Kwa wenye kuweza kuchezesha kichwa tu....

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
5,059
13,719
Chemsha Bongo...
--------------------------------

Inspekta Gamba akiwa anaelekea kazini saa moja asubuhi akakuta kikundi cha watu kando ya mtaro. Kwenda kujionea kunani, akakuta kumbe wamezingira maiti ya mwanamke.

Akawaamuru wasogee kando. Akaanza kuichunguza ile maiti ambapo akakuta pete ya ndoa kidoleni. Pia akakuta simu kwenye pochi. Hivyo akaona amtaarifu kwanza mumewe. Akapekua phonebook na kukutana na namba ya "Hubby".

Akampigia na kumwambia, "Mimi ni Inspekta Gamba wa Jeshi la Polisi. Pole sana kwa taarifa nitakayokupatia. Mkeo ameuwawa."

"Haiwezekani!! Mbona katoka mzima asubuhi hii hii kuelekea kazini!!" Mume akajibu kwa taharuki.

"Njoo uthibitishe." Inspekta akakata simu. Kisha akapiga makao makuu kuita askari.

Ndani ya robo saa mume wa marehemu akawa amefika eneo la tukio. Alipomuona tu marehemu mkewe akaishiwa nguvu na kupiga magoti kando ya mwili huku akilia.

Inspekta akawaambia askari waliokuwa wameshafika eneo la tukio wamkamate mume wa marehemu ndio muuaji.

Swali: Je Inspekta alijuaje kwamba mume wa marehemu ndio muuaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom