuwa nzuri sana na ndizo zinazonifanya niishi mpaka leo. The beats make me feel like crying with deep emotions!
Firstlady1 na Sugar Wa Kweli, sijui kama ndio nyinyi wamoja au vipi, lakini ninakushukuruni pia for being so touched!
Kwa ujumla, ninakushukuruni nyote kwa advices zenu.
Kabla sijachukua uamuzi wangu wa mwisho kutokana na ushauri wenu mlionipa, ninaona bora kwanza nilipe kodi ya chumba ninachokaa ili huko mbele nisije kuelezwa kuwa nimehama nyumba bila ya kulipa kodi.
Kwahivyo, landlord wangu Nd. Maxence Melo Mubyazi, ninakuomba at any time baada ya kuisoma hii msg uende any branch ya Western Union hapa DSM kuchukua kodi ya chumba ninachokaa ya Dollar 110 (equivalent to TShs 150,824.80). Kama utapata matatizo huko Western Union, tafadhali wasiliana na mimi.
Nimeengeza makusudi Dollar 10 kwasababu nipate kumpita Bubu, ili BUBU ATAKE KUSEMA kwani namjua yeye anapenda kushindana katika mambo mazuri..
In fact, Nd. Melo, tayari nishakuletea details kuhusu haya malipo kwa email tokea jana. Soma kwanza email msg yako kabla hujaenda huko Western Union, kwasababu watakuuliza masuala fulani fulani utakapokuenda.
Nd. Wana_Forum, ninakutakieni kila la kheri katika haya mapigano yetu against UFISADI katika nchi yetu na kwa mara nyengine ninakushukuruni tena na tena kwa comments zenu na advices zenu mlizonipa.
Kama kuna mmoja wetu ambae ataweza kumueleza Bwana Chenge aturejeshee vile vijisenti vyetu vya commission ya Radar alivyotunyanganya itakuwa ni vizuri sana ili tupate kuwajengea shule ya kisasa wale watoto wetu wa Mbagala.
Kila la kheri.
Ndugu yenu / Ngida Wa Ngida (Ngida1)