Kwa wanaume tu; soma hapa!

Naomba mawazo yenu/wazo lako binafsi je wewe unaweza kuoa mke mwenye watoto wawili.umempenda huyo dada na umemkuta anaishi na watoto wake .na hakuna mahusiano yahuko alikowapata !je will you be comfortable with that family?wale watoto wawili kuwa pattern parcel ya familia yako!kweni ninamaana kubwa kuuliza hivi ,nahitaji majibu na sababu .either wewe unaye mtoto wako huko nje au huna
karibuni ndugu zangu mnipe mawazo yenu

Kwangu mimi si tatizo hata kidogo kwa mambo yote mawili.Nikiamuwa kumuowa mwanamke nitamuowa kama alivyonitambulisha mwenyewe. Tatizo ni kudanganyana eti ooh wewe ndio wa mwanzo halafu nakuta tu pyee hapo nitagombana nae, lakini nikishajuwa nachukuwa second hand nimeshapenda sijali.
Halafu hili la watoto kama ulivyosema, dunia imebadilika hivi sasa tu lakini tuliolelewa hapo nyuma kidogo tulijikuta kwa watu wasio mama zetu au Baba zetu na wakitupenda sawa na watoto wao ambao huenda nao wako kwa watu wengine!
 
Tatizo hapa ni mkengeuko wa wanaume wa namna ya kufikiri..........
Kama mwanaume anayo mapenzi ya dhati kwa mwanamke anayetaka kumuoa mwenye watoto hata wanne, hilo haliwezi kumsumbua.
Lakini pia inategemea sana malezi ya mwanaume huyo kwamba amefundishwa nini na jamii kuhusu kuoa wanawake wenye watoto tayari. Kumbukeni tu kwamba kila kitu tunachofanya tumefundishwa au tunafanya rejea kutoka kwa wale waliotuzunguka........
 
kaka hizo tunaziita step families,kasurf kwenye net,uzielewe prons na cons zake.kwa ufupi kwa mwanzo kwa hao watoto utakuwa polite outsider.baadaye uncle, then step dad.
 
kama ni watoto wadogo under 7yrs naweza nikamuoa mamayao na kusetle nae.ila kuna restrictions flan flan hivi(sitaki kuwaona baba yao kwangu)
upande wa pili wa sh ni wanandugu wa mwanaume sizani kama wanaweza wakawa comfotable na huyo mwanamke.
Mimi nadhani kumpiga marufuku baba ya watoto haufanyi vizuri, hapo ndio utachochea watafutane chemba mwisho wa siku wanakumbushiana.
Isipokuwa kama huyu mzazi ni mwanamme na uwezo anao anakuja kuja nyumbani kufanya nini si awabebe wanae akawalee!?
Kama mzazi ni mwanamke nae aje kwa uwazi kuwaona watoto tena sio kwa kificho na sio kila siku.

nivea unachotakiwa kukifanya ni kuwa muwazi kwa mwenzi wako sie wanaume tunapenda kuambiwa ukweli, Sio leo mnaanza mapenzi unamwambia watoto baba yao hawajali wana hana mpango nao, mie najifunga kila kitu nawajali watoto kesho na keshokutwa oooh! baba ya watoto sijui anataka niniiiiii au............! pasipo kutaka ushauri unajifanyia mambo kienyeji bila kushirikishana.
Kuna msemo wa kiswahili usemao "Ukipenda boga...................
 
Naomba mawazo yenu/wazo lako binafsi je wewe unaweza kuoa mke mwenye watoto wawili.umempenda huyo dada na umemkuta anaishi na watoto wake .na hakuna mahusiano yahuko alikowapata !je will you be comfortable with that family?wale watoto wawili kuwa pattern parcel ya familia yako!kweni ninamaana kubwa kuuliza hivi ,nahitaji majibu na sababu .either wewe unaye mtoto wako huko nje au huna
karibuni ndugu zangu mnipe mawazo yenu

nadhani ungepata uzoefu mzuri kama ungeuliza si wanaume wote, ungechukua wa umri fulani tu. sisi vijana wenye wivu mnene wa mapenzi tutaonyesha haiwezekani. na tukisema inawezekana basi ni ktk masharti ambayo si ya kibinadamu kabisa. tukikua tutaelewa baada ya kuona hali halisi
 
Kama mnapendana sana unaweza ukafanya hivyo kwa mtazamo wangu
 
If wishes were horses,all beggars would ride.......majuto ni mjukuu......
Hao mnaowasema kwenye thread hii ie kaoa/kaolewa kaachika,ana watoto anataka aingie kwenye ndoa,kaolewa ana watoto ex anambugudhi,hana mtoto kaoa mwenye watoto,kaolewa na mwenye watoto, etc etc yote haya ukiwauliza wahusika wakuu watakwambia..'ningejua'.
Ideally kila mwanamke angependa a white gown wedding,kila mwanaume angependa apige suti/kanzu aoe bikra.Bahati mbaya maisha hayako hivo.
Kwa wale ambao mungali vijana bishanga nasema kueni muyaone,wale wa rika langu and above tumeona mengi na hakuna lililopostiwa ktika thread hii ambalo in one way or another hatujakutana nalo in reality,either kwetu binafsi au kwa marafiki ndugu au jamaa.
Nawasilisha.
 
Bro,watoto nimatokeo tu haijalishi aliwapataje ikiwa moyo wako umempenda na unaona mnaweza mkajenga nyumba yenu muoe,hakuna shida,mimi ningemuoa ikiwa tu baada ya kusomana tabia nikagundua ni mtu niliyekuwa ninamuhitaji katika maisha yangu.Mwanamke bikra,mwanamke asiyekuwa na mtoto/watoto,mwanamke aliyewahi kuwa na mtu ninayemfahamu siyo vigezo vyangu(they are not issues)vya kutafuta mwenzi wa maisha....
 
Kaunga na Kongosho, baadhi ya wanaume huwatelekeza watoto wao hivyo mdada ambaye yuko katika hali hii ni rahisi kuwa na mahusiano ukilinganisha na yule ambaye bado ana mawasiliano na Baba wa watoto. Wanaume wachache wanaweza kukubali hali hiyo ila wengi huwa wanasepa.
 
BAK nakubaliana na wewe kabisa
lakini kwa hali ya kawaida unawezaje mkataza mtoto kwenda muona baba yake?

Hata kama baba wa mtoto hatakanyaga kwako lakini at some point lazima kuna mawasiliano labda iwe alitelekeza mtoto.

Mbaya zaidi baba mwenye mtoto awe ana uwezo kuliko anayetaka kuoa hapo ndo sumu kabisa.

Mi nadhani wanamme wanapenda kuwa 'in control' so akiona kuna mwanamme mwingine karibu yake anapoteza amani.

Ila kweli for 'weak hearts' hasa wanamme bora wasijihusishe na wanawake wenye watoto kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Inbidi uwe na roho mgumu, maana mtoto ni bond kubwa, na wenye watoto wanakuwa wametengana sio kwamba wameachana, km wewe ni mtu kutoka iringa ningekushauri tafuta tu binti achana na huyo mama.
 
Inawezeka mkuu, coz mtoto wa mwenzio wako pia. Ila ni wale wenye neema ya Mungu ndan yao nat else!
 
Hili linawezekana kwa kuwa mhusika anajua kabla ya kuingia kwenye hiyo ndoa, lakini pia haya mambo ni ya kisaikolojia zaidi kwa wanaume walio wengi mfano mzuri japo ni wa nje ya maadili ni hivi, unakuta mkaka hajaoa na anamsifia mke wa mtu ni mrembo na pengine anatoka nae na huyo mke wa mtu ana watoto hata watatu lakini hapa haionekani kama ni shida lakini mtu huyuhuyu linapokuja suala la kuoa anakwambia mwanamke huyu ana mtoto/watoto hivyo inakuwa ngumu kuoa. Kama uliweza kutoka na mke wa mtu mwenye watoto na pengine ulikuwa una wapenzi wengine wana watoto kwanini linapokuja suala la kuvuta jumla unarudi nyuma? Mie nadhani ni suala la kimtazamo tu hili
 
Jodoki Kalimilo uko sawa kabisa, yan unakuta mtu ana mahusiano na mdada/mkaka mwenye mtoto/watoto na anaenjoy sana kana kwamba ukimwambia aachane na hyo dada/kaka anaweza kunywa hta sumu. sasa ifike umtamkie suala la ndoa. utasikia oh me cwez kuoa / kuolewa na mwenye mtoto.hv wakati wa mahusiano kabla ya ndoa hakuona huyo mtoto/hao watoto? dah inashangaza kweli kweli. . .
 
Last edited by a moderator:
Hili linawezekana kwa kuwa mhusika anajua kabla ya kuingia kwenye hiyo ndoa, lakini pia haya mambo ni ya kisaikolojia zaidi kwa wanaume walio wengi mfano mzuri japo ni wa nje ya maadili ni hivi, unakuta mkaka hajaoa na anamsifia mke wa mtu ni mrembo na pengine anatoka nae na huyo mke wa mtu ana watoto hata watatu lakini hapa haionekani kama ni shida lakini mtu huyuhuyu linapokuja suala la kuoa anakwambia mwanamke huyu ana mtoto/watoto hivyo inakuwa ngumu kuoa. Kama uliweza kutoka na mke wa mtu mwenye watoto na pengine ulikuwa una wapenzi wengine wana watoto kwanini linapokuja suala la kuvuta jumla unarudi nyuma? Mie nadhani ni suala la kimtazamo tu hili
Umechumbia aliyezalishwa nini!!?
 
Umechumbia aliyezalishwa nini!!?

Hapana mkuu, hizi faulo tunaziona mitaani zinafanyika au wewe hujawahi kuona au kusikia mtu yupo comfortable na mwanamke ambae ana mtoto lakini kuchukua jumla hataki hata kama utamshikia bunduki? tena hata kwenye familia zinatokea unakuta dada yako ameolewa akiwa na mtoto lakini inatokea kaka katika familia hiyohiyo anataka kuoa mke ambae ana mtoto unakuta familia inaanza kujadili wakati hata nyie kuna mwanafamilia ameolewa akiwa na mtoto.
 
Kiukweli ni vigumu kupata jibu la kweli hapa,mtu anaweza kukuambia anaweza kuishi nawe lakini akawa hamaanishi hivyo.Mimi binafsi katika maisha yangu ni bora niwe na mwanamke mwenye mtoto/watoto,si maanishi nikipata anaefaa halafu akawa hana nitamkataa,hapana,ila mwenye mtoto/watoto ndo first nina sababu zangu kufanya hivi,lakini ni bora ukawa makini sana!
 
Jmos iliyopita nilikuwa kwenye harusi ya dada mmoja anaolewa na ana watoto wanne
Mwanaume ni kijana kabisa nadhani 30-35 years na yeye hana mtoto.
Maswali milioni yalikuwa yanatembea kichwani kwangu...
FirstLady1 DU JAMANI KILA MTU NA BAHATI YAKE NA SIKU HUZI HII KITU IMEENEA SIJAJUA WANAUME WANALICHUKULIAJE JE NAHISI KUWA WNAJUA AMESHAJIFUNZA MAISHA SASA NI NIDHAMU NA ADABU AU LA I DONT KNW WHAT GOES ON THEIR MIND
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom