Kwaheri Jenerali Davis Mwamunyange

Kwaheri Jenerali Davis Mwamunyange

Leo inatarajiwa kuwa siku ya mwisho wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange kuwatumikia watanzania katika nafasi hiyo ya juu kabisa katika masuala ya ulinzi na usalama.

Jenerali Mwamunyange alikuwa amalize muda wake mwezi Januari mwaka jana lakini rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliona ni vyema Jenerali Mwamunyange anayesifiwa kwa kulifanya Jeshi la Wananchi kuwa la kisasa aendelee kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja ambao unakoma leo 31.01.2016.

Lakini pia yawezekana rais Magufuli nayeye akaona ni vyema kumuongezea muda wa kuhudumu......

=======
LEO inatarajiwa kuwa siku ya mwisho ya utumishi jeshini kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange.

Jenerali Mwamunyange ambaye alizaliwa mwaka 1959, alikuwa amalize muda wake Januari 30, mwaka jana, lakini Rais Dk. John Mgufuli alimwongezea mwaka mmoja wa utumishi jeshini.

Mwamunyange ambaye ni Mkuu wa Majeshi wa saba tangu jeshi hilo lianzishwe mwaka 1964, ametumikia nafasi hiyo kwa miaka tisa na mienzi minne sasa.

Wengine ni majenerali wastaafu, Mrisho Sarakikya (1964-1974), Abdallah Twalipo (1974-1980), David Musuguri (1980-1988), Ernest Kiaro (1988-1994), Robert Mboma (1994-2002), George Waitara (2002- 2007).

Januari 30 mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya JWTZ (Ngome) Upanga, Dar es Salaam, Jenerali Mwamunyange alisema. “Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016, lakini Rais na Amiri Jeshi Mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 Januari, 2016 hadi tarehe 31 Januari 2017,” alisema.

Jenerali Mwamunyage alisema sababu iliyomfanya Rais Dk. Magufuli kumwongezea muda huo, imetokana na kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo.

Pia Oktoba 30, mwaka jana akiwa kwenye kilele cha sherehe za miaka 52 ya kuanzishwa kwa JWTZ zilizofanyika Bagamoyo mkoani Pwani, Rais Dk. Magufuli alimwahidi Mwamunyange kumpa kazi nyingine baada ya kustaafu kwake.

"Watu wameanza kusema nataka 'kuimilitarize' Serikali (kuendesha serikali kijeshi), lakini ukweli ni kwamba wanajeshi wana sifa nzuri ya maadili na uchapa kazi na hata wewe Mkuu wa Majeshi (Mwamunyange), ukistaafu nafasi zipo za kufanya kazi," alisema Rais Magufuli.


Chanzo: Mtanzania



Kwa jinsi alivyoliunganisha jeshi letu vema na wanajeshi wakawa wamoja zaidi,akaimalisha mafunzo mbalimbali,nidhamu,maslahi ya wanajeshi,mavazi kutoka sare pana pana hadi hizi za kisasa,jinsi alivyomnyamazisha Kagame na chochoko zake kule Congo kupitia kupigwa vibaya kwa M23 na kumnyong'onyesha kwa yale mavifaa ya kisasa siku zile pale uwanja wa uhuru,me namwombea kwa Mungu ampe maisha marefu lakini mh rais JPM akiona inafaa amteue kuwa mkuu wa idala nyeti ya usalama wa taifa ili kulilinda zaidi taifa,kuifanya idala iwe makini zaidi na itilie mkazo mambo ya msingi na yanayowza isaidia nchi zaidi kama vile kufanya ujasusi nyeti wa kiuchumi,kiteknorojia,kifedha na hata ikibidi ujasusi wa kwenye maeneo nyeti kimataifa,na kuwafanya waache kutufatilia sie wachngiaji wa Jf,kuubana upinzani na kuisaidia CCM badala ya nchi,
akienda pale ataunganisha idala mbili muhimu jeshi na idala ya usalama na kwa kuwa anakubalika pote nchi itakuwa imara zaidi na wananchi tutakuwa salama zaidi ya sasa,na uzoefu wake ni muhimu zaidi wakati huu tukikabiliwa na ubabe na vitisho vya bilionea Trump akiwa white house maana kwa kauli zake ataamsha mengi ni vema kama nchi tujipange
ni maoni yangu ya kizalendo tu.plz mabosi wa idala msiagize kucha zangu ziondolewe bado nazipenda
 
Hii habari kwa upande wa tarehe na kumbukumbu za matukio iko very poor.Mara leo tarehe 31.01.2016 mara mwaka jana january(january2016) Kikwete alimwongezea muda na bla bla blaa nyingi....


ime-be uptudated ikiongezewa nyama
 
Inawezekana Bongo hatuna. Siujui mfumo wetu maana karibia kila kitu ni siri.
Ndio maana tunaijua mifumo ya nje kuliko ya kwetu. Jeshi letu libadilike. information kama hizi ni public na hazikupaswa kuwa debated with no where to get them.

That being said, Trump hawezi kuwa 5*G kwa sababu sio mjeshi. Atabakia CiC of US Armed forces
Kwani uliambiwa trump ndio 5* general?
Msiwe wavivu kupitia kwenye wikipedia
5 Star Generals of American Military History
 
Kuna kumkumbuka MTU especially tz kwa mambo mawili,la kwanza huwa ni kimaslahi ametuachaje na la Pili ni kitaaluma hasa hasa kazi unayoifanya na kwa Jeshi ni vitu viwili kitaaluma na kimaadili ameawachaje.

Mara nyingi hayo ndiyo mambo ambayo kiongozi anapoondoka wengi huwa wana angalia hapo alipoingia alitukutaje na sasa anaondoka anatuachaje.

Mengine huwa yako ndani ya hayo kama mshikamano,umoja,upendo,bidii ktk kazi nidhamu n.k.

Najaribu kurudi nyuma kidogo enzi za CDF Mboma alipoingia 1994 alikuwa na changamoto zake hali ya uchumi wa nchi ilikuwa ngumu makusanya ya Kodi walikuwa chini sana na Jeshi lilipitia kipindi kigumu sana ktk mahitaji.

Hata baadhi ya askari walifanya ndivyo siyo mtaani kwa wanainchi bala wenzako mmoja alipokuwa amefanyiwa lolote ambalo si zuri.

CDF Waitara 2002 alifanikiwa kurudisha heshima ykwa kuwabana askari ktk maadili ya Jeshi na kuareview recruitment procedure za kijeshi ili kuwapata vijana wenye maadili Emma ndani ya Jeshi na hiyo ilisaidia kujenga Jeshi imara zaidi hasa ktk kipindi cha mpito kiuchumi ambacho nchi ilikuwa inapitia.

Changamoto aliyoipata CDF Mboma ni kuwa nchi ilikuwa ktk kipindi kigumu kiuchumi kwa hiyo pamoja na nidhamu nzuri na taratibu nzuri lakini uchumi ulikuwa mgumu sana.Lakini Wanajeshi wengi wanaoujua maana ya Jeshi walimpenda sana.

CDF Mwamunyange 2007 akachukua nafasi huku nchi ikiwa na Neema na Rais Mkapa alijitahidi sana kuimarisha uchumi na hata Rais Kikwete alipoingia Ikulu pesa nilikuwepo ya kutosha ndipo sasa Makazi mengi ya majeshi yamejengwa,vifaa vingi vya kisiasa Rais Kikwete amenunua na kuboresha maslahi ya wanajeshi awamu kwa awamu.

CDF Mwamunyange anaondoka akiwa ameliacha Jeshi ktk hali nzuri tu ila mabadiliko ni tu kwa sasa Yale Maduka ya duty free ndiyo hayapo tena ndani ya kambi za Jeshi kama ilivyozoeleka.

Hatujui CDF mpya a nakuja na yapi mapya ukiacha Yale ya kawaida ndani Jeshi kama majukumu ya kila siku.
 
Duh hakuona Wa kumpa nafasi yake and then jeshini kuna nidhamu ya hali ya juu?
Ambiguous

Jana nilipita nikaona tent pale uwanjani jeshini upanga sikuelewa somo
linahusu nini
 
H


Inanisikitisha kama nawe ni mfuasi wa Wikipedia mkuu. Ingekua source nyingine ningeweza kubisha kwa uhakika
Una maana hata quotation ya Newton's third Law of motion iliyo Wikipedia ni uongo? Au kuwa Magufuli ni Rais wa Bongo nayo ni uongo? Nilitarajia ujikite kwenye ukweli wa data zenyewe badala ya kuishambulia Wikipedia. najua kuna taarifa pale haziko accurate. Lakini kwa hii issue wako right.

Kama unadhani hawako sahihi basi usishambulie tu bali onesha kwa ushahidi kuwa waliyoandika sio kweli. Ndio mijadala ya kistaarabu inapaswa kuwa!
 
Mtanzania Fanyeni utafiti mwamnyange hujawai kuwa Mnadhimu Bali kabla Hajawa cdf alikuwa mkuu wa Jkt akiwa na cheo Cha meja generali
baada ya GENERAL MBOMA kustaafu pamoja na aliyekuwa Chief of Staff SAYORE kama sikosei Mkapa alimteuwa Waitara kuwa CDF na Gau kuwa CoS huyu Gau alikuja kurithiwa na Abdlurhaman NShimbo wakati Nshimbo anapata misukosuko ya ubadhirifu hasa kwenye mradi wa kilimo kwanza alipelekwa CHINA kuwa Balozi akimrithi mzee wa Jaramba Balozi Ramadhani Mapuri. baada ya kuondolewa na kuwa balozi nafasi ya NSHIMBO ilishikwa na MAJOR GENERAL Mwamunyange ( huyu pia aliwahi kuwa mkuu wa utambuzi jeshini- CMI chief of military intelegence, Na mkuu wa JKT aliyechukua mikoba ya NSHIMBO) baada ya kupandishwa cheo na kuwa Lieutnant General na aliyekuwa Commanding chief Kanali Jakaya kikwete. ambaye baadae (kama mwaka mmoja hivi yaan 2007 ) alimpandisha tena cheo na kuwwa FOUR STAR GENERAL na kumteuwa kuwa CDF na vilevile alimpandisha Major General NDOMBA kuwa Lt General na kumteua kuwa CoS
 
Back
Top Bottom