Kwaheri Ukoloni- Kwaheri Uhuru...Dk. Harith Ghassany

Kwaheri Ukoloni- Kwaheri Uhuru...Dk. Harith Ghassany

Kiganyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
1,242
Reaction score
765

Dk. Harith Ghassany ni mwandishi wa kitabu kinachoongelewa Tanzania nzima sasa hivi na huenda kikavuka mipaka na kuingia nchi nane zinazopakana na Jamhuri ya Muungano.
Kitabu hiki chenye kurasa 500, kinazungumzia namna gani Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalipikwa Dar es Salaam, Algeria na mashamba ya mkonge ya Tanga na kupakuliwa Zanzibar.


Kwanini uliamua kuandika Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru?
Nataka ifahamike kuwa mimi binafsi nina damu ya Kiarabu na ya Kiafrika. Nia yangu kukiandika kitabu ni kuziondowa fitina za upotoshaji wa historia ili uhusiano mkongwe baina ya Wazanzibari waliochanganya damu, baina ya Wazanzibari na Watanganyika (Watanzania), na baina ya Waafrika na Waarabu, upate kuendelea kutitirika na kuimarika kwa maslahi ya kujenga amani na neema kwa faida ya walio wengi na vizazi vya baadae vya pande zote.
Kusamehe kwenye udhaifu ni kuakhirisha uadilifu. Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru hakikuja kupigana au kuwapigania wenye kutaka kuviendeleza vita vya jana na vya juzi, bali kimekuja kuleta suluhu na amani katika Zanzibar na Tanzania.
CHANZO: http://kitoto.wordpress.com

Nauliza Wakuu,
Kuna aliyesoma kitabu hiki??

Je dhima hasa ni ipi?

Ni suluhu gani anayozungumzia Dr Ghassany??

Naomba Mwongozo kwa GT wote mliobahatika kukisoma na mliokuwepo enzi za mapinduzi au mlioisoma vema historia ya Tanganyika na Zanzibar!

Kiganyi, JF.
Mwanzo - wotepamoja.com



[TD="align: center"]
[/TD]
 
Back
Top Bottom