Kwa wataalam wa Umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wataalam wa Umeme

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by KakaJambazi, Apr 2, 2011.

 1. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Nina digital stabilizer ya tropical Power, wakati mwingine inaonyesha "Input ni 218V,,Output = 231V"

  Inawezekanaje hii?
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  unaitumia kwenye nini?
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Kwe tv na hme theator.
   
 4. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni kama kuna tatizo lolote. Yawezekana output yake ni 230V na haiwezi kuwa accurately. Hivi ikiwa 229V au 231V bado inakaribiana kabisa. Usihofu. Wakati mwingine inategemeana na vifaa vilivyounganishwa katika stabilizer hiyo.
   
 5. P

  Percival JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na jibu la GM7. Stabilizer yako imekua set at 230V na umeme unaoingia ni 218V unakua stabilized to 231V ambayo ni sawa 230 kama alivyosema GM
   
 6. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mkuu,, sasa kama yenyewe imepokea mfano 200v kutokea kwenye sacketi, inatoa wapi 220v kutumiwa na vifaa nilivyoconnect.Hizo 20v zinatoka wp?
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Si ndio maana ya voltage stabilizer? Umeme ukishuka au ukipanda, kwa kiwango cha hiyo stabilizer, iuweke sawa. Sioni tatizo hapo.
   
 8. S

  ShockStopper Senior Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Voltage Stabilizer, Tafsiri rahisi:
  voltage, ni kiwango cha umeme
  stabilizer, inatokana na neno stable, kinachosababisha kuwa stable
  stable ni sifa ya kutulia, kutobadilikabadilika.

  Voltage Stabilizer upande mmoja inapokea umeme wa kiwango kinachowezakubadilika toka kwenye line,
  upande wa pili inatoa umeme wa kiwango fulani kwenda kwenye matumizi.

  Hivyo,
  Voltage Stabilizer ni chombo kilichokusudiwa kutoa kwa ajili ya matumizi, umeme wa kiwango kisichobadilika 'stable' hata kama kiwango cha umeme toka kwenye line kitakuwa kinapanda na kushuka ovyo ovyo.
  Kitu cha kujali ni kuwa Voltage Stabilizer itoe umeme wa kiwango kinachohitajiwa na chombo unachotumia (mfano 230V). Iwapo line voltage itapanda zaidi ya kiwango hiki, stabilizer itashusha itoke 230V, na ikishuka (mfano 200V), stabilizer itafidia itoke 230V.
  Ndani ya Stabilizer kuna auto transformer (steps up or down) kufanikisha hilo.
  Iwapo hiyo uliyonayo ni Digital maana yake ni kwamba digital circuit ndiyo inaiongoza transformer wakti gani wa kupandisha na kwa kiasi gani na wakati gani wa kushusha na kwa kiasi gani.

  Hata hivyo,
  TV za siku hizi zimetengezewa Auto voltage circuit (check name plate nyuma ya TV yako karibu na mahali pa kuchomeka waya wa umeme).
  Iwapo utakuta maandishi mfano wa haya, 190~260V AC, ina maana kuwa umeme wa Tanesco ukishuka hadi 190V, TV yako itaendelea kufanya kazi na ukipanda hadi 260V bado hakutakuwa na tatizo.

  Kwa hiyo kimsingi chombo chako hakihitaji stabilizer bali kinahitaji Surge Protector, chombo cha kujihami dhidi ya umeme unaosababisha madhara. Bei yake ni ndogo kuliko ile ya stabilizer, jipatie Protector na hifadhi Stabilizer kwa matumizi yenye huo uhitaji.

  Asante kwa kuhitaji kueleweshwa, nakaribisha maswali mengine kuhusu vyombo vinavyotumia umeme.
   
 9. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  mkuu mimi ninahitaji kujua mchanganyiko uliyotumika kuiwezesha tube light kuwaka. Maana hizi taa huwa zina element mbili.yaani mwanzo na mwisho.ila katika utendaji wake taa huonekana yote imewaka.pia hizi taa kunawakati huwa zinagoma kuwaka zinakuwa zina blink tu.ila ukipima kipimo kinakuonyesha kuwa ni nzima.
   
 10. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hicho kifaa chako sio stabilizer ila ni regulator, stabilizer huwa inafanya output kuwa stable, ila regulator yenyewe ina uwezo wa kuongeza umeme ukiwa mdogo na kupunguza umeme ukiwa mkubwa!!
   
 11. S

  ShockStopper Senior Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwanza gonga hii link hapa chini uipitie halafu ikibidi urudi kwa ufafanuzi.
  Regards!

  HowStuffWorks "How Fluorescent Lamps Work"
   
 12. S

  ShockStopper Senior Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kuna haja ya kujua na kutofautisha twist za lugha za kibiashara na zile za kitaaluma.
  :smile-big:
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  ya kichina hiyo mkuu be careful
   
 14. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Watu wengine mna obsession na china wakatii hapa bongo au africa hata kakiwa wanda ka vifungo au hata tooth stick hakuna.

  Sasa si bora hao wachina. Na duniani nchi gani haitumii bidhaa za china?

  Punguzeni siasa
   
 15. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Wachina wana madaraja tofauti ya bidhaa zao, hiyo Stabilizer kama ingekuwa made in China for Europe/USA angeweza kuinunua? usilalamikie China kwani inakupa kitu kulingana na pesa yako, The more is Cheap the more is fragile, impermanent, poorly made, temporary, undependable,
   
 16. ogm12000

  ogm12000 JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 311
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Uko sawa kaka ! ni voltage regulator, dc-dc converters ambazo inaweza kuwa buck converter, buck-boost au boost converter ambazo ni types za switching regulators. buck-boost ina step up and down lkn ina invert output voltage. ila SEPIC yenyewe ina punguza au kuongeza umeme bila ku invert output voltage. Kwenye hizi regulator inaweza kuweka zener diode ili ku stabilize output voltage. Ukitaka knowledge zaidi fuatilia power electronics. Boost converter zinatumika pia katika Maximum power point tracking (MPPT). Zinakuwa embedded ili kuhakikisha source either solar PV cells, TEG, Fuel cells, etc zina give maximum power
   
 17. MAHENDEKA

  MAHENDEKA JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  hongera kwa maelezo mazuri,ila mimi nina maswali 2
  1.nijuavyo mimi kazi ya saketi breka,ile inayokaa karibu na main switch ndani ya nyumba ni kuzuia shoti ya umeme mkondo geu au altenating current ,sasa kwa nini vitu mfano Tv,redio ndani vinaungua bila circuit breaker kujua/kudetect ?
  2.kuna jambo moja huwa nalifahamu kinadharia tu ila practically niliwahi kujaribu lakini niliishia njiani ni hivi "krichoff" alisema katika saketi yeyote nyaya za umeme mbili au zaidi zinapokutana katika pointi moja(node).basi pointi hiyo inakuwa neutral,yaani haina umeme!!
  "in any closed circuit/loop/mesh the summation of currents let say i1 +i2+i3=0" and "the summation of potential difference at that particular point v1+v2+v3 also is equal to zero,jambo ambalo kinadharia nalikubali kabisa..Sasa swali langu ni kwamba je unaweza kushika kwa mikono mitupu sehemu kama junction box bila madhara?,binafsi nshawahi kuunganisha live na neutral ktk switch halafu nikataka niguse junction yake lakini nilisita kidogo baada ya kuona cheche kwa mbaali..kwa hiyo bado nina contradiction kati ya nilichokisoma na nilichokiona..kama una ufahamu na mambo haya nifafanulie
   
 18. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Labda nikusaidei hilo swali la kwanza, Ukijaribu kufungua hiyo wanayoita Socket break uone waya wake utashangaa it is all about 4mm, sasa mpk uje ukatike Redio Tv zimeshakwenda, sasa Tanesco wanakomalia sana Earth Leakage Socket Break na hawakuwekei umeme mpk uiweke baada ya kuona hizo za kwao ni hewa, yenyewe ikihisi tu kuna hitilafu inazima.

  Kuhusu swali la pili umenikumbusha mbali sana nikiwa 2nd year, ni kweli kwenye closed circuit yeyote current =0 but kwa practical sijawahi jaribu, wewe ulikuwa na moyo kuunganisha live na neutral bila mzinga!!!
   
Loading...