Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kiukweli Empress Ki ndio ilinifungua macho kuhusu siasa hata za hapa kwetu, bonge moja la drama aisee
 
Umesahau kuwa nilizaliwa pale Nilizaliwa Pale Yodongseong na nikakulia Gwamingseong na Pyeongyangseong. Utagundua kuwa vita zipo damuni, kifupi naendelea na Wang Guhn, nataka nifuatiliea General Park Sulhae atamuoa dada yake Kyeo non?!, and what will happen baada ya kifo cha Binti wa Yanggil,.

Nilitaka kula ugali na mboga maana ugali mkavu unakaba shingo.
 
nikupe pole sana kwa kusubiria ndoa ya general park dhidi ya dada yake kyu hyun.
teh teh teh bora nisikuhadithie kinachotokezea mbeleni.

merciful buddha
wanawake wenye msimamo kama jiwe la msingi la klabu ya simba oyeeeeeeee
 
Fanya uwe unatuchambulia na muvi zetu zile.. Sio kwa uchambuzi huu murua kabisa!
Ungekua unachambua za Hollywood ningeinjoi sana. U good
 
Kumbe muendelezo mpaka mwakan looh
 
Sungnyang na Mfalme wa Koryo wanisamehe sana kwa kweli maana walikuwa majembe lakini huyu Togon yaani hapandi kichwani mwangu kwa kweli
 
Wakati tukiendelea na *Ongoing* si mbaya pia tukijikumbusha Projects zilizopita nyuma. Watu wa 'Mitandao' wanasemaga 'Throwback Thursday' lakini hii ni katika Korean Drama.

Ni wangapi waliopata kuishuhudia Project moja hivi ya takribani miaka mitano iliyopita, inayokwenda kwa jina la Doctor Stranger?

Kama umepata kuitazama basi 'Hongera Sana' na kama bado wala hujachelewa kwa maana ipo na inapatikana kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao na wavuti mbalimbali za K-Drama Ulimwenguni.

Ni Drama yenye maudhui ya kisasa, wengine mnapenda kusema "ya kimjini mjini" au naweza kusema kuwa si ya kijijini bali ni ya mjini iliyokuwa ikirushwa hewani na kituo kikubwa sana cha Televisheni cha SBS cha nchini Korea Kusini mnamo May 5 hadi July 8 mwaka 2014.

Drama hii inahusu au inamhusu kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Park Hoon. Kijana huyu anaishi na baba yake mzazi aitwaye Park Cheol. Park Hoon na babaye wote ni raia wazalendo kabisa na watiifu wa sheria bila shuruti wa taifa la Korea Kusini.

Nitaelezea kisa cha mwanzoni kabisa cha Drama hii kinachohusu maisha ya utotoni ya kijana huyu Park Hoon pamoja na baba yake:

Baba yake Park Hoon ni daktari bingwa hususani katika masuala ya upasuaji (Thoracic Surgeon) taaluma ambayo ilimvutia pia kijana huyo mdogo kuisomea na kujifunza pia kupitia baba yake. Tukirejea utotoni kipindi Park Hoon akiwa mdogo mnamo mwaka 1994, walipelekwa nchi jirani ya Korea Kaskazini kipindi ambacho kulikuwa na hatari kubwa sana ya kutokea kwa vita baina ya nchi hizo mbili.

Kabla sijaendelea, huenda utakuwa ukijiuliza kuwa huyu ndugu yetu Park Hoon hakuwa na mama?

Hapana! Alikuwa naye lakini wazazi wa kijana huyu Park Hoon waliachana ama walitengana kisha mtoto yaani Park Hoon kubaki upande wa baba yake.

Ni kitu gani basi kingesababisha vita hiyo kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini?

Ni kuwa, Serikali ya Korea Kusini ilipenyezewa taarifa ya siri kuwa Marekani ilikuwa na mpango wa kushambulia vinu vya nyuklia vya Korea Kaskazini na iwapo Marekani itafanya hivyo basi akina 'Kiduku' lazima nao watalipa kisasi kwa kupitia Korea Kusini ambaye ni mmoja wa washirika wakuu wa Marekani.

Ilikuwa ni "patashika nguo kuchanika" maana vifaru vya kijeshi vya Korea Kusini vilikuwa vikipita barabarani na Jeshi la Korea Kusini lilikuwa tayari kabisa kuikabili Korea Kaskazini lakini kwa upande wa wanasiasa hasa viongozi wa juu wa Korea Kusini hawakuwa tayari kwa vita hiyo na jirani yao Korea Kaskazini maana kwa mtazamo wao kama vita ingetokea basi ingeleta madhara makubwa sana ambayo ingechukua muda mrefu sana kuyarekebisha madhara hayo.

Bahati nzuri na nikutoe hofu ni kwamba vita haikutokea na amani ilirejea lakini ilibaki kidogo tu ama kwa kifupi naweza kusema "Almanusura Wazichape". Hali ya utulivu na amani haikurejea tu ghafla bali kuna mtu alifanya kazi kubwa sana ya kuuzima mzozo huo, naye si mwingine bali ni Bw. Park Cheol, baba yake mtoto Park Hoon.

Ni kitu gani alichokifanya huyu ndugu yetu Park Cheol kilichosababisha vita isitokee?

Ni kwamba katika utawala wa Korea Kaskazini kulikuwa na mgonjwa wa moyo ambaye alikuwa akikaribia kufa. Si mwingine bali ni kiongozi wa kwanza wa taifa hilo la Korea Kaskazini ambaye bado alikuwa madarakani, Kim Il-sung (Babu yake Kim Jong-un wa sasa).

Sasa, Wamarekani walikuwa wakivizia kifo cha huyo 'Bwana Mkubwa' wa Korea Kaskazini ili waitumie fursa hiyo kuipatia 'kichapo' nchi hiyo na kuharibu miundombinu yao ya nyuklia, ambapo nayo Kaskazini kivyovyote ingelipa kisasi kwa shambulio dhidi ya Korea Kusini. Na kama vita vingeibuka, viwango vya mionzi vilivyosababishwa na shambulio la nyuklia pekee vingefanya theluthi moja ya taifa hilo ya Korea Kusini isikalike kwa miaka 200 ijayo. Hatari sana!

Kutokana na kujulikana kwa Dk. Park Cheol (Baba yake Park Hoon) nchini Korea Kusini kutokana na taaluma yake na uwezo wake wa hali ya juu ilibidi ufanyike mpango wa haraka sana wa kumpeleka daktari bingwa huyo kulekule Kaskazini ili akamtibie jamaa mpaka apone la sivyo akifa tu, 'balaa' litakalotokea baada ya hapo watakao baki hai watasimulia wajukuu zao.

Mpango huo wa kumpeleka Bw. Park Cheol huko Korea Kaskazini unasimamiwa vilivyo na Waziri aliyefahamika kama Jang Suk-joo ambaye alikuwa na ukaribu sana na Daktari wetu Dr. Park Cheol.

Baada ya Dr. Park Cheol kupelekwa huko Korea Kaskazini kibao kiligeuzwa na aliwekwa kizuizini pamoja na mwanaye Park Hoon mpaka pale atakapofanikiwa kumfanyia upasuaji wa matibabu ya moyo Mkuu wa taifa hilo la Korea Kaskazini ambaye tayari nilikwisha kukutajia jina lake hapo awali (Babu yake Kiduku).

Uwezo wa Dr. Park Cheol na moyo wake wa ushujaa uliwezesha kufanyika kwa upasuaji huo wa moyo na kufanikiwa kumrejeshea uhai mgonjwa aliyekaribia kufa.

Wakati utakapokuwa ukitizama hicho kipande (Scene) katika hiyo Drama hukohuko uliko lazima utapata hisia fulani hivi ya shangwe kutokana na mafanikio ya Dr. Park Cheol katika chumba cha upasuaji huku akiwa amezungukwa na walinzi na huku bastola ikiwekwa kichwani pa mwanaye Park Hoon ambayo ingeusambaratisha ubongo wa mwanaye huyo endapo baba, Dr. Park Cheol angeshindwa kumtibu 'Bwana Mkubwa' wa taifa hilo.

Ushindi huo wa Dr. Park Cheol katika chumba cha upasuaji ndiyo uliwezesha kumponya mwanaye na yeye pia bila kusahau taifa lake la Korea Kusini dhidi ya vita sababu kutokana na hilo, Marekani ilighairisha mpango wake wa mashambulizi baada ya 'Bwana Mkubwa' wa Korea Kaskazini kuokolewa kutoka katika kifo baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo na Dr. Park Cheol.

Nyumbani Korea Kusini ilikuwa ni shangwe na furaha iliyoje baada ya kufanikiwa kuzuia vita iliyokuwa ikikaribia kutokea na kila mwananchi wa Korea Kusini alisherehekea kwa namna yake. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa, mafanikio ya Dr. Park Cheol yalimpa sifa sana yule Waziri Jang aliyempeleka Dr. Park Cheol kule Kaskazini. Ni jambo la kushangaza kwelikweli maana wananchi walimsifu zaidi Waziri Jang bila kujua kuna 'mwamba' mmoja yupo Kaskazini huko akifanya yake ili taifa lipone.

Mfano hata wewe msomaji wa bandiko hili, siku ufanye jambo kubwa sana na la maana katika jamii linalohitaji ujasiri na ushujaa wa hali ya juu alafu sifa ziende kwa mwingine kabisa, sijui utajisikiaje!

Kilichotokea baada ya jamaa, huyo Waziri kulewa 'sifa' matatizo mengine nchini Korea Kaskazini yakaibuka ambapo Dr. Park Cheol pamoja na mwanaye walikataliwa kurudi kwao Korea Kusini ikiwa ni njama za ndugu Waziri kuyaiba mafanikio ya Dr. Park Cheol na kujinufaisha kisiasa ili aweze kuyatumia mafanikio hayo kama karata muhimu ya Uchaguzi wa Urais uliokuwa ukikaribia nchini Korea Kusini.

Dr. Park Cheol na mwanaye walinyang'anywa haki ya kurudi nchini kwao na kulazimishwa kusalia katika nchi ya ugeni baada ya visa vingi sana na vya hatari kutokea.

Wakiendelea na maisha mapya kabisa nchini Korea Kaskazini mtoto mdogo kabisa Park Hoon anakutana na msichana mdogo pia aitwae Song Jae-hee na kuzoeana ghafla licha ya kukutana kwa siku ya kwanza kabisa.

Hapo nimeelezea kwa uchache tu kuhusu maisha ya utotoni ya kijana Park Hoon pamoja na baba yake bila kusahau misukosuko waliyopitia.

Ni nini kiliendelea baada ya hapo?

Je walifanikiwa kurudi kwao Korea Kusini?


Ili kuyapata majibu ama majawabu ya maswali hayo basi itafute Drama hiyo inayokwenda kwa jina la Doctor Stranger na bila shaka maswali hayo yatajibika machoni pako wakati utakapokuwa ukiendelea kuitazama Drama hiyo.

Ahsante sana na pia karibu kwa maoni au maswali!



 
Nakuheshimu sana jombaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…