Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Sipati Picha Joseon Ingekuwepo Mpaka Leo!
 
Hiyo Dong Yi Iko Poa Sana Story Yake. Ila Usiiangalie Kama Hupendi Drama Ndefu Zenye Slow Story!

Duh! Kwa Ji Chang Wook Umecheki K2 Tu. Sishangai Sababu Drama Zipo Chungu Mbovu, Si Rahisi Kuangalia Zote Ilhali Kila Day Zinachomoka Mpya.

Ji Chang Wook Zipo Nyingine Nzuri Tu Alizo Feature Ukiacha Hiyo K2. Kama Vile;

Healer
Empress Ki
Suspicius Partner
Warrior Baek Dong Soo


Drama Nyingine Kali Na Sio Mbaya Kurudia Kama Tayari Umeshaiona!

Let's Fight Ghost
Kill Me Heal Me
Doctor Stranger
Shine Or Go Crazy
W Two Worlds
Come Back Mister
What Happens To My Family
Queen In Hyun's Man
Suspicius Housemaid
Cruel Palace
Night Watchman's Journal
 
Asante, nitaanza kufuatilia moja baada ya nyingine kati ya hizo.
 
The Player ipo vizuri nilishuka nayo jumla jumla kila katikati ya week iki updatiwa tu mpaka ikaisha
 
Let's Fight Ghost bonge la drama story nzuri sana.
 
Kheri ya mwezi mpya wa December chingus, Mungu atujaalie uwe ni mwezi uliojaa baraka na neema zinazozidi uzito wa vijisenti trillioni 1.5 kwa kila mdau humu ndani.
kwa nini December kiupande wangu?
  1. ndio mwezi wa mwisho wa mwaka huu 2018.
  2. waumini wa imani ya ukristo duniani husherehekea kuzaliwa kwa mtakatifu wao aliyetakasika kuliko kiumbe yeyote aliyezaliwa na mwanamke.
  3. huyu lofa aliyeandika ujumbe huu atatimiza mwaka wa 3 tokea awe mwanachama wa JF ifikapo 15/12/2018 endapo atakuwa na uhai.
  4. na kama mambo yataendelea kuwa mazuri basi inshaalllah kama ilivyokuwa mwaka jana tutapeana updates za tunzo zitakazo fanyika mwishoni mwa mwezi huu kupitia mashirika ya KBS, SBS na MBC drama awards .Hili litawezekana kama mtandao wa soompi watakuwa live.
natumai bado tunakumbuka kilichotokezea mwaka 2017.
  • SBS drama awards: muigizaji bora wa mwaka alikuwa ni JI SUNG kupitia drama ya INNOCENT DEFENDENT.
  • MBC drama awards: muigizaji bora alikuwa ni mzee Kim Sang Joong kupitia drama ya the rebel thief who stole the people.
  • KBS drama awards:washindi walikuwa ni mzee cheon ho jin kupitia family drama inayoitwa my golden life na mzee kim young chul kupitia family drama inayoitwa father is strange.
nimalizie kwa kumtakia kheri ya kuzaliwa Khantwe, nilitaka niwe mtu wa mwisho kumtumia ujumbe utakaomjaza furaha lakini cha ajabu kila ninapotembelea jukwaa la chit chat nakuta bado watu wanaendelea kumtumia jumbe za pongezi huyu ahjumma mtarajiwa.
nimebaki najiuliza maswali yasio na majibu kama uchumi wa Afrika.

hivi huyu mwanamke ni mtakatifu sana anayemkaribia bikira maria aliyemzaa yesu kristo?

hivi huyu mwanamke utakatifu wake anamkaribia khadija yule mke wa mtume wa waislamu?

sidhani kama anawafikia hao japo kwa 40% bali silaha yake kubwa ni kuishi na watu wote humu ndani kwa upendo na hekima zinazoendana na lugha inayopendeza kutumika kwa rika lolote lile.
kumbe mwanzoni nilikuwa nafanya makosa nilipokuwa naogopa kunukuu hata comment yake pindi alipokuwa anatoa mchango wake humu ndani kwa kudhani ni goi goi.
naomba unisamehe noona kwa ujinga wangu.​
naamini kupitia thread hii nitatimiza ndoto yangu ya kuwa wa mwisho kumtakia kheri ya kuzaliwa.

sitaki stori za wakorea siku ya leo kwa sababu bado nina hasira na jose mourinho na watoto wake wazembe.
 
Wakuu mimi napenda sana series za action kama 24hrs ya jack bawa, na na zile iris 1 na 2........kiufupi Napenda action zenye kuonyesha system ya uongozi kama maraisi nk na ulinzi wao na changamoto pia........ So nataka kurudi koreans kwa mwenye kujua series zenye hayo mambo tafadhali
 
Playful kiss umeshaangalia??

Black night
 
Daah ilikuwaje sikuona hii jamani..asante sana sunbae sio kwa maneno haya mazito yaliyoniacha mdomo wazi. Nimekuwa mvivu wa kupita jukwaa hili kwa kuwa sina access ya kdrama kwa sasa kwa hiyo yanayoongelewa mitaa hii yote mapya kwangu naishia tu kuumia roho... Mungu akubariki na akuongezee siku tuendelee kufaidi hekima zako maana kwa hekima hata sisi wahenga umetuacha mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…