Kwaheri Jenerali Davis Mwamunyange

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Leo inatarajiwa kuwa siku ya mwisho wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange kuwatumikia watanzania katika nafasi hiyo ya juu kabisa katika masuala ya ulinzi na usalama.

Jenerali Mwamunyange alikuwa amalize muda wake mwezi Januari mwaka jana lakini rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliona ni vyema Jenerali Mwamunyange anayesifiwa kwa kulifanya Jeshi la Wananchi kuwa la kisasa aendelee kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja ambao unakoma leo 31.01.2016.

Lakini pia yawezekana rais Magufuli nayeye akaona ni vyema kumuongezea muda wa kuhudumu......

faf8cc92-cf12-455e-bcd7-2bfe0f464e21.jpg

=======
LEO inatarajiwa kuwa siku ya mwisho ya utumishi jeshini kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange.

Jenerali Mwamunyange ambaye alizaliwa mwaka 1959, alikuwa amalize muda wake Januari 30, mwaka jana, lakini Rais Dk. John Mgufuli alimwongezea mwaka mmoja wa utumishi jeshini.

Mwamunyange ambaye ni Mkuu wa Majeshi wa saba tangu jeshi hilo lianzishwe mwaka 1964, ametumikia nafasi hiyo kwa miaka tisa na mienzi minne sasa.

Wengine ni majenerali wastaafu, Mrisho Sarakikya (1964-1974), Abdallah Twalipo (1974-1980), David Musuguri (1980-1988), Ernest Kiaro (1988-1994), Robert Mboma (1994-2002), George Waitara (2002- 2007).

Januari 30 mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya JWTZ (Ngome) Upanga, Dar es Salaam, Jenerali Mwamunyange alisema. “Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016, lakini Rais na Amiri Jeshi Mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 Januari, 2016 hadi tarehe 31 Januari 2017,” alisema.

Jenerali Mwamunyage alisema sababu iliyomfanya Rais Dk. Magufuli kumwongezea muda huo, imetokana na kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo.

Pia Oktoba 30, mwaka jana akiwa kwenye kilele cha sherehe za miaka 52 ya kuanzishwa kwa JWTZ zilizofanyika Bagamoyo mkoani Pwani, Rais Dk. Magufuli alimwahidi Mwamunyange kumpa kazi nyingine baada ya kustaafu kwake.

"Watu wameanza kusema nataka 'kuimilitarize' Serikali (kuendesha serikali kijeshi), lakini ukweli ni kwamba wanajeshi wana sifa nzuri ya maadili na uchapa kazi na hata wewe Mkuu wa Majeshi (Mwamunyange), ukistaafu nafasi zipo za kufanya kazi," alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema anapenda kuteuwa wanajeshi katika nafasi mbalimbali serikalini kwa sababu anasukumwa na upendo wake kwao kutokana na sifa walizonazo za kuwa na maadili na kuchapa kazi.

Baadhi ya maofisa wa JWTZ waliotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo, walisema jambo la kustaafu ama kutostaafu kwa Mkuu wa Majeshi lipo katika mamlaka ya Rais.

Taarifa nyingine zimedai kuwa takribani wiki moja sasa kumekuwa na shughuli katika kambi mbalimbali za jeshi Dar es Salaam za kumpongeza Jenerali Mwamunyange kutokana na utumishi wake jeshini.

Kabla ya Mamunyange kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete Septemba 2007, alimpandisha kutoka cheo cha Luteni Jenerali kuwa Jenerali na kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi.

Kabla ya uteuzi huo, Mwamunyange alikuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ. Januari mwaka jana, alipokuwa akitangaza kuongezewa muda, alitangaza pia mabadiliko yaliyofanywa na Rais Magufuli jeshini.

Mabadiliko hayo ilikuwa ni pamoja na kuwateua, Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, ambapo kabla alikuwa Mkuu wa Tawi la Utendaji wa Kivita na Mafunzo Makao Makuu ya Jeshi.

Jenerali Mwamunyange, alimtaja pia kamanda mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi kuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Meja Jenerali Sirakwi alikuwa Mratibu Msaidizi Mkuu Baraza la Usalama wa Taifa- BUT.

JWTZ ilivyong’ara

Ndani ya miaka tisa ya Jenerali Mwamunyage, JWTZ imefanya kwa mafanikio shughuli mbalimbali za kulinda amani katika mataifa yenye vita pamoja na operesheni nyingine za kupambana na waasi wakiwamo wa Kundi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mwaka 2008, Majeshi ya Umoja wa Afrika yaliyoongozwa na JWTZ kwa kushirikiana na Jeshi la Shirikisho la Comoro, yalifanikiwa kukikomboa kisiwa cha Anjouan kwenye operesheni ambayo haikupata upinzani.

Operesheni hiyo, iliyopewa jina la `Demokrasia Comoro’ ilifanya Kanali Mohamed Bakar aliyekuwa akikiongoza kisiwa hicho kimabavu baada ya kujitangazia utawala mwenyewe Julai, 2007, kutorokea kisiwa cha Mayotte kilichopo chini ya utawala wa Ufaransa.

Tangu mwaka 2009, JWTZ imekuwa ikipeleka wanajeshi wa kulinda amani Darfur nchini Sudan, shughuli ambayo inaelezwa kwamba imefanywa kwa weledi mkubwa.

Msemaji wa JWTZ, Meja James Macheta alipoulizwa kustaafu kwa Jenerali Mwamunyange, alimtaka mwandishi wetu kuwa na subiri kwa kile alichodai yuko barabarani anaendesha gari.

Chanzo: Mtanzania
 
Mtanzania Fanyeni utafiti mwamnyange hujawai kuwa Mnadhimu Bali kabla Hajawa cdf alikuwa mkuu wa Jkt akiwa na cheo Cha meja generali
 
Back
Top Bottom