Nimeshangazwa sana na fikra za kizamani ambazo nimeziona Tanzania kwa wanaume. Mimi kama mwanaume ambaye sikuwa Tanzania kwa muda mrefu nimesikitishwa sana na tabia ya kihuni ya wanaume hasa walio na wake.
Tanzania kuna magojwa na kila familia ina ndugu ambaye amepatwa na ukimwi lakini nimeshangazwa na tabia ya wanaume kuwa na wanawake wa pembeni wakati wana wake nyumbani. Cha kushangaza wanaume hata marafiki zangu wamekuwa wakishinda kwenye klabu za baa baada ya kazi na wanawake wa pembeni huku wake zao wakiwa pekee na watoto nyumbani. Swali je kwanini umeoa kama hauko tayari kutulia?, Je mke wako ukimpelekea magojwa kama ya ukimwi ni nani ataangalia watoto wako kama wote ni wagojwa? Je hizo pesa ungeziweka na kuzitumia na mke wako kwenda kupumzika sehemu huoni kwamba ni muhimu zaidi?. Kitu ambacho ni cha ajabu zaidi ni kwa wanaume wengi kuona kama kitu hiki ni cha sifa na ukipata pesa kidogo ni lazima uonyeshe watu kwamba una uwezo wa kuwa na wanawake wengi!!.
Tofauti wa wanaume wengi tulio ugaibuni tatizo letu ni kupata wanawake wazuri kwani tunajua umuhimu wa wake wazuri kwenye maisha. vilevile tumekuwa tunajitegemea wengi kuanzia miaka 21-23 hivyo tumekuwa mapema sana. Wengi vilevile tumeona wanawake wa kila aina hivyo mambo ya wanawake si mageni hata kidogo. Lakini tukiamua kuoa tunatulia kwani tunajua kwanza sio sifa kwa jamii kuwa na wanawake wengi lakini vilevile tumekuja huku kutafuta na si kujionyesha au kufanya uhuni. Hivyo kwa mawazo yangu Wanaume wa nje ni bora sana kwenye ndoa kuliko wanaume wengi wanaoishi Tanzania ambao wengi ni wahuni wa kutupwa.
Ushauri ni wanaume wenzangu acheni ushamba na uhuni sio sifa kuna familia nyingi sana sasa wana wajane kwasababu ya magojwa, watoto wanahitaji pesa ya bar kwa elimu, nchi yetu inahitaji tujihusishe na shughuli za maendeleo ya nchi yetu masikini. Kikubwa zaidi ni kwamba itakuwa vizuri ukitumia muda wa jioni kufanya mazoezi kwani Tanzania hata huduma ya afya ni ya kiwango cha chini sana.
Mimi siandikagi kwenye mapenzi lakini nimeona hili badilikeni ni mawazo tu.