KHERI ya KUTIMIZA miaka 3 NDANI ya JF (siku ya jana)
Teh teh teh nilitaka nijaribu kuandika kwa kiingilishi lakini nimeshindwa, naogopa wazee wa ngeli wasije kunizodoa asubuhi yote hii wakanifanya nikose hamu ya kukandamiza bakuli langu la UROJO kama
meok goo anapokosa bakuli la wali na supu ya mende kwa ufadhili wa hela ya European Union.
ningelikuwa ni mtenda dhambi kama ningelishindwa kuandika ujumbe huu wa shukurani kupitia thread hii ambayo nusu ya comment zangu nimeziandika humu ndani (comment 1298)
huwezi amini nakumbuka ni kama juzi tu najaza fomu ya kujiunga na JF mida ya jioni, baadae naandika ujumbe wangu wa kwanza ndani ya thread hii baada ya kuwa msomaji wa muda mrefu, nakutana na wakorea uchwara kupitia keyboard, naanzisha utani wa ajabu haliyakuwa si tabia yangu, mara paaap nakufa kwa kucheka peke yangu.
kilaza kama mimi ninayeshindwa hata kuandika sentensi nzuri zenye kubeba haiba ya matukio husika ya sherehe muhimu basi niwatakie wakorea uchwara wote pasina kuangalia asili zetu za kiimani sikukuu ya kuzaliwa mtakatifu yule wa nazareth majuma machache yajayo.
kama kuna yeyote humu ndani niliwahi kumkera na akachukia kama wanavyochukiana mashabiki wa vyura na mikia naomba anisamehe.
jamani hapa mtaani kwetu ndani ya wiki mbili hizi wameshafariki watu 5, mamamaaaaaaaaaaa nadhani huyu malaika mtoa roho ananipigia misere kwa honda ya bajajiiiiiii na toyo.
ili niwe muhenga wa kati kati ndani ya JF napaswa nitimize miaka mingapi?
nasubiria keki zangu zilizotengenezwa kwa siagi na mayai ya maneno japokuwa wale niliowakuta wamekuwa wavivu wa kutembelea humu ndani kwa sababu zisizoepukika.
daebak, niilikuta hii thread ikiwa ukurasa wa 24 lakini leo imeshafikisha ukurasa wa 402, nawaomba munipe dawa itakayoniwezesha niache kuifuatilia hii thread tafadhali.
Age is an issue of mind over matter. If you don't mind, it doesn't matter. - Mark Twain.