Kwa wanaume tu (vichwa vya familia)

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,713
1,263
Heshima kwenu wanaume

Najaribu kutafuta busara za kiume, ni tabia gani ambayo ni kero na imekuwa sugu kutoka kwa wake zenu/marafiki wa kike, hata michepuko kama ipo?

Tukizingatia kwamba, hakuna mwanadamu mkamilifu, ila kuna tabia ambazo ni kero zonazopelekea kuachana.

Kama mwanaume, naomba uniwekee tabia 3-5 unazochukia kwenye ndoa yako na mahusiano, na kama ungepewa rungu na Mungu kutengeneza mke mpya, ungemuwekea zipi upate kitu OG.

Comment zako kwenye hii thread, zitanitengeneza mimi (kama mwanamke) na pia nitashare na wanawake wenzangu.

Angalizo: usibeze thread yangu, usinitukane, usikashifu.

Hii ni thread kwa wanaume tu.

Wasalaam.

~~~~

UPDATE:

Salut kwenu vichwa vya familia (Wanaume),

Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kutoka katika kilindi cha moyo wangu. Nimefurahi sana, uzi huu umeitikiwa kwa kishindo. Mungu awabariki sana.

Asante kwenu wote mlio na msiochangia mada hii, maoni ya wachache yamewakilishwa vyema.

Maoni yamepokelewa, nayachambua ili niyawakilishe kwa wanawake wenzangu, kama nilivyoahidi hapo awali. Nashukuru, maoni yenu yamenibadilisha kwa namna moja, kuna makosa nimekuwa nikifanya bila kujua kama namkera mwenza wangu/boyfriend/mchepuko nk.

Nina ka jambo kangu na vichwa vya familia/wanaume, nitakuja hapa muda si mrefu kukawakilisha.

Kaeni mkao wa kula. Msichoke/msikate tamaa kutukosoa pale inapobidi.

Asante sana.

Wasalaam

Carol.
 
Mwanamke mwenye msimamo kwenye mambo sahihi asiyeyumbishwa na mazingira/hali yeyote uvumilika katika kero zake.

Turudi kwenye mada.

Sasa wengi ya wanawake kuna mambo wanakuwa wanakurupuka kufanya maamuzi na mambo mengine wanafanya kwa mihemko. (Wanakera sana)

Kuna upuuzi wa mwanamke kila kitu anachofanyiwa/anafanya lazima a-publish.(Wanakera zaidi)

Kuna aina ya mavazi mwanamke hata kama mpo kwenye mahusiano unaona kabisa anakuwa na ujasiri kuvaa mbele yako, basi unam-categorise katika kundi fulani.

Summary:
1. Mwanamke huna msimamo
2. Maisha ya maonyesho
3. Uvaaji
 
1. Kuongea sana kama cherehani bila hoja ya msingi
2. Kutokuelewa pale nnapomuambia kwamba kwa sasa/tarehe hizi sina hela. Au namuambia sina hela jioni, asubuhi ananipa listi ya vitu vya kununua!
3. Kung'ang'ania kitu. Akitaka kitu chake hata kama ni cha kijinga, ataking'ang'ania na nikikataa ataendelea kua ananisumbua kila siku mpaka nachoka naamua kukubali
4. Kutokunielewa siku ambayo mimi sitaki ku do. Ila yeye akiwa hataki anaona sawa tu.
5. Kuuliza uliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu.
 
1. Gubu
Mwanamke hutakiwi kuwa na gubu mpaka mwanaume akirudi kazini hajiskii hata raha kukaa nyumbani. Hata kama una shida mwache apumzike kwanza, then tafuta muda baadae ili umwambie kwa utulivu.

2. Wivu wa kupitiliza
Hii tabia wanaume wengi hatupendi, mwanamke unakuwa na wivu mpaka na simu za kikazi anazopigiwa mumeo! Tena wengine hata wakiona namba ngeni ndio kabisa.

3. Kujenga tabia ya mazoea
Mwanzoni mwa ndoa, mnajifanya watiifu sana, baada ya muda kupita huwa mnajenga tabia ya mazoea kiasi kwamba yale mnayokuwa mnawafanyia waume zenu mwanzoni mwa ndoa mnayaacha kisa tu mmewazoea. Hii tabia wanaume wengi wanaichukia na ndio chanzo cha wanaume wengi kuwa na michepuko kwani michepuko hawajengi tabia za mazoea, kila siku wanakuona mpya. Kama mwanzoni ulikuwa na tabia ya kumpokea mumeo akirudi kazini usiache hata kama siku asipokuja na kitu.

4. Ufedhuli/ujeuri
Mwanamke hutakiwi kuwa fedhuli/jeuri kwa mumeo. Kauli ndogo tu kwa mumeo inaweza kusababisha naye akakudharau.

5. Kuwa na sauti ya juu kuliko mumeo
Mwanamke hutakiwi kuwa na sauti ya juu kuliko mumeo, hata kama mumeo hana ubavu/tena wanawake wengine wao huwa ndio wanajifanya waongeaji sana kuliko waume zao hasa pale wanapotembelewa na mgeni.
 
Nikiwa kama baba wa nyumba, moja kabisa ni mke kukaribisha majirani kuja kuangalia TV ndani kwangu.

Ya pili ni kujichubua au kuweka vitu bandia kwenye mwili mfano, wigi, kucha bandia, hereni kwenye K na mamekap yaliyozidi.

Ya tatu ni kushabikia mpira! Mwanamke kama unashabikia mpira pita mbali nami
 
Asante sana, umeelezea kwa ufasaha sana.
 
Nikiwa kama baba wa nyumba, moja kabisa ni mke kukaribisha majirani kuja kuangalia TV ndani kwangu
Ya pili ni kujichubua au kuweka vitu bandia kwenye mwili mfano, wigi, kucha bandia, hereni kwenye K na mamekap yaliyozidi.
Ya tatu ni kushabikia mpira! Mwanamke kama unashabikia mpira pita mbali nami
Safiii...point namba 2 imebamba sana. asante mno.
 
1. Tabia ya kuninunia bila sababu.

2. Tabia ya kukata a kuoga nami bafuni

3. Tabia ya kukataa kuongozana nami popote.

Tabia iliyo mbaya kuliko zote kutonipigia magoti anaposalimiana nami ama kunikaribisha chakula yaani full dharau muda wote.
Nimekuelewa sana. Point taken. Asante sana
 
MKE

1. Gubu
2. Kupekuwa simu yangu kila baada yadakika 15
3. Kubana mapaja hadi siku akijisikia yeye genye.

Nimenukuu kutoka kwa jirani hapa... Mie bado nipo nipot
hakuna shida, tabia nyingi zinafanana. Ukiona kwenye zilizoandiwa basi chomekea.
Kilichonileta kwenye huu uzi ni kukusabahi tu mkongwe mwenzangu Caroline Danzi

Halafu baadaye baadaye nitarudi kumwaga mapoint ili Joanah aache tabia zake zinazowakera wanaume
watu8, tuko pamoja.
 
I am vey happily married, though nikikumbukia enzi zile:

  • Uongo
  • Take me for granted
  • Being too dependent
  • Inability to keep time
  • Dharau

We-nye walikuwaga na hizo tabia enzi zile na wakapita kwa anga zangu, najua mpaka leo watakuwa wananikumbukaga
 
1. Gubu
2. Mdomoo au maneno mengi ishu ndogo mtu anaifanya kubwaaa na kuongea sana bila kumaliza
3. Kumbania papuchi mmeo. Hapa wake wa ndoa huwa wanafeli sana unakuta mtu zaidi ya mwezi anabana miguu tu mwisho wa siku mumeo anaamua kukuacha tu anapiga kazi za nje
4. Kutokujishughurisha katika kutafuta hela mwisho wa siku mke unakua tegemezi kupitiliza
5. Kupekua simu ya mwanaume na kuanza kuuliza maswali
 
6

6. Uongo
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom