Kwaheri Lowassa, kwaheri CHADEMA...

Kwaheri Lowassa, kwaheri CHADEMA...

Kweli asee kwa heri lowasa mtaani karibu Ikulu, kwaheri chadema upinzani karibu Ikulu. Karibu ccm upinzani.. Karibu magufuli kambi rasmi ya upinzani.
 
lowassa ni tegemeo lililokufa rasmi juzi pale jangwani, kila aliyemuona amekwishakata tamaa
NB:UONGOZI HUAMBATANA NA AFYA BORA
 
siku zote ma jiniasi (watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri) hawanaga maneno mengi ila vitendo hilo lisikupe shaka, watu jana jagwani tulienda kumuona lowasa na majembe wengine hata wasingeongea chochote still hatupo tayari kuichagua CCM.
unajua story ya mtaani mida hii ni kuwa hata kama UKAWA WANGESIMAMISHA JIWE TUTACHAGUA HILO ILA SIYO HAWA MIUNGU WATU WA CCM

Kama wanatka mipasho si wanaye Mkwele?
Kama wanataka data na sifa za kinafki.... urokole feki si wanaye Pombe?

UKAWA vitendo, story vijiweni... Kazi mwanzo mwisho huwezi kasi hii kaa pembeni uwe mtazamaji!
 
Hivi ni kweli Lowasa sio muongeaji au anafanya makusudi,mbona alipokuwa ccm,alikuwa anahutubia kwa mpangilio unaoeleweka?

Hana hoja ataongea nini? Kin gone afya yake haimruhusu kuongea sana.
 
Huyu muasisi na mhandisi wa mnachokiita mfumo ndani ya CCM hafai kutuongoza kabisa, ikulu anaisaka kwa njia yoyote au kupitia chochote kile.
 
Nianze kwa kukupa pole Lowassa,halafu nikuage.

Ulichokifanya Jana pale jangwani kimedhihirisha kabisa wewe ni msanii wa hali ya juu na bila shaka unaitendea haki taaluma yako ipasavyo, kwa hili nikupe hongera nadhani baada ya October 25 utajiunga na kina Ray na utasaidia tasnia ya filamu kufika mbali.

Lowassa umekosa sera umekuwa ukirudia yale yale kila kukicha.

Umati mkubwa uliookuwepo pale jangwani kwa siku ya jana ulikuja kusikiliza ilani ya UKAWA na walitaka kusikia kutoka mdomoni kwako ukahaidi utawafanyia nini, unasema unaleta mabadiliko,hicho ndicho walichotaka kusikia na si habari za babu seya, bilali na masheikh wa uhamsho.

Kuwaambia wananchi wakasome ilani kwenye website ni kuwakosea heshima na kutothamini muda wao. Ni wananchi wangapi wenye access ya internet?

Ndiyo wananchi tunataka mabadiliko lakini siyo mabadiliko ya kiini macho kama yako lowassa.

Hotuba yako imeshindwa kukidhi kabisa kiu ya wananchi, umekosa mipango umekuwa mtu wa kusemewa na wapambe wako,wewe ndiyo mtendaji tunataka useme wewe.

Chadema huu ndiyo mwisho wenu,baada ya uchaguzi tunawasahau kabisa kwenye ulingo wa siasa. Mmeamua kulamba matapishi yenu na kutaka kuwalazimisha watanzania walambe pamoja na nyie ila wengi tumejitambua tumevunja uaminifu wetu kwenu.

Kama Mbowe aliamua kuchenji gia hewani sisi tutachenji ardhini ifikapo October 25.

Siioni nafasi ya Lowassa na UKAWA baada ya uchaguzi.

Kwaheri Lowassa, kwa heri UKAWA.

Ndoto za mchana na utasubiri kweli hilo litokee. Habari za Richmond sio kwamba zimeanza leo. Huenda hata kwenye kanga zako limeandikwa. Unaweza kuwa mwana siasa mzuri sana lakini mwisho wa siku ukajikuta kwamba huna jinsi zaidi ya umbea umbea tu. Na hilo ndio lina msumbua Doctor sasa.
 
Ikulu si mahali pa kujaribu ni patakatifu na makini ccm jipangeni kutekelza ilani hawa waacheni na scripts zao
 
Back
Top Bottom