Kwaheri Lowassa, kwaheri CHADEMA...

Kwaheri Lowassa, kwaheri CHADEMA...

Kusema kweli lowasa amewavunja moyo wanamabadiliko wote sio UKAWA tu hadi wa vyama vingine

Wapumbavu na malofa tu hao, wanataka kusikiliza bass ya muziki kwa kuweka spika juu ya mtungi (chungu) achana nao waache wapotee dii
 
Nianze kwa kukupa pole Lowassa,halafu nikuage.

Ulichokifanya Jana pale jangwani kimedhihirisha kabisa wewe ni msanii wa hali ya juu na bila shaka unaitendea haki taaluma yako ipasavyo, kwa hili nikupe hongera nadhani baada ya October 25 utajiunga na kina Ray na utasaidia tasnia ya filamu kufika mbali.

Lowassa umekosa sera umekuwa ukirudia yale yale kila kukicha.

Umati mkubwa uliookuwepo pale jangwani kwa siku ya jana ulikuja kusikiliza ilani ya UKAWA na walitaka kusikia kutoka mdomoni kwako ukahaidi utawafanyia nini, unasema unaleta mabadiliko,hicho ndicho walichotaka kusikia na si habari za babu seya, bilali na masheikh wa uhamsho.

Kuwaambia wananchi wakasome ilani kwenye website ni kuwakosea heshima na kutothamini muda wao. Ni wananchi wangapi wenye access ya internet?

Ndiyo wananchi tunataka mabadiliko lakini siyo mabadiliko ya kiini macho kama yako lowassa.

Hotuba yako imeshindwa kukidhi kabisa kiu ya wananchi, umekosa mipango umekuwa mtu wa kusemewa na wapambe wako,wewe ndiyo mtendaji tunataka useme wewe.

Chadema huu ndiyo mwisho wenu,baada ya uchaguzi tunawasahau kabisa kwenye ulingo wa siasa. Mmeamua kulamba matapishi yenu na kutaka kuwalazimisha watanzania walambe pamoja na nyie ila wengi tumejitambua tumevunja uaminifu wetu kwenu.

Kama Mbowe aliamua kuchenji gia hewani sisi tutachenji ardhini ifikapo October 25.

Siioni nafasi ya Lowassa na UKAWA baada ya uchaguzi.

Kwaheri Lowassa, kwa heri UKAWA.


Tumemuona, tumemsikia kilichobakia ni akili mu kichwa

Akili mu Kichwa.jpg
 
Mnataka rais wa mipasho au muimba taarab?kama mnataka rais wakweli ni lowassa lkn wakuongea ni ccm
 
Subiri sindano ikuingie wewe. Wasomi maprofesa wameona cha maana kutoka kwa Lowasa jana. Hotuba yake imelenga kila sekta na inatekelezeka. Sasa wewe aliekutuma kamwambie watanzania hawataki propaganda wanataka mabadiliko na mabafiliko ni kupitia kwa Lowasa.
Mnajisumbua tu ndugu zangu wana ccm...

yaani wewe unaonekana umekula matapishi mpaka HUJIELEWI hata kidogo.
 
Kama mitandao ipo watu walifata nini jangwani?..alafu usidhani kwamba kila mtu ana smartphone na pia usidhani kuwa kila mtu anaujuzi wa kuingia kwenye mitandao....napia kama unajua nini maana ya uzinduzi usingeshabikia hili jambo la kuwaambia watu wakaangalie kwenye net[quote}/

Asilimia kubwa ya target group la Lowasa walimuelewa aliposema watakuta vitu kwenye website ( Ninyi msioelewa endeleeni kusikiliza matatizo yaliyoshindikana ndani ya serikali ya ccmm kupitia mgombea wenu) Ziko smartphone za mpaka laki moja siku hizi lakini watu wa ccm mnaweza kabisa msijue zinapatikana wapi maana nyie hata mkiambiwa na ndg Magufuli kua mtapewa kila mmoja milioni akishinda mtaamini. Ambae hataweza mchakamchaka wa CDM wa mabadiliko kwa kwenda mbele kama wewe akae pembeni.
CHANGE IS MANDATORY THIS YEAR
 
Tumekuwa tukidanganywa na Maneno Mengi Majukwaani Mwisho wa Siku taifa lipo hapa tulipo. Hakuna Kubwabwaja Sana

Jukwaani, Matatizo ya Watanzania Hayawezi tatuliwa kwa Ilani ndefu na Maneno matamu bila vitendo.

Nadhani Lowassa Atakuwa Rais Bora Sana Kwa Personality aliyoioyesha na campaign za Kistaarabu, Bila Kumtukana Mtu

Wala Chama. Nadhani Lowassa Anaweza Kuliunganisha Taifa Hili.

.............
 
Hivi hakuna mengine yanayoweza kujadiliwa mpaka kila mtu anaanzisha thread hii?

Elekeza nguvu hizi kuanzisha post yenye kusambaza sera za chama chako na mgombea wako

Upuuzi na ulofa ulio tukua plus ametoa kituko cha mwaka! Watu wengine wana zeeka vibaya! Magufuli amesema atalala nao kitaratiiiiiibu!
 
Kweli kabisa, serikali ilimsomesha ni bora sasa akamalizie muda wake kwa kuwafundisha wasanii wetu, atakuwa amefanya jambo la maana sana.
 
Yaani watu wanaacha kazi zao na kwenda kujazana pale jangwani,wengine walikesha usku mmja kabla ya siku pale jangwani,wengine waliwahi majumbani kufungulia tv zao alafu unaongea kwa dakika kumi na sehemu kubwa ya ulichoongea ni vijembe then unatuambia sisi wote ni wasomi tukasome ilani yako mtandaoni....dah inasikitisha

ilikuuma eeeh !!! kwa hiyo ulitaka mpaste kama kawaida yenu.
 
We linamo kwel umezoea kudanganywa kama maisha bora kwa kila mtz nk. Ccm ina sera miaka 50 na bado inadanganya danganya tuu
 
Tatizo lenu ni nini hasa? It was very short but clear. Alisemea elimu, kilimo, afya, michezo, ajira na kuendelea etc. Sasa watu nadhani mushakariri kina Magufuli wanakuja kurap. Ilani ya cdm iko safi, ila tu humu kuna watu na viatu. Usikivu ni below zero

Hajasema chochote kuhusu ufisadi kwa hiyo hajajisafisha na ataendelea kutufisidi. Mwakyembe kasema serikali imeingizwa kwenye la dowans la bilioni 115 lililotokana na Richmond kashfa ambayo Lowasa aliisababisha. Dowans ni kampuni yake na Rostam! Tutamwaminije?
 
Hivi ni kweli Lowasa sio muongeaji au anafanya makusudi,mbona alipokuwa ccm,alikuwa anahutubia kwa mpangilio unaoeleweka?
 
Ngoja LOWASSA azunguke nchini kufanya mazoezi ya viungo. URAIS hapati ng'oo! Labda atapata kura nyingi za Watu wa Kaskazini
 
Back
Top Bottom