Una hakika kuwa haya hayakuzungumzwa? au aliyezungumza wakati huo hukumpenda? au chombo alichotumia kutoa habari hukukiamini? haya yapo tena mengi, na hao munaowaona watukufu hizi ndio kazi zao.NI kweli haya ni madai mazito lakini hauwezi kuyaamini na kuyafanya ndo hali halisi ya bwana Pombe eti kwa kuwa mtu mmoja kajisikia leo kuyatoa. Miaka zaidi ya 10 imepita toka alipotenda baadhi ya haya, ulikuwa wapi kuyasema?
Hata kama madai yako ni ya kweli, umejiangusha wewe mwenyewe maana hukuyatoa mapema. Matokeo yake madai yako yanazidiwa nguvu na utendaji wake na hivyo watu kumwona yeye anafaa zaidi kuliko madai yako.
Kitila Mkumbo yuko sahihi kwenye hili. Waziri ni mbunge na si mwanafunzi wa shule ya msingi anayemuogopa kiranja wake. Kama mbunge, dhamana yake kubwa ni kwa wale waliomchagua na si kwa huyo aliyempa cheo cha uwaziri. Waziri makini anapaswa kutetea kile tu ambacho anamini kwa dhati kuwa ni kwa manufaa ya waliomtuma na si kwa sababu aliyemteua anadhani hivyo. Anapoona mambo hayo mawili yanagongana, waziri makini anapaswa kuachia kofia ya uwaziri na kubakiza ile muhimu zaidi ya ubunge. Mwaka 2003 Robin Cook, kiongozi wa chama cha leba bungeni, mwenye wadhfa ya uwaziri, alijiuzuru nafasi hiyo baada ya kutokubaliana na uamuzi wa serikali ya Tony Blair kuvamia Iraq. Waziri mwingine, Clare Short nae ingawa awali aliunga mkono uamuzi wa Blair lakini baada ya kutafakari nae akaamua kuachia ngazi. Ndivyo inavyotakiwa. Kwa upande mwengine, Colin Powell mpaka kesho kutwa atalaaniwa kwa kutoa ushahidi wa uongo Umoja wa Mataifa juu ya WMD za Iraq. Hawezi hata siku moja kujitetea kuwa alifanya hivyo kwa vile aliagizwa na rais wake. Alichosema ni kuwa alidanganywa.
Maadili ya kazi hayana maana utekeleze maamuzi au maelekezo ambayo sio Just. Wakina Himmler, Goebbels, Eichmann na wengine kibao waliokuwa wakiendesha concentration camps chini ya serikali halali ya Nazi Germany, hawakuweza kujitetea kuwa walifuata maagizo ya Fuhrer wao! Mtu ukiwa kiongozi wa ngazi yeyote unatakiwa kupima haki ya kila unachoagizwa.
Kwa vile wengi walimuandama Zitto haina maana kuwa alikosea. Yeye alistahili sifa kama kiongozi kusimamia principle zake. Kilichotakiwa kufanywa ni kuonyesha kuwa hizo principle zilikuwa potofu na si kumbeza.
Kwa hali hii, kwenye suala la uuzaji wa nyumba za serikali pamoja na kuwa uamuzi ulikuwa wa kabineti nzima ( si BWM peke yake), waziri aliyepewa dhamana ya kutekeleza maamuzi hayo hawezi kukwepa kuhusishwa na uamuzi huo. Swali lingine linachofuata ni namna utekelazaji huo ulivyofanyika. Je, ulikuwa wa haki na uwazi? Je ulikuwa na mafanikio yeyote kwa maana kuwa serikali ilifaidika vipi? Kama matarajio yetu hayakufikiwa, ni kitu gani kilisababisha hali hiyo? Yote haya ni maswali halali na yanastahili majibu kutoka kwa mtu yeyote aliye makini na mwenye mapenzi na taifa letu. Maswali kama haya yanapaswa kuulizwa kwa yeyote yule ambaye amepewa nafasi ya uongozi katika nchi yetu. Bahati mbaya hatupendi kuuliza maswali magumu maana tunachokitaka ni platitudes!
Amandla.....
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa mengi uliyongea yana ukweli mtupu LAKINI ktk system iliyo kamilika.
Kwa jamii ile jinsi ilivyoharibika nafikiri nikumwonea bure Magufuli kuhoji kwamba ugawaji na process ilikuwa just. Kwa Tanzania huwezi simamia kitu chochote kwa u-just, labda usiamamie mwenyewe kila idara, na hata hivyo bado huwezi.
Mimi nafikiri swali ambalo ni genuine la kuulizwa ambalo nakubaliana nalo moja kwa moja kwa hali ya Tanzania, nafikiri ni hili je Magufuli alinufaika je na uuzwaji wa nyumba hizo tulete na vidhibitisho tuache zile hadithi tulizosimuliwa wakati ule kwamba sumaye anamiliki morogoro yote kumbe uzushi mtupu.
Sio kila mtu anayeuliza maswali ni mpinzani. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuuliza maswali na wale wenye majibu kutoa majibu. Kuna ishu nyingi kwa mtendaji yeyote aliyekuwa katika nyadhfa za juu kama Mheshimiwa Magufuli. Kwa mfano, kuna masuala ya barabara. Je zote tulizoahidiwa zilijengwa? Na kama zilijengwa kwa kiwango gani na gharama gani? Kama hazikujengwa, nini kilisababisha kutokujengwa kwake? Mheshimiwa Magufuli alisimamia vizuri matumizi ya magari ya miradi na ya serikali. Je serikali iliokoa kiasi gani katika zoezi hilo?
Mheshimiwa Magufuli aliwahi kuwa waziri wa ardhi. Je palikuwa na nafuu katika kero ya upatikanaji wa viwanja? Jee uvamizi wa viwanja na maeneo yalio wazi ulipungua na wale waliofanya hivyo kuchukuliwa hatua? Ni sera gani wizara hiyo ilibuni kuwaboreshea wakazi wa nchi yetu makazi yao?
Mheshimiwa Magufuli aliwahi kuwa waziri wa uvuvi n.k. Je katika wakati wake, uvuvi haramu ulipungua? Jee sekta hii ilipanuka ili kuchangia zaidi katika pato la taifa na lishe ya wananchi wake? Na maswali mengine kama hayo.
Vile vile, yeyote ambaye atajitokeza au atapendekezwa kugombea urais wa nchi yetu, inabidi aulizwe maswali kutokana na utumishi wake au utendaji wake katika sekta yeyote ile aliyoshiriki. Kama alikuwa mfanyabiashara basi itabidi tujue kama alikuwa na mafanikio na jinsi alivyopata mafanikio hayo. Kama alikuwa mbunge awali, nae ni lazima tujue mchango wake katika bunge na kwa wale waliomchagua. Kama alikuwa mtumishi wa Mungu, nae vile vile.
Ni lazima tujitahidi ili tuchague mtu tukiwa macho wazi. Wakati wa visingizio umepita.
Amandla......
hili wazo binafsi haliwezi kupostiwa kwenye original post ya burigi lazima uanzishe yako? too many new posts hata za maana sasa hatuzisomi.
Haya maswali uliyouliza ni mazuri na kama kweli ulitaka mjadala wa namna hii basi ilikuwa unaya shot mapema tu badala ya kutanguliza hisia kuwa watu wanaosifia utendaji wa Magufuli ni sawa na wale waliokuwa wakimshabikia Kikwete,hoja ambayo nashukuru kuna member hapa amekujibu vizuri sana.
Lazima tukubaki kwamba,hakuna binadamu yeyote aliyekamilika.Magufuli kama binadamu hajakamilika,hivyo ni wazi kuwa hata katika utendaji wake kuna makosa alishayafanya na atayafanya.HAKUNA BINADAMU/KIONGOZI ASIYEFANYA MAKOSA.Kwahiyo Magufuli kufanya makosa isiwe nongwa.Muhimu ni kupima uzito wa hayo makosa na kisha kulinganisha na uzito wa mafanikio yake ya kiutendaji katika Taifa hili.Sasa isiwe ni kutafuta vijimakosa tuu alivyowahi kufanya na kuvishikia bango eti hafai kuwa kiongozi as if labda Tanzania tulishawahi kuongozwa na Malaika au tuna Malaika tunayemtegemea kuja kutuongoza.
Sipingi kujadili mabaya ya Magufuli,lakini mpaka sasa sijaona baya la msingi kusema eti hafai kuwa kiongozi hasa nikimlinganisha na wanasiasa wengi ninaowasikia kuwa wana nia ya kugombea Urais Tanzania.
Mze kila mtu ana good na bad History hata magufuri ana mema mengi tu amefanyia taifa hili mfano ameweza kusimamia wizara mbalimbali kwa ufanisi mkubwa kulinganisha na wenzake waliopata kupita katika wizara hizo mfano ujenzi wa barabara aliweza kusimamia vizuri zaidi na hiyo ndiyo sifa tunayompamba nayo sana kwa kweli hata mimi ninampongeza lakini hata humo ukiangalia kwa ndani utagundua kuwa kuna vitu vingi alifanya ambavyo kimaadili vinamwangusha kuwa kiongozi bora na ukweli utabaki ndani ya samaki kumi walioza angalau yeye hajafikia hali mbaya anaweza kiliwa hata kwa ndimu
Ni muhimu kupata taarifa kama hizi kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wetu, na si vizuri kuwakatisha tamaa wanaotoa taarifa hizi na kuwapa watu fulani utakatifu wakati pengine hawana.
Nakumbuka mwaka 2005 watu walivyokuwa wamepagawa kwenye forum ya uchaguzi.com (kama JF ya leo), ulikuwa huwezi kusema neno lolote watu wakaelewa na ulikuwa unaitwa majina yote ya usaliti hapa duniani ukimkosoa mgombea wao kipenzi. Niliandika makala kuhusu sababu 15 kwa nini CCM wamteue SAL-ngumi, mateke na matusi niliyopata kutoka kwa wana uchaguzi.com siwezi kusahau, na leo ndiyo hao wanaoongoza kumpiga mawe aliyekuwa mgombea wao kipenzi.
Sasa tusirudie kosa tulilofanya mwaka 2005 kwa kuendekeza ushabiki wa kijinga na kudharau watu wanaotupatia taarifa za upande wa pili wa wale wanaotaka kuwa viongozi wetu. Huu sio muda wa ushabiki na ubazaza usio na mantiki.
Lazima kila kiongozi tumpime vya kutosha na lazima tugeuze kila jiwe.
Naunga mkono hoja.Mods please ziunganisheni na ile nyingine manake bado iko moto inajadiliwa na huyu mkuu hana hoja yoyote ya kuijadili independently
Wandugu,
Binafsi nimegundua kuwa Burigi ni jasiri sana. Alichokifanya nimekuwa nakisikia sehemu kadhaa na mara zote "reaction" ya watu imekuwa karibu sawa na ya humu ukumbini.
LAKINI NAOMBA JAMBO MOJA,
Kwa nini tusiache "prejudice" halafu tukachunguza na kupima alichokileta hapa ukumbini halafu tukajua ukweli? Kuna wengi tu humu ama tunawafahamu watu waliofanya ama wanafanya kazi zinazowafanya wamfahamu Mh. Magufuli, kwa nini tusifanye utafiti halafu tukauleta hapa (kwa manufaa ya taifa letu)? Maana kama Mh. Magufuli anafaa basi asije kupigwa majungu tukakosa kiongozi mzuri, lakini pia tusije tukapata kiongozi bomu ikija kubainika kuwa tuliyoambiwa ni ya kweli.
Naomba kutoa hoja.
Kwa ile hoja ya burigi hivi hata kama kweli alifanya hivyo magufuli, ni kosa kubwa la kukosa urais? hata hamna haja ya kuchunguza amefanya makubwa sana, na vyote alivyosema burigi si kwamba kachukua pesa kajiwekea kwenye account yake kwa manufaa yake na familia yake bali ni kwa wapiga kura wake. na sio kama hawa wengine mafisadi wamechukua pesa nyingi kwa ajili yao binafsi. kwa mimi naona hakuna cha kufatilia hapa. ni watu wachache wanataka kumuharibia magufuli.