Kwa wenye magari woote, Inawezekanaje kulipia road license gari ambalo ulishauza?

Prof Decentman

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
276
140
Leo nilisimamishwa na trafic maeneo fulani. Nikiwa na ujasiri gari yangu ipo salama kwa kila kitu..nikaambiwa nitoe kadi ya gari baada ya kutoa nikaambiwa kuna tatizo kidogo niende kuwaona watu wa TRA na kufika hapo wakanitajia orodha ya magari yenye jina langu kama nayafahamu.

Nikakumbuka magari hayo nilishayauza muda mrefu na nilishasahau. Baada ya hapo nikaambiwa nikalipaki gari ktk yadi then niende tra. Kufika kule nikaambiwa niyalipie road licence yale magari ambayo nimeyauza ili niweze kupata gari langu ninalotumia ambalo halina kosa lolote.

Baada ya hapo ikabidi nihangaike kuazima pesa ili niwalipie hao watu ambao hawakubadili umiliki ktk kadi za gari maana nilikuwa na safari muhimu muda huo.

Nikajiuliza maswali, hivi kweli tumefikia hapo kwamba unakamata gari nyingine kulipia gari nyingine??
Is it fair? Kwa nn isikamatwe gari husika??
 
Mkuu unatisha aisee!!umetuambia hapa 'Magari' hayo ulishayauza muda mrefu! Ina maana ni zaidi ya Gari moja,napata ukakasi kidogo hii story kama umeiedit hivi
1.road licence gharama za kerenew zinapanda kila mwaka unapokuwa hujarenew pamoja na fine, kutokana na Cc ya Gari husika...INA maana halo kwa Gari moja utakuwa umelipa laki kadhaa kama sio milioni kadhaa.
2.kulikuwa na ugumu gani kumtafuta uliyemuuzia Gari,au mliuziana kama Kuku bila mkataba?!
 
Vp kama gari lilishaharibika na halitumiki tena? Nonsense
Kujiweka safe side kwa lolote lile ukishauza gari nenda na mnunuzi TRA mkabadili umiliki itawasaidia wote wawili
Kuna jamaa aliuziwa gari kumbe mmiliki wa kwanza alishawahi kuandikiwa faini ya sh 30000/=halafu hakulipa, siku gari inakamatwa ile faini pamoja na adhabu na riba ilikuwa imeshafika laki na 80
Bwt siku hizi kama gari hulitumii tena kwa uchakavu ubovu nk bado unatakiwa kwenda kutoa taarifa TRA ukiwa na ithibati za ki police
 
Leo nilisimamishwa na trafic maeneo fulani. Nikiwa na ujasiri gari yangu ipo salama kwa kila kitu..nikaambiwa nitoe kadi ya gari baada ya kutoa nikaambiwa kuna tatizo kidogo niende kuwaona watu wa TRA na kufika hapo wakanitajia orodha ya magari yenye jina langu kama nayafahamu.

Nikakumbuka magari hayo nilishayauza muda mrefu na nilishasahau. Baada ya hapo nikaambiwa nikalipaki gari ktk yadi then niende tra. Kufika kule nikaambiwa niyalipie road licence yale magari ambayo nimeyauza ili niweze kupata gari langu ninalotumia ambalo halina kosa lolote.

Baada ya hapo ikabidi nihangaike kuazima pesa ili niwalipie hao watu ambao hawakubadili umiliki ktk kadi za gari maana nilikuwa na safari muhimu muda huo.

Nikajiuliza maswali, hivi kweli tumefikia hapo kwamba unakamata gari nyingine kulipia gari nyingine??
Is it fair? Kwa nn isikamatwe gari husika??
mkuu mi hata
kama ningekuwa manji nisingelipia kupeana hasara tu
 
Pole sana mkuu kwenye kila kadi ya gari kuna sehemu ya kubadili umiliki ungekuwa unajua ungeajaza tu hapa ingekusaidia sana kaka. nimeattach na hiyo sehemu kwenye kadi.
 
Attachments

  • Capture.PNG
    Capture.PNG
    303.3 KB · Views: 371
Vyema kubadilisha jina la umiliki wa gari unapokuwa umeliuza la sivyo unaweza ukajikuta unafikishwa mahakamani kwa kosa la uhalifu ikiwa uliyemuuzia alilitumia kwenye matukio ya uwizi, kwa kigezo cha jina kwenye kadi ya gari ni ushahidi tosha wewe kuwa mtuhumiwa
 
Taratibu huwa zipo, kwa hiyo tujifunze kuzifuata. Unapouza gari hakikisha unayemuuzia humpi gari mpaka ametransfer umiliki, unapo scrap gari ni lazima uwape taarifa tra.

Unapo uza gari halafu umiliki kwenye kadi na tra bado unaonekana ni wakwako jua system inakutambua wewe kama mmiliki, lolote likitokea basi lazima uwajibike.
Unaposcrap gari lazima tra wawe na taarifa ili walitoe kwenye system ukiscrap na hukuwapa taarifa basi hilo gari linahesabika ni la kwako nawanaendelea kuhesabu madeni yao tu..
 
Kinachotuumiza gari inapouzwa huwa hatuuzi kwa mmiliki wa kudumu inaweza kuona gari inatembea kwa watu hata watatu, na likishaenda vijijini huwa hata motorvehicle hazilipiwi, nashukuru Niliwahi kuuza gari moja jamaa alivyoenda kulipia motorvehicle wakamgomea ikabidi anitafute tukaingia mkataba tukabadilisha jina
 
mkuu shukuru mungu kuwa hayo magari hakuna lililotumika kwenye tukio lolote baya maana hata huu uzi usingeweza kuutuma hapa JF! tuwe makini na hivi vitu vidogo vidogo huwa vinaleta matatizo makubwa kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom