Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Burigi, Feb 11, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. B

  Burigi Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Nimekuwa ni msomaji zaidi kuliko mchangiaji kwa muda mrefu lakini nimekuwa nikishangaa sana watu wanapokuwa wanaongea vitu wasivyovielewa ama kwa ushabiki au kwa kutokuelewa.

  Mfano; Watu wameandika sana kuhusu uwezo wa Dr John Pombe Magufuli kuwa anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia vigezo dhaifu sana kuwa kila anapopewa Wizara hufanya vizuri nafikiri hicho si kigezo tosha kabisa cha mtu kuwa Rais.

  Kwa wasiomjua Mh. Magufuli nilitaka leo wamfahamu;

  Kwa ufupi tu kidogo ili na wao wapime kama kweli anafaa kuwa kiongozi wa nchi katika nafasi kubwa kama ya Urais.

  Magufuli ni mtu mwenye visasi sana na yupo tayari kuumiza umma wa watu katika kulipa visasi kwa wasio mjua Mh. Magufuli alipata kugombea Ubunge jimbo la Biharamulo mara mbili bila kupita mara zote aliangushwa na kina marehemu Phares Kabuye kwa kura nyingi sana.

  Aliweza kupata Ubunge pale tu Wilaya ya biharamulo ilipogawanywa majibo mawili yaani, Biharamulo Magharibi na Biharamulo Mashariki, hivyo akafanikiwa kuingia Bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo Mashariki wakati upande wa Biharamulo magharibi akiwa Mh. Choya.

  Baada ya kupata Ubunge aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo Mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuli alipata Unaibu Waziri, hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na kwa influence miradi yote mikubwa ya Wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri, watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote kama mnakumbuka vizuri alifikia kugombana na Mbunge mwenzake wa mashariki aliyefikia kusema kama Magufuli anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilichomuudhi sana Magufuli na kuhakikisha anafanikisha Mh. Choya anadondoka katika Ubunge wa Biharamulo Magharibi.

  Alifikia hatua ya kuwaleta wageni wakitaifa direct Jimboni kwake hata bila kupitia Makao Makuu ya Wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua Biharamulo Magharibi kwa kumnyima Ubunge mara mbili, hapa nataka kuwaonyesha kiongozi huyu mcheshi mchapakazi lakini mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee wanawake na watoto.

  Je, mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa Umma?

  Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form, mpokea form alijificha na alijitokeza wakati muda wa kurudisha form umekwisha akaonekana mrudisha form amerudisha form too late lakini, Mh. Magufuli alikuwa ameshawatisha viongozi wa chama na serikali Wilayani Biharamulo atakaepokea form za Bwana huyo basi yeye ni Naibu Waziri atahakikisha hana kazi watu wakatii na wakafanya dhuluma ya kumpitisha Magufuli bila kupingwa. Je, mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

  Mwaka 2005 kijana mdogo (jina nalihifadhi) kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF Wilayani Biharamulo alichukuwa form kugombea jimbo la Biharamulo Mashariki kwa Magufuli huku akiwa na support kubwa sana ya vijana, na alikuwa anaenda kumwamgusha Mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho, alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi Mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere, walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mme wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana.

  Alipofika Mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za Ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench Mh. Waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam.

  Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa gharama za mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli.

  Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa Waziri akafika akakaribishwa Mh. Magufuli kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. Magufuli akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa.

  Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi BLUE GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.

  Huyu ndiye Magufuli, je, anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?

  Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindishia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo. Huyu ndiye kiongozi anayeweza kuongoza watu?

  Mh. Magufuli alipigana na kulobby kwa nguvu zote kuhakikisha Chato inakuwa wilaya ili Biharamulo Magharibi wasifaidi mapato ya ziwa ambayo yanapatikana upande wa Chato na Nyamirembe na ndiyo kilichokuwa chanzo kikuu cha mapato cha wilaya ya Biharamulo. Lengo ikiwa ni katika kuendelea kulipa visasi kwa nini upande wa magharibi walikuwa hawampi kura kwa mihula takribani miwili, alifaulu na Chato ikawa wilaya mpya toka Biharamulo.

  Alipojikuta amesahau kuwa mgodi wa Tulawaka upo Biharamulo na haupo Chato alianza kuwatesa viongozi wa Wilaya ya Biharamulo kuwa ule mrahaba wa mwisho wa mwaka unaotolewa na migodi kwenye Halmashauri za Wilaya migodi ilipo, alitaka Biharamulo igawane nusu kwa nusu mrahaba wake na wilaya ya Chato.

  Huyu ndiye Mh. Magufuli. Je, rais anaweza kuwa na tabia hizi chafuchafu namna hii?

  Iliposhindikana akiwa Waziri wa Ardhi Mh. Magufuli kwa makusudi kabisa alibadilisha mawe ya mpaka kwa amri kama Waziri wa Ardhi kuiingiza Tulawaka ndani ya Wilaya ya Chato.

  Hivyo siku si nyingi Chato itadai Tulawaka ipo kwao na watapora haki ya wana Biharamulo swala hili lipo wazi kabisa, Halmashauri ya Wilaya kupitia Baraza la Madiwani limelalamika sana kuhusu ushenzi huu wa Magufuli, huyu ndiyo mtu anaweza kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

  Mwaka jana katika mpaka mwingine wa Biharamulo na Chato kijiji cha Biharamulo kinachopakana na Chato huko Kata ya Runazi wanakijiji waligundua kuna dhahabu na kuna wachimbaji wadowadogo Mh. Magufuli yupo analazimisha kubadili mipaka ili hiki kijiji kihamie Wilayani Chato na kumekuwa na mgogoro wa kiutawala unochochewa na yeye,

  Huyu ndiyo Mh. Magufuli anaepigiwa debe humu ndani kama anaweza kuwa Rais, Rais huangaliwa pande zote mafanikio na madhaifu kwangu mimi madhaifu ya MagufuLi ni mengi kuliko mafanikio.

  Mtakumbuka kilio cha nyumba za Serikali lakini huyu jamaa mkumbuke ni bingwa wa kusimamia wakandarasi na kutaka viwango katika ujenzi lakini yote tisa kumi Mh. anajenga ghorofa pale kwake anapoishi Oysterbay, nendeni mkaone maajabu ya mussa wajenzi mafundi mchundo hata ramani hazijapitishwa sababu wachoraji ni watu wa mitaani na mafundi ni vibarua mchundo huyu ndiyo Mh. Magufuli.

  Lakini skendo kubwa ya huyu bwana ambayo waandishi wangefuatilia kumjua vizuri ni jinsi alivyochezea mipaka ya Wilaya ya Biharamulo kubadilisha DN za vijiji na kusogezwa mawe yaliyoazinishwa na Serikali bila hata Serikali kujua.

  Kuzipeleka Chato hii ni hujuma kubwa na anastahili kujiuzulu waandishi nendeni mkawahoji wananchi na viongozi wa Wilaya Biharamulo mjue huyu mtu kitu alichofanya, mtu wa namna hii hawezi kuwa kiongozi kabisa.

  Huko jimboni kwake wafanyakazi wa Serikali wote walio against naye amewaumiza sana wengine hata kufunga vibiashara vyao vidogovidogo ili tu wakubaliane naye kifupi hajawahi kupita bila kupingwa ila amekuwa akipita kwa hila kubwa.

  Naomba kuwakilisha ili tumpime kwa pamoja.

  Je, tabia hizi zinaweza kumpa urais kweli?

  TUMPIME KWA PAMOJA HAYO NI MAONI YANGU TU.
   
 2. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Naanza kwa kusema ukiona zaidi ya nusu ya madai ni uzushi basi huna budi kuhitimisha yote ni uzushi, maadai ya mudai katika maada hii ni ya kuzua na yaliyo na mlengo wa kushoto.

  Historia fupi ya Biharamulo
  Biharamulo magharibi ni sehemu iliyo na asilimia kubwa kama sio zote ni wasubi na wakati mashariki yake ni mchanganyiko yani wasukuma,wajita,wazinza,wasumbwa nk, ktk eneo hili hakuna wasubi na kama wapo basi idadi yao haizidi 0,0001%.

  Msuguano
  Ghilba za wasubi dhidi ya wakazi wa mashariki hazikuanza jana ni giliba zao ambazo wanazitafsri leo kuwa ni visasi vya Mangufuli dhidi yao na wabaya wake kutake advantage dhidi ya Magufuli. Kiuhalisia kutoelewana kati ya mashariki na magharibi ni uhasama wa siku nyingi ambao waazilishi ndo hao magharibi.

  Ushuhuda
  1.Enzi za magharibi hakuna mwanafunzi aliyekuwa anafaulu kutoka mashariki kwenda sekondari kama ilikuwa ikitokea basi ni maramoja baada ya miaka takribani 5, watoto wa mashariki wameanza kuingia sekondari baada ya baraza ku-introduce mambo ya picha na uchakachuaji kushuka. Na hata hivyo wakati huo magharibi walikuwa na shule yao ya sekondari KAGANGO ambayo kwa plan ya mwanzo ilikuwa ijengwe ktk kijiji Nyamirembe enzi hizo , na hata hivyo ilihamishwa na kujengwa magharibi Na siyo hiyo tu hii KAGANGO ilikuwa marufuku kuchukuwa mtoto kutoka mashariki.

  2.Pamba inalimwa mashariki, jineli ipo chato na godauni za kutosha na bandari iko nyamirembe yapata km 5 kutoka chato, Lakini wakati wa ghiliba za wamagharibi, pamba wali i process chato na kuipack ktk marobota na kuacha kuhifadhi magodauni ya chato na nyamirembe na badala yake waliyasafirisha kutoka chato mpaka biharamulo yapata maili 50 hivi na kuyatunza huko na kisha kuyasafirisha kutoka biharamulo mpaka nyamirembe bandarini yapata maili 55 hivi. Lakini kumbuka chato na nyamirembe ni kama maili 5 na pia nyamirembe kuna godauni na pia chato kuna godauni.

  Barabara
  Mpango wa barabara wa awali yani kutoka mwanza hadi mreba bukoba ndo kama ilivyojengwa, ila hapo katikati ndo uchakachuaji wa ramani hiyo walipoichakachua na kusema ipite biharamulo. Hata ktk akili ya kawaida kuijenga barabara hiyo kupitia biharamulo ni sawa sawa na wewe kujenga barabara kutoka Dar kwenda mtwara na ukaijenga hivi .. kutoka Dar ukaipeleka Tanga harafu ukajenga daraja ktk bahari ya hindi kutoka Tanga hadi mtwara. Inge kuwa na sense kidogo kama hiyo barabara ingetokea shinyanga kupitia kahama hadi biharamulo na kuelekea bukoba napo nasema sense kidogo.

  Kosa la Magufuli
  Kosa lake kubwa Magufuli ambalo mie namulaumu nalo ni ..kuyasimamia mambo kwa mjibu yanavyotakiwa kuwa. Naamini kwa mtu yeyote mwenye ubinadamu japo kiduchu kama mbengu ya haladali angelifanya kama alivyofanya na anavyofanya magufuli. Makosa yapo na yapo ili mwanadamu ayatende, makosa ya magufuli ni makosa ya kibinadamu na si ya kihasidi(nduli).
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Madai ya kitoto
  Eti kuipa chato hadhi ya wilaya, kwa hiyo mleta maada alitaka indelee kuwa nini? hata hivyo hiyo ilikuwa plan ya serikali kuipa hadhi ya jimbo na baadae wilaya na ni madai ya kitoto maana wakati mashariki inakuwa jimbo Magufuli kama sikosei alikuwa mwalimu wa sengerema sekondari. Tatizo ni hiyo plan imekutana na mchapa kazi Magufuli ni kuiwaisha japo tayari imechelewa.

  Huyu anayelia na chato kuwa wilaya eti kuiua biharamulo kwa hiyo ana maanisha Magufuli ana njama pia ama aliapa kuiwa Mwanza kwa sababu Geita inakuwa mkoa ikijitenga kutoka mwanza kwa maana anayefanikisha haya ni Magufuli na je Magufuli chuki yake pia inaelekea kuua mkoa wa kagera kwa maana CHATO inajitoa kagera na kuunda mkoa mpya wa Geita?

  Eti fundi mchundo anajenga ghorofa, hoja gani hii wadau.
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Makali yenyewe imejaa 'half-truths' yaani uongo mwingi kisha ukweli kidogo ulioongezewa chumvi. Naweza kukosoa hoja zote za mtoa mada lakini nitaelezea chache.

  Kugombea Ubunge: Magufuli hakuwahi kugombea na kushindwa mara 2; alijaribu mara ya 1 mwaka 1990 na akashindwa na Mzee Kabuye, safari iliyofuata 1995 alishinda. Hakuwa na influence yoyote kutenganisha majimbo kwani wakati huo hakuwa na umaarufu wowote kisiasa, umaarufu alionao sasa umetokana zaidi na matokeo ya kazi zake akiwa waziri.

  Barabara: Hiyo barabara ya Chato sio barabara kuu bali ni zile za daraja ya vijijini na wala sio kweli kuwa Magufuli aliipindisha ipite kwake. Ujenzi wake ulienda sambamba na ule wa barabara kuu ya Muleba-Rusahunga ambao uliingiliwa na migogoro ya 'ulaji' hadi mkandarasi akasimamishwa; sijui kama hili nalo mnadai ni njama za Magufuli?

  Naona hizi ni siasa za 'ELIMINATION' kuelekea 2015; Jamani hebu punguzeni kurusha mawe, tangia hapo hapa jamvini wengi wanampigia chapuo ya Uwaziri Mkuu uraisi siyo saizi yake.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana JF: Hebu someni makala hii iliyotka katika gazeti la The African on Saturday wqiki iliyopita. Nadhani hii imetulia sana -- ikionyesha kwamba Magufuli si lolote bali ni mnafiki mkubwa:  Dr Magufuli: An authentic anti-graft crusader or creative publicity seeker?

  By Hilal K. Sued

  “A hypocrite is the kind of politician who would cut down a tree, then mount the stump and make a speech for environmental conservation.”
  - Adlai E. Stevenson – mid 20th century US politician


  The greatest majority of politicians of this world fall under this category. It’s no doubt human nature that manifests in various demeanours. And the most melancholy thing about human nature is that a man may guide others into the path of salvation, without walking in it himself, that he may be a pilot, and yet a castaway.

  Our own politicians, in particular those in the ruling party are good rostrum orators when it comes to assaults against corruption, but the assaults remain just where they were made – the rostrums.

  I was impressed the other day by an elderly participant at the symposium on the need for new constitution organised at the UDSM who said “I trusted Mwalimu Nyerere. When he used to say he hated corruption, you can clearly sense all his body parts speaking the same language. But not now.” Nowadays our leaders say they hate corruption with tongue in cheek.

  John Pombe Magufuli, the current Minister for Works has a reputation of portraying himself as a man of industry and diligence, a prolific anti-corruption crusader hence a “no nonsense minister.” Unfortunately he’s nothing of the kind, only that he has a penchant for publicity, and perhaps an eye to 2015. For being prolific does not necessarily mean one is an accomplished person.

  One has only to take a moment and ask: Since he became a cabinet minister nearly 15 years ago (it’s the second time now to hold the Works portfolio) – how many big cases on corruption he landed in court out his efforts? I’m first talking about cases, not convictions.

  The other portfolios he held during this period include that of Land and Human Settlements, and Fisheries. Everybody knows that Works and Land are among the most corruption tainted ministries.

  Granted, there is currently a case involving foreign fishermen caught fishing illegally within our territorial waters that is still in courts and that came into being during his stint at Fisheries. But that is not about corruption directly involving Tanzanians – the issue he loves to show that he is not a man for compromise.

  The case itself is not moving and is mostly becoming an embarrassment to the government, apart from being costly. The tons fish (tuna) seized was reported to be valued at more than 2 billion shillings – but had to be donated free to government institution for fear of going bad. And that came after the government incurred hundreds of million of shillings in refrigeration costs.

  So what started with a huge media publicity to show that Mr Magufuli was very much concerned in safeguarding our natural resources ended with a huge loss to the government. Besides, it’s doubtful whether the whole issue has been, or could be taken as deterrent or even warning to other foreign vessels fishing within our territorial waters. The seizure of the foreign vessel in question was done with the aid of South African navy as we do not have the means to do it ourselves.

  When he was at Fisheries he personally supervised the confiscation from poor fishermen illegal fishing gear including gillnets (small-meshed nets). Many said why didn’t he first go to the necks of the local manufacturers or importers of such nets?

  That is one. Secondly there has always been talk by CCM administrations to bring to a halt the misuse of official cars and the importation of luxury vehicles for its officials. However all this lacked willpower and spirit behind, and remained just that – talk.

  Several years ago as minister for Works, Magufuli, whose portfolio included the administration of government vehicles wanted to make history by being seen to act tough on the vehicles misuse by government officials. He launched a crackdown on them, so he said. He announced that some of these officials were even found to have turned the official vehicles under their charge into their private property by fixing onto them private number plates and painting their own names.

  The crackdown, that started with a bang and widely reported by the media ended with a whimper. No one was arrested, prosecuted, suspended or even sacked as a result of the crackdown.

  Wait for more. Several years ago, Magufuli, with full media coverage, was shown on TV speaking at a meeting with some TANROADS workers in which he accused agency officials of embezzlement of public money. He disclosed that there was evidence TANROADS officials purchased cars at almost twice their normal prices, and asked the agency to investigate further and book the culprits.

  It would have been better had he delayed his public castigation of the agency until such time the investigations were over, and then call the media to announce that several TANROADS officials “will tomorrow appeared in court to answer charges of embezzlement, corruption… “

  Since nothing came out from his utterance, then it is easy to see that it was only designed for public consumption, that’s all. And that has always been the modus operandi of many of our leaders – media publicity followed by lack of action.

  And as Minister for Lands and Human Settlement during the last years of Mkapa Administration, newspapers reported him being enraged by what he termed “the widespread habit” of tenants passing the rented NHC residences to their descendants and that he was ordering a verification exercise on all NHC buildings.

  Many of us know that in NHC the bulk of the dirt is the thriving business of tenants leasing the quarters to other people illegally, making big money in the process. And this is done with the full knowledge and connivance of NHC officials. Many Tanzanians know about such deals that have been going on for years, including Magufuli.

  The illegal transactions were so widespread, and the public knowledge of them so open, that people came to accept the goings-on as entirely legal. Change of tenancy to an NHC flat or shop, without adhering to the normal procedures is often accorded legal status by the corporation’s officials – at a price of course. There has been no secret about that at all.

  I also find it odd that Magufuli was only enraged by “the widespread habit” of tenants passing the rented NHC residences to their descendants, and not by the widespread corruption among the NHC officials behind the shenanigans. And was Magufuli aware that the “verification” exercise on the legality of NHC tenancy contracts was being undertaken by the same NHC officials, a fact that ensured its becoming fruitless? The fact that nothing came out of the exercise followed by huge silence from him shows that he’s not a serious corruption crusader.

  Perhaps the biggest hypocrisy from Magufuli was his agreeing to be part of one of the greatest ‘sins’ committed by the CCM government – the decision to sell government quarters to civil servants. This was the brainchild of the then President Mkapa and came up at the dawn of his second term.

  The decision immediately drew a lot of criticism, with many people, including politicians, activists and other people, saying it would be burden to the government to house its incoming civil servants. It was as if the third phase government thought it was going to be the last government in this country.

  But what angered many and viewed as ‘unforgivable sin’ on the exercise was its total secrecy – who were the buyers, at what prices and so on. Many said that if at all, the houses should have been sold through public auction, a prescribed procedure of selling government property. Others said the houses were a national resource and the property of all Tanzanians not just the few civil servants.

  However, information that seeped into the media explained the reason behind the secrecy – that some heavyweights had bought houses in prime areas at given away prices – in some cases even less than five per cent of their economic values. It was also reported that some houses were sold to un-entitled persons, or that nepotism ruled over the sales.

  Three years ago one weekly newspaper in Kiswahili reported that John Magufuli was alleged to have personally supervised the selling of some 8,000 government houses instead of the Tanzania Building Agency (TBA).

  The paper further alleged that some houses were sold to his brother even though he was not a civil servant. Magufuli was also said to have also pressurised the TBA to sell a unit at the Kinondoni Flats, to his nephew after arranging short-term employment for him at TANROADS.

  It was further reported that some government officials who bought the houses have not paid for them in full, despite the give-away prices they were given.

  This was later verified in the 2009 Parliamentary Budget session when the Minister for then Infrastructure Development, Shukuru Kawambwa told MPs that the government had repossessed 125 houses it had sold to civil servants between 2001 and 2005.

  He said the repossession followed the discovery of a massive breach of regulations and procedure governing the sales. He said 34 of the houses were in areas reserved for hospitals, whilst others were inside sensitive areas including police and prison camps.

  Two weeks ago Magufuli was at it again. He announced to the press that he had unearthed fraud involving sh 5 billion that was to be paid out to ‘owners’ of 61 houses that were found to be ‘non existent’ but earmarked for demolition to pave way for the expansion of roads in Dar es Salaam.

  He said he would refer those involved in such dirty deals to appropriate authorities for further action. That ends it. Why didn’t he wait until investigations are complete for court action? Nothing will come of it as he will not speak about the subject again. You wanna bet?

  And this week he decided that that the life size advertising billboards along our roads were an eyesore to him and has threatened to demolish them saying their erections had infringed road reserves.

  He threatens to frustrate USD 50 million business and billions of shillings of income to city and other council authorities, as these roadside were erected from legal contracts between them and advertisers. Why does he seem to loathe the rule of law?

  ends   
 6. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wanaompenda Magufuli wana-refer mazuri aliyowafanyia Watz, yapo na yanonekana ...wanavigezo/data!
  Wewe unatoa maneno mengi kuhusu mabaya ya Magufuli ni maneno matupu yasiyo na ushahidi wa wazi, ni mambo unayafahamu wewe tu na ushahidi wake unao wewe mwenyewe basi!!
  Nakushauri wakati mwingine, huna hata haja ya kuandika mambo mengi; unaweza kuandika mistali hata miwili lakini ukaeleza ushahidi wa wazi juu ya unalosema na utaeleweka...vinginevyo unabaki kuonekana mtu mwenye roho mbaya, mzushi, wivu, mchawi nk
   
 7. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  We mtu mpaka unafikia hatua ya kuandika karibu paragraph ishirini na tano, unamzungumzia mtu mmoja tu "MAGUFURI" kwani watanzania hawana uwezo wa kutambua nani anafaa na nani hafahi? Mkuu wakati mwingine ni vizuri kuwatendea haki binadamu wenzenu hata kama una bifu nao. Ni mtu gani kwenye akili timamu ambaye anaweza kubeza beza jihudi za Mh.MAGUFURI katika utendaji wake wa kazi, ni wizaragani ambayo amewahi kupewa akaonekan ANAPWAYA - jaribu kuwa mkweli hapa - Mzalendo huyu ni all weather; sasa hulka yake yakutokuwa a no nonsense guy ndio achukuliwe kwamba hafahi!!!!

  Je unataka kuwapigia debe viongozi wengine ambao hawajibiki chochote, na wala hawajulikani kama wapo wizarani kweli au wemekwenda likizo, wewe hao ndio unawaona ni fresh wanaweza kukabidhiwa nchi kama Kiongozi mkuu.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mkuu huwa naogopa kuchangia sana mada za magufuri kwasababu me natoka Biharamulo Magharibi na ye anatoka mashariki na ninajua mambo mengi kumuhusu. Naongeza machache uloyasahau. Pale chato kuna nyumba za halmashauri ya wilaya,, yeye alilazimisha zijengwe kwenye viwanja vya babake na amezikodisha kwa serikali anavuna pesa kila mwezi. Aliwahi kuwa na ugomvi wa mkuu wa wilaya wa kwanza wa chato kwa kukataa kukaa kwenye hizo nyumba hadi sasa sijui yule mkuu wa wilaya aliishia wapi.

  pili; Wakati generator za umeme zinaletwa Biharamulo Magharibi bado ilikuwa wilaya moja na chato lakini Magufuri alitaka zijengewe kule kwake hadi Mzee mkapa alipoingilia kati ndo zikajengewa magharibi. Na wiring ya magharibi ilitangulia kumalizika kama miezi mitano kabla ya Chato lakini yeye aligoma umeme usiwashwe hadi chato wamalize. na mwaka jana walikuwa na mgao wa umeme wa kufa mtu na alilazimisha chato ipate masaa kumi na manne mchana kutwa na kule magharibi wakawa wanapata masaa kama sita hivi usiku.

  Kama hitoshi, Biharamulo ilikuwa katika harakati za kuwa Mkoa na ilikuwa ikigombea na Chato lakini kwa vigezo Chato wahakuweza kuipiku Biharamulo alilofanya Magufuri ni Kulazimisha mkoa upelekwe Geita ingawa geita hawakuwa wameomba mkoa lengo ni kuiua Biharamulo.

  Wakati Wilaya ya chato inaanzishwa, wafanyakazi wengi walokuwa Biharamulo walihamishiwa chato nadhani ni wakati amelazwa kule ujerumani baada ya kupewa sumu. Na aliporudi aliamuru wale wafanyakazi wahamihswe akisema mhawezi kukaa na wasubi na wahaya kwani walimchafua sana.

  Juzi kuna lami ilokuwa inajengwa Biharamulo kuunganisha Lusahunga na Muleba lakini baada ya uchaguzi ilifungwa kwa madai kuwa hawana pesa hadi hapo baadaye, magufuri alipokuwa katika ziara za kuwashukuru wananchi wake kwa kumpitisha bila kupingwa mpakani mwa chato na Biharamulo paitwapo Buziku wananchi wake walimwomba lami walau na hapo ilpite alisema "tatizo ni wale watu wa Biharamulo ni wabishi nataka niwaoneshe kuwa tunaweza na kwa taarifa yenu ile lami yao imefungwa" sisiemi haya kutoka hewani kwani kuna jamaa alikuwa akisikiliza hotuba na aliirekodi!

  Siandiki haya kwa chuki sina chukimnaye ila ni maoni yangu tu.

  Magufuri ni mchapakazi hasa na asiyeogopa kitu anapokuwa katika kazi na vigezo vizuri lakini Tuendelee kumpima!
   
 9. Mhubiri

  Mhubiri Senior Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ukiendelea kusimama palepale utakuwa unakosea sana.Utendaji wa Kikwete ulikuwa haujulikani kabla hajawa Rais.Hivyo mashabiki wake wengi walikuwa ni wafuata mkumbo.Walimpenda ama kwavile alikuwa yuko 'simple',ni mtu wa kujichanganya na watu,ama walivutiwa na charisma na popularity yake.Magufuli ni case tofauti kwa sababu utendaji wake unajulikana tayari hata na watu wa vijijini.Tunajua mapungufu yake pia.Tulishajua jinsi alivyosimamia zoezi la uuzaji wa nyumba za serikali,tunajua alivyobomoa kituo cha mafuta Mwanza na kama madai ya Burigi ni sahihi basi walau tutajua kuwa kumbe Magufuli kuna mambo fulani fulani,yasiyofaa ameyafanya jimboni kwake.Utendaji wa Kikwete ungekuwa exposed walau nusu tu ya huu wa Magufuli,naamini angeshinda lakini siyo kwa ile asilimia 80+.
  Kwahiyo mkuu,hawa ni watu tofauti,wenye sifa tofauti.

  Kusema kwamba hakuna binadamu asiyefanya makosa,simaanishi kuwa natetea wafanya makosa,kwamba wanafanya hivyo kwavile wao ni binadamu hivyo wameumbwa kufanya makosa.HAPANA.Ninachomaanisha ni kupima dhamira ya mtendaji,kupima yale makosa na kuangalia uzito wake.Siwezi kwa mfano kusema,eti swala la Mkapa la kujibinafsishia kiwira au ishu ya Richmond ni makosa ya kibinadamu hivyo wananchi tusipige kelele,tuwasamehe.HAPANA.Lakini ukija hapa ukasema Magufuli hafai kuwa kiongozi,kwavile ana kimada,nitakujibu mkuu!

  Unauliza mazuri yaliyofanywa na Magufuli?Mbona yako mengi mkuu?Naamini utakuwa unayajua maana hata jinsi ulivyouliza maswali yaonyesha unajua.
  Kwa uchache:
  Ana guts,anafanya maamuzi kama kiongozi bila kumuangalia nyani usoni.Mchapakazi,mbunifu na mfuatiliaji mzuri wa maagizo yake.Mfano:Akiwa Waziri wa Ujenzi wa Mkapa,alimshauri bosi wake Rais Mkapa,badala ya kutegemea fedha za wafadhili,watenge kidogo pesa kutoka mapato ya ndani ili ziende kwenye ujenzi wa barabara. Alisimamia vizuri sana swala la ujenzi wa barabara.Alikuta wizara imeoza,TANROADS wanalipana mamilioni,kazi hazifanyiki.Akawabana TANROADS,wakandarasi na matokeo yake yalionekana.
  Akiwa ujenzi hukohuko wakati wa Mkapa,aliyapa namba za serikali magari yote ya serikali yaliyokuwa na namba binafsi na kutumika ndivyo sivyo.Zoezi lililomjengea maadui wengi.
  Haya ni machache,lakini yako mengi yenye kuonyesha uthubutu wa Magufuli hukohuko ujenzi,ardhi na hata Mifugo.
   
 10. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa nikitizama ITV habari jioni ya leo,nikamuona mhe. John Pombe Maghufuli akiwataka wale wabunge wa Dar es salaam wanaojidai wana uchungu sana na wananchi wa kigamboni waende ofisini kwake awakabidhi kivuko wakiendeshe wao kwa faida kama wanaweza.

  Kwangu mimi,mheshimiwa Maghufuli ameonyesha msimamo ambao kwa muda mrefu sasa tumeshindwa kuuona hadharani kwa viongozi wetu wakubwa.viongozi wetu wengi wamejionesha kujawa na propaganda na harakati za kisiasa ambazo mwishowe zina lengo dhahiri la kutetea maslahi yao binafsi kwenye jamii na ulingo wa siasa kwa ujumla.

  Alichoonesha mheshimiwa maghufuli ni msimamo juu ya jambo lenye mtazamo wa maendeleo kabisa kwa wananchi,hata kama wengi wetu tumeamua kulitizama kwa mtazamo wa emotions zaidi badala ya kufikiri vizuri.

  Wananchi wote wanaopinga ongezeko la nauli ya pantoni pale kigamboni inawapasa kufikiria mara mbili kwanza.Ivi ni nchi gani duniani kuna nauli ama gharama ya kitu chochote isiyopanda kwa miaka 14 mfululizo!?Ni dhahiri kuwa sisi wote tungependa bei za vitu na huduma zote tutumiazo kila siku zibakie hivyo daima dumu.Je hili litakaa liwezekane??nakataa.

  Pili, wananchi wanatakiwa kujua kuwa huduma kama hii ya kivuko ni 'public good' kama waitavyo wachumi.Ni huduma ambayo inatumiwa na sisi wote na kwa hivo lazima italipiwa kwa njia moja ama nyingine kwa sababu tunaihitaji.Hivyo basi,yeyote anayepinga kupandishwa kwa nauli ya hii pantoni,basi awe tayari kwa muda wote kuongezewa kodi nyingine,sehemu nyingine ili kusaidia uendeshaji wa kivuko hiki,iwe ni kupitia PAYE,VAT ama kodi nyinginezo.Tofauti tu hapa ni INSTANCE ya kutokea kwa hii TAX BURDEN.

  Tatu,tunapaswa kujiuliza,je hawa wananchi na viongozi wa siasa wanaopinga ongezeko hili la nauli iwahusuyo watu wachache tu wa kigamboni wana uchungu kweli na wananchi wa taifa hili??Je walikuwa wapi siku zote sukari ikipanda toka shilingi 1400 kwa kilo mpaka 2600 kwa kilo ndani ya miezi michache tu!?wakati rais kikwete akiingia madarakani(miaka chini ya 7 iliyopita),nauli za daladala Dar es salaam zilikuwa wastani wa sh.150 kwa safari za karibu,sasa ivi ni zaidi ya mara mbili ya bei hiyo na hawa 'wapendwa wananchi' na viongozi wao wanafiki hawajawahi kuleta mgomo ama kusimama kuipinga hiyo serikali ya mhe. Kikwete iliyowaletea hii dhahma yote kwa kutokuwa na sera thabiti za kiuchumi.

  Ni dhahiri basi,wale wote waliosimama katika jina la kupigania haki za wananchi wa kigamboni na kumpinga mhe. Maghufuli hawajui wanalopigania na zaidi sana hawamjui adui yao.

  Hata baba akichekacheka sana na wanawe nyumbani dunia ndiyo itawafundisha vizuri na wakati wanajifunza inaweza kuwa jioni mno.Nchi yetu imekuwa masikini kwa sababu ya kukosa viongozi wenye msimamo wa kupigana dhahiri dhidi ya maadui wetu wakubwa ikiwamo ufisadi uliokithiri na matumizi mabaya ya rasilimali za serikali.

  Maghufuli-umetenda vema.
   
 11. m

  msemakweli Tanganyik Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 5, 2013
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nimekuwa msomaji zaidi wa Jf kuliko mwandikaji lakini naomba nitoe maoni kidogo juu ya hii hoja. Ndugu mtoa hoja tunashukuru kwa ujumbe uliojaribu kuutoa kwa wana jf ingawa umesahau kuwa Dr. Magufuri watanzania hawajamfahamu leo.

  Ninao wasiwasi kuwa wewe unahisi kwamba Magufuli amewafanyia makubwa wapiga kura wake akiwa kama mbunge jirani ambapo wapiga kura wameona, sasa unaanza kuhisi kuwa akiwa Rais itaumia zaidi na umeanza majungu yako. Ufanisi wa mbunge katika jimbo la Biharamuro mashariki umekuathiri nini katika jimbo la Biharamuro magharibi?

  Dr.Magufuri alipomaliza digrii yake mlimani kazi yake ya kwanza alikuwa Mwalimu shule ya sekondari sengerema na alifungisha somo la hesabu na fizikia.Kunako mwaka 1982 wanafunzi walifanya mgomo na kuharibu vifaa vya shule na kupiga waarimu hivyo wanafunzi wote wakapewa suspension kwa miezi kadhaa ili uchunguzi ufanyike kubaini waliosababisha mgomo huo.

  Wakati waliporudishwa shuleni wakiwa wamebaini waliongoza mgomo na hatua kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufukuzwa ilikuwa imebaki miezi mitatu tu wanafunzi wa kidato cha nne wafanye mitihani ya taifa.Mkuu wa shule muda huo bwana Lukas Thomas Marwa aliwaomba walimu wawasamehe wanafunzi na wawape ushirikiano kwa sababu bila hivyo maisha yao kielimu yalikuwa yameshaharibika.

  Katika waalimu waliojitolea kufundiha hadi usiku wa manane mmojawapo ni John Pombe Magufuri wakati huo wanafunzi wakimwita Bwana mdogo kwa jina la utani kutokana na umbo lake dogo ukilinganisha na umri wa wanafunzi wa wakati huo. Matokeo yalipotoka mwanafunzi wa kwanza kitaifa katika somo la somo la fizikia alitoka Sengerema.

  Magufuri baada ya kumaliza digrii yake ya pili hakurudi kufundisha kama ilivyo kawaida ya wengi wetu labda wakati huo kwa sababu ya wazi kuwa mashirika ya umma yalikuwa yanalipa mshahara mkubwa kuliko serikali akaajiriwa na Nyanza cooperative union kama meneja mwendeshaji.

  Lile shirika wakati huo lilikuwa lina nunua mazao kutoka kwa wakulima hasa pamba na kupeleka kwanye vinu vyake vya kuchambulia lakini shirika hilo lilikuwa kama mali ya kundi fulani hivi la watu kwa hiyo watu walikuwa matajiri kwa kununua pamba hewa na kutumia magari yaliyokuwepo ya kusombea pamba kama yao binafsi kwa kupakia abilia na mizigo.

  Magufri alipofanywa meneja uendeshaji miradi ilileta tija kwani ununuzi wa pamba hewa na chafu ulikoma, kukopwa kwa wakulima kwa kutokuwa na fedha za kuwalipa kulikoma,Magari yakadhibitiwa na hayakuwa kama miradi ya watu tena.Ukweli hakupendwa na watu hasa hao waliokuwa wanafaidi.

  Kwa hayo machache ninashawishika kuamini kuwa Dr.Magufuri anaweza asiwe mzuri sana kufuatana na vyegezo mbalimbali vya kila mtu atakavyokuwa ameviweka lakini kwa kulinganisha na aliyokwishafanya hapo nyuma kabla hajawa Naibu waziri na waziri kamili ukizingatia pia naye ni binadamu wa kawaida ambaye angependa maisha mazuri kama wenzake wanaokuwa matajiri miezi michache tu ya unaibu waziri basi naona sababu ulizozieleza ndugu yangu Burigi hazimfanyi Dr. Magufuri awe mbaya kiasi hicho.

  Na labda nimalizie kwa kusema kuwa mimi si mwana CCM ambacho Dr. Magufuri anaweza kugombea kama atanuia na nafahamu kuwa hapendwi na baadhi ya wakubwa kwa sababu utendaji wake wakati fulani unagusa maslahi ya watu hao.
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kama ambavyo mtoa mada alivyoonyesha Dr Magufuli ni mtu hodari sana kumanipulate sheria ili kutimiza malengo yake hata kama wananchi wataumia vipi yeye hajali. Kwa bahati mabaya sana kwa kuwa watanzania wengi ni wavivu kusoma hususna kusoma sheia basi Magufuli akitamka kuwa nafuata sheria basi wengi huamini kuwa nafuata sheria lakini anacofanya Dr Magufuli ni kugeuza sheria kama menu ya hoteli ambapo mlaji huchagua chakula akipendacho na kuacha kile asichopenda.

  Sisi wakazi wa Jimbo la Ubungo tunaopakana na barabara ya Morogoro yametukuta ndio maana tunamfahamua sana huyu jamaa jinsi alivyotufanya tuishi kama tunaishi uhamishoni.

  Kati ya 1970 na 80 Tanzania chini ya Mwalimu Nyerere ilitekeleza sera ya vijiji vya ujamaa kwa kuwahamisha kwa nguvu watu toka katika makazi na mashamba yao na kuwahamishia katika vijiji vipya vua ujamaa vilivyoanzishwa. Katika utekelzaji wake Serikali ilifiikia hatua ya kuwachomea nyumba wananchi waliokataa kuondoka katika makazi na mashamba yao na kuahmia katika vijiji vya ujamaa vilivyoanzishwa. Nyumba na mashamba vilichomwa moto, mashamba kutelekezwa ili mradi watu wahamie vijiji vy ujamaa.


  Katika mikoa mbali mbali vijiji vya ujamaa vilianzishwa kando kando ya barabara kuu za nch (Highways); katika Jimbo la Ubungo baadhi ya vijiji hivyo ni pamoja na vijiji vya ujamaa vya Kimara, Temboni, Mbezi, Kibamba, na Kiruvia vilivyoanzishwa kando kando ya barabara ya Morogoro na wananchi kuhamishiwa katika viji hivi na kugawiwa ardhi Serikali a Jamahuri ya Muungano wa Tanzania toka pembezoni kabisa ya barabara Morogoro.

  Wakati wa ugawaji huo wa ardhi katika vijiji hapakuwepo kitu kama hifadhi ya barabara. na kuthibitisha hilo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwapatia hati za kumiliki ardhi kwa miaka 99 baadhi ya wananchi waliohamishiwa, kuhamia katika vijiji hivi kwa ajili ya kuishi na kulima. Sasa kama Serikali iliwahamishia wananchi katika aradhi hiyo inayoitwa hifadhi ya barabara kwa nguvu na kuwagawia aradhi hiyo na kufikia hatua ya kuwapatia hati miliki ndani ya ardhi hiyo ya hifadhi ya barabara; nani mwenye kosa ni wananchi au Serikali yenyewe?


  Mwaka 1999 Tanzania ilipitisha Sheria ya ardhi ya vijiji namba 4 na 5 za 1999, Kifungu cha 15 cha Sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya 1999 ikinatamka kuwa "Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya tarehe 01 Januari 1970 na tarehe 31 Desemba 1977, kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu kwa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo......

  Aidha kifungu cha 16 kinatamka kuwa "Kwa madhumuni ya kuepusha mashaka na ili kuwezesha kuwapo kwa usalama wa miliki ya ardhi na hivyo kuchangia maendeleo ya ardhi ya kijiji, masharti ya Kifungu cha 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na Halmashauri ya Kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya tarehe 01 Januari 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii na kwamba badala ya tarehe zilizotajwa katika kifungu cha 15, kumewekwa tarehe kati ya tarehe 01 Januari 1978 na tarehe ya sheria hii kuanza kutumika".

  Vilevile Sheria ya barabara ya Morogoro ya 1967 inatambua kuwa eneo la hifadhi ya barabara kuu hapa nchini ni Mita 22.5 kila upande kutoka katikati ya barabara. Aidha Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 iliongeza eneo hilo kufikia Mita 30 ikimaanisha wananchi wana haki ya kulipwa fidia kwa ardhi ilyoongezwa kuwa hifadhi ya barabara.

  Aidha Kanuni za barabara za sheria hiyo zilizopitishwa mwaka 2009 zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara zote kuu hapa nchni hautapungua Mita 3.25. Hivyo upana wa hifadhi ya barabara wa Mita 30 unao uwezo wa kuzalisha njia za barabara mpya (Mita 30 gawanya kwa Mita 3.25= 9.2)

  Hivyo eneo halali la hifadhi ya barabara hapa nchini linao uwezo wa kuzalisha njia 18, yaani 9.2 kila upande katika barabara ya Morogoro kabla Dr Magufuli hajatumia ubabe wake kuwabomolea wafikia wananchi walioko nje ya Mita 30 kila upande.


  Lakini kutokana na dharau kwa maisha ya binadamu na ubabe huku Dr Magufuli akifahamu kuwepo kwa sheria iliyotajwa hapo inayolinda ardhi ya wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia (alikuwa mmoja wa wabunge na naibu waziri wakati sheria ya ardhi ikipitishwa mwaka 1999); mwaka 2001 wakati wa ukarabati mkubwa wa barabara ya Morogoro alimuagiza mkandarasi aitwaye Scabphil Colas kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi walioko nje ya eneo halali la hifadhi ya barabara yaani kuanzia Mita 30 hadi 120 toka katika ya barabara kupiga nyumba hizo alama ya X, kupanda mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara.

  Toka mwaka 2001 wananchi wa maeneo haya wamekuwa wakiishi kama wako uhamishoni kwa kushindwa kutumia ardhi yao kujiletea maendeleo na kujipunguzia umaskini. Ndio maana katia ya Ubungo na Kibaha huwezi kupata huduma zozote muhimu kama vile mabenki, ATM, Supermarket n.k.

  Ili kuonyesha naman Dr Magufuli anavyoweza kutumia madaraka yake vibaya, alipoteuliwa tena kushika wadhifa huo 2010/11 aliiagiza TANROAD kuwelea alama za X nyumba zote zilizoko ndani na nje ya eneo halali la hifadhi ya barabara yaani nje ya Mita 30 hadi Mita 120; aidha mara kwa mara amekuwa akiwapotosha watazania kuwa wananchi hawa ndio wanaosababisha msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro. Kama tulivyoona eneo halali la hifadhi ya barabara la Mita 30 lina uwezo wa kuzalisha njia mpaya za kupita magari 9.2 kila upande wa barabara. Je ni kweli kuwa wananchi weny nyumba zao nje ya Mita 30 wanansababisha msongamano wa magari ilihali Dr magufuli na Serikali haijweza kujenga hata njia moja mpya ya magari katika eneo halali la hifadhi ya baraba la Mita 30? Huu kama sio upotoshaji wenye nia mbaya kwa wananchi ni nini?

  Huyo ndio Dr Magufuli anayeweza kujua sheria fualani inalinda haki za wananchi lakini kutokana na mapaungufu ya kikatiba yaliyopo hapa nchini akatumia ubabe kufanikisha malengo yake ya kisiasa bila ya kujali athari zinzowapata wananchi wengine kwa maelfu/

  Mara kwa mara Dr Magufuli maekaririwa akidai kuwa nyumba zote zilizowekewa alama ya X zilizon dani na nje ya eneo halali la hifadhi ya barabara zitabomolewa pasipo fidia yoyote kwa kuwa wananchi wakilipwa fidia ni kuitia hasara serikali.

  Sasa hawa wananchi ambao walichomewa nyumba zao na kuhamishiwa katika vijijivya ujamaa kanda kandao ya barabara ya Morogoro wana makosa gani; kama kweli walivamia eneo hilo mbona Serikali anayoitumika imekuwa ikiwapatia hati miliki?


  Kama kweli Dr Magufulia ana uchungu na kupotea kwa fedha za serikali alipaswa kuwa maeshajiuzuru zamani kwani amekuwepo katika mabaraza ya mawaziri ambayo yamehusika na upotevu mkubwa sana wa fedha za watanzania k.m IPTL, EPA, MEREMETA, TANGOLD, RADA, RICHMOND, DOWANS n.k.
   
 13. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni muhimu kupata taarifa kama hizi kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wetu, na si vizuri kuwakatisha tamaa wanaotoa taarifa hizi na kuwapa watu fulani utakatifu wakati pengine hawana.

  Nakumbuka mwaka 2005 watu walivyokuwa wamepagawa kwenye forum ya uchaguzi.com (kama JF ya leo), ulikuwa huwezi kusema neno lolote watu wakaelewa na ulikuwa unaitwa majina yote ya usaliti hapa duniani ukimkosoa mgombea wao kipenzi. Niliandika makala kuhusu sababu 15 kwa nini CCM wamteue SAL-ngumi, mateke na matusi niliyopata kutoka kwa wana uchaguzi.com siwezi kusahau, na leo ndiyo hao wanaoongoza kumpiga mawe aliyekuwa mgombea wao kipenzi.

  Sasa tusirudie kosa tulilofanya mwaka 2005 kwa kuendekeza ushabiki wa kijinga na kudharau watu wanaotupatia taarifa za upande wa pili wa wale wanaotaka kuwa viongozi wetu. Huu sio muda wa ushabiki na ubazaza usio na mantiki.

  Lazima kila kiongozi tumpime vya kutosha na lazima tugeuze kila jiwe.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kitila, Thanks for sharing your experience na pia kwa angalizo...

  Burigi ana rights za kutoa maoni yake na mtazamo wake kama tulivyo wengi ndani ya JF.... lakini nachelea kusema kwamba the guy is biased.

  Nimeona kama vile ameamua kuwa m-biharamulo peke yake na kutuacha watanzania wengine wote ambao tumefaidika na Magufuli. Pia nadhani ni vyema kukubali kwamba hakuna kiongozi yoyote asiye na kasoro na kibaya zaidi hajawahi kutokea kiongozi yoyote duniani ambaye hana visasi, kwani kisasi ni nini?? ina definition lakini wengu wetu hutumia baadhi ya maneno kufikisha ujumbe tu.

  Mimi na wewe tuna visasi na watu wasiopenda maendeleo au kufanya kazi; mimi nina visasi na watu wanaodhani ati watanimaliza tu simply because i differ with them, siwezi kuwa mnafiki niseme sina visasi wakati najua wakinikama watanimaliza.... NADHANI UMENISOMA MAANA YA "VISASI" NILIVYOITUMIA HAPO

  Magufuli is way beyond comperation na watu kama Mrema, JK nk... najua ana kashfa zake kama ile ya Sundi Malomo, yule shemeji wa Bujiku na hata ya pesa na nk... hizo ni kashafa, kwangu hazijathibitika na siwezi kumuondoa kwenye top list kwani siwezi kumlingalisha na lowassa, mwandosya, rostam, mkuchika, kinana, nchimbi, makamba, Jk nk

  Burigi anasahau kwamba anakanyaga kila kilomita kwenda kwao biharamulo kwa faida yake na tunada ma magufuli, ni burigi huyuhuyu anashindwa kuelewa kwamba huyo magufuli ameacha positive impact kila alipopita na hasa kwenye kudai na kutetea haki na sheria kufuata mkondo wake.

  Kwa sisi tunaoishi kimbiji, zile sleepless nights zimerudi na wavuvi harmu tuna wasiwasi wanatumia mabomu ambayo hata wanajeshi hawana (makubwa sana) ... ni wkasababu ile wizara ya vitoweo, imerudia kuwa wizara ya vitoeo... na utaona tutakavyokwisha sasa

  Sijui nisemeje au niiweke vipi post yangu, lakini nasikitika sana burigi ameamua kutulazimisha tumjue magufuli kwa kupitia biharamulo pekee wakati yeye magufuli hatumii hata 5% ya muda wake huko

  Hilo la kusema anakuja na wageni hapiti wilayani, nasema inategemea purpose ya visit, kama ni ya kiserikali au kisiasa... TUSILAZIMISHE WATU WAFANYE TUTAKAVYO ILI NA SISI TUWE WA MAANA

  TO ME BURIGI IS A TYPICAL TANZANIAN, GOOD IN DEFAMING PEOPLE, FOR A FEW COINS AND VERY BAD IN PERFORMING HER/HIS DUTIES

  THIS THREAD ONCE AGAIN HAS UNEARTHED TYPICAL WA-TZ... KUSEMANA SEMANA KAMA WATU (AS INDIVIDUALS) BADALA YA KUWA GREAT MINDS KUDISCUSS ISSUES

  SHAME ON BURIGI AND SHAME ON US WHO ALWAYS WISH TO DISCUSS PEOPLE INSTEAD OF ISSUES
   
 15. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Haya ni madai mazito sana.

  Kama ni kweli jamaa amefikia hatua ya "Kukidnap" watu ili akae madarakani basi jamaa hafai.

  Haijalishi amefanya nini kwa Taifa hili yeye akiwa kama kiongozi, kwani kitendo cha kufanya mbinu za kimafia na kuvunja sheria za nchi kwa ajili ya madaraka kwa kweli hakikubaliki.

  hii inanikumbusha skendo ya "Richard Nixon" na issue ile ya Watergate. Watu makini hawawezi kufurahishwa na uongozi wa visasi na Uvunjaji wa sheria kwa ajili ya "Power at any cost".

  Wana JF tuwe makini sana na Viongozi wa CCM na wale wa UPINZANI, inavyoonekana tumekata tamaa kabisa kiasi kwamba akitokea kiongozi mmoja akafanya kajambo fulani kazuri basi tunamkubali moja kwa moja, inabidi tuwachunguze watu hawa, tuweke rekodi zao wazi, tuwapime kwa nyendo zao hapo ndo tutakuja kujua kwamba fulani angalau anafaa.

  Madai aliyoleta mwanzilishi wa mada ni madai mazito, na ushahidi ukipatikana muheshimiwa hana budi kufikishwa katika vyombo vya sheria.

  JAMANI TUSIAMINI KIRAHISIRAHISI TUWAPIME HAWA, TUWACHUNGUZE KABLA HATUJAWAPA DHAMANA KUBWA ZA UONGOZI WETU.
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Asante bw. Burigi kwa taarifa hizi kuhusu zinazoonyesha upande wa pili wa Dr. Magufuli.

  Kuna mambo ambayo kwa kweli hauhitaji kuwa mtaalam sana kujua kuwa yana walakini. Mfano hili la kutumia nafasi yake kama waziri wa ujenzi kubadilisha mwelekeo wa barabara kuu (trunk road) ili ipitie jimboni mwake ni jambo la dhahiri. Nilipopita njia hiyo binafsi nilishangazwa na jinsi ilivyokata kona kubwa kuelekea Chato.

  Lakini huyu bwana alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha nyumba za serikali zimeuzwa zote na akachukua fursa hiyo kwa kutumia nafasi yake kugawa nyumba ya serikali kwa kimada wake. Na sasa Burigi anatoa taarifa kuwa huyu bwana alitumia tena mamlaka yake kama waziri wa ardhi kubadilisha mipaka ya wilaya yake ili kulipatia manufaa jimbo lake. Haya mambo yanaonyesha kuwa kuna trend ya huyu bwana kutumia nafasi zake kujinufaisha yeye binafsi na jamaa zake.

  Mimi binafsi siamini kuwa Dr. Magufuli ni presidential material. Ni kweli kuwa amekuwa akichapa kazi vizuri kwenye wizara anazopatiwa kwa kulinganisha na mawaziri wenzake wa CCM ambao ni watendaji wabovu. Kwa hiyo hiki tunachokiona kama utendaji mzuri kimsingi ni utendaji wa wastani tu ambao unakuzwa kwa sababu kigezo tunachotumia kumpima utendaji ni cha chini sana.

  Badala ya kuita tuhuma za Burigi kuwa ni crap ni vyema tukachukua muda kuzitafakazi na kuona kama zina substance kwani ni vizuri kuujua upande wa pili wa huyu bwana ambaye tayari kuna watu wanajenga hoja kuwa awe rais.
   
 17. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Katika makosa makubwa na ya kutisha yaliyofanywa na utawala wa BWM ni pamoja na kuuza nyumba za Serikali. Na inabidi watu wakumbuke kwamba sio nyumba zote ziliuzwa, bali ni zile tu zilikuwa katika maeneo mazuri sana (prime location). Na vizuri tukakumbuka pia kwamba Mhe Dkt John Pombe Magufuki ndiye aliyesimamia kwa nguvu zake uuzaji wa nyumba hizi za Serikali.

  Historia ni muhimu sana katika kumjua kiongozi. Ndio maana wenzetu wana utaratibu wa kuandika 'biography' za viongozi ili kuwajua vizuri.
  We need to know our leader centre, left and right. Tuwajua wanayoyafikiria, kuyasema na kuyatenda. Wasiwasi wangu ni kwamba hatuwajui viongozi wetu vizuri, na maamuzi yetu mengi yanaenda kishabiki. We are giving our leaders too much easy ride and that is why it is easy for them to turn on us, and we easily find ourselves having nothing sensible to do because of guilt consciousness. Kwa kifupi tunapowamwagia masifa viongozi wetu, masifa yaliyojengwa kishabiki tunajiweka umateka, na ndio maana tunakuwa wakali tukiambiwa upande wa pili wa hawa watu. Kamwe tusiendelee kumsifia baba kwa kumnunulie mwanae nepi!!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,577
  Trophy Points: 280
  Kwa aliyefika Biharamulo na kufika Chato, ukiombiwa Biharamulo ndio makao makuu ya wilaya, unaweza kulia, ni vumbi kwa kwenda mbele na majengo ya mwaka 47 yakiwa katika hali ya choka mbaya!

  Nenda Chato, ni lami mpaka mlangoni, maghorofa ya kisasa ya NHC na maendeleo ya hali ya juu.

  Wakati wa uchaguzi mdogo wa Biharamulo, vihoteli vya Bi'mulo vyote vilikuwa vimejaa, tukalazimika kulala Chato kwenye bonge la hoteli la multi millions!, guess ni la nani?.

  Pamoja na yote haya, Magufuli ni genius, ni kichwa kichwa kweli, kama hayo yote ndiyo ameyafanya Chato ndani ya kipindi cha miaka kumi yake ya ubunge, hata kama ni at the expense ya Biharamulo, amini nakuambia, akichukua nchi ataigeuza ahera within the first five years.

  Aliyoielevete Chato from nothing into heaven, ndivyo ambavyo atawainua Watanzania toka umasikini uliotopea mpaka kuwa nchi ya maziwa na asali!.
   
 19. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,870
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  Mbona hata kwenye hiyo Crap ya jamaa yetu Buzwagi haimo? Au na wewe umechanganya taarifa na Tulawaka, maana jamaa ndo ameongelea huo mgodi na siyo Buzwagi usimtuhumu bure ndugu yangu.

  Kuhusu mambo ya Mh. Magufuli nafikri huyu jamaa katumwa huyu ukimwuliza baada ya muda kidogo atakwambia EL ndo anafaa kuwa Rais. Kama ni hayo mambo ya wakubwa mbona CCM wote wako hivyo? Hivi ni nani kati ya wanasiasa wa CCM huwa anashinda kihalali? Mkulu mwenyewe mpaka achakachue sembuse Wabunge!! Hebu mwenye ujasiri asimame mbele ya kadamnasi atuambie kama ameshinda kihalali!

  Na kuhusu kupindisha barabara, mbona viongozi wote wanafanya hivyo? Wala Mh. Magufuli siyo wa kwanza! Hamkusikia jinsi Pesa 2 alivyojipendelea jimboni kwake mpaka wenzake wakalalamika!! Hivyo hivyo na Mh. Kawambwa naye alipopewa wizara ya miundombinu huyo akachakachua barabara na kupendelea jimbo lake au hamkusikia jinsi wabunge wa Tabora walivyomkalia kooni? Kwa hilo wala Mh. magufuli hatuwezi kumlaumu hata kidogo. Au wewe unataka mpaka apigwe mawe na wapiga kura wake ndo ufurahi? Tumwache atumie nafasi aliyonayo maadam anawaendeleza wa-TZ hao hao, kuliko kama angepeleka tumboni mwake hapo tungekuwa na hoja ya kumtuhumu.

  Kwa kupima kwangu na kuangalia vigezo vya uwajibikaji Mh. Magufuli ndo yuko afadhali kuliko viongozi wengine wa CCM (Hata ugonjwa unazidiana ndugu yangu Magufuli ana uafadhali) nenda kokote utamkuta yuko vizuri. Hao unaotaka kutuambia si ajabu ndo Papa na Nyangumi katika ufisadi. Kama hilo halitoshi tunakuomba utuelekeze wa kwako unayefikria kwamba ni bora kuliko wengine.
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wa Ngima!

  Huna hoja wewe, jitahidi usiwe unafata mikumbo fikiria na kuwa na independent mind. Nina mjua Magufuli hata ukitaka simu yake nitakupa. Ifike wakati hata kama wewe ni mpinzani lililo zuri tulikubali si kupinga tu. Pamoja kuwa sikubaliani na CCM ila unaposema hakuna mwema CCM nadhani unamtindio wa ubongo. Nakupa scenario CCM 2015 wakamsimamisha John Pombe Magufuli, na upinzani mkamsimamisha Edward Lowassa sababu amedefect CCM na kuja CHADEMA mkamuweka mgombea wenu, nina uhakika itakula kwenu. Kamwe magufuli na mapugufu yake hawezi kuwa Lowassa, jamaa anajua kusimamia kazi. Tuanahitaji raisi kama huyo. Nimeweka mfano wa Lowassa kusudi tu maana upinzani hubeba kila kapi mfano Mh Shibuda etc etc etc.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...