Kwa watumiaji wa huduma ya Uber..

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,285
Naomba kujua ni reliable kiasi gani... Sjawahi tumia hii kitu, nna safari ambayo ntajitahidi kuja kuchukuliwa na taxi kutoka kitunda hadi ubungo terminal asubuhi sana.. Je naweza kuiamini uber kwa maana ya ku request uber mapema asubuhi na ikafika kwa wakati maana nisije nikakaa nasubiri uber hadi nikaachwa na basi... Nauli zenyewe ndo kama mjuavyo..
Asanteni.
 
Uber safi sana kijana wangu ..bei zao ziko very affordable .
Kama una Uber apps tayri utaona zipi ziko karibu na location uliopo
 
Mkuu , Uber ni nzuri sana na gharama zake zinakuwa sio mbaya.Ila kama unasafiri asubuhi sana kabla ya saa 12 au saa 1 usitegemee sana uber kwa kuwa madereva wengi wanaanza kazi kama 12 na nusu hivi hivyo utachelewa basi hapo ubungo.
 
Mkuu , Uber ni nzuri sana na gharama zake zinakuwa sio mbaya.Ila kama unasafiri asubuhi sana kabla ya saa 12 au saa 1 usitegemee sana uber kwa kuwa madereva wengi wanaanza kazi kama 12 na nusu hivi hivyo utachelewa basi hapo ubungo.
Na huu ndo wasiwasi wangu maana Basi linaondoka saa 2, na nipo kitunda huku.. Ntapata kweli uber mida ya angalau saa 12 kasoro hivi ili niwahi..
App ninayo tayari
 
Fanya utaratibu mwingine pia ikifika mda unaotaka kutoka anza na UBER pia kama hutopata basi ile plan B yako ndo solution
 
Pia unaweza kuunga na taxify, uwe na zote mbili.Mfano mimi nikiwa nimeita uber nikakutana na mpuuzi asiyejua kujali muda au ukimuuliza alipo analeta ujinga na cancel na kuita Taxify.
 
Hivi umewaza kwamba inawezekana ukaamka asubuhi halafu kukawa hakuna dereva karibu?

Yaani unaambiwa hakuna dereva karibu yako ni ama uendelee kusubiri au akili ikurudie ujue kua vitu serious vinahitaji serious measures.

Nilifanya mchezo kama wako.

Nikajikuta naenda barabarani kutafuta bajaji.

Usicomplicate vitu mzee.
 
Uber is nice, kuna siku nilikua na kiasi kikubwa sana cha fedha nilipaswa kufanya manunuzi, nikachukua uber mambo yalienda vizuri tuu
 
Back
Top Bottom