Kwa wanaume tu; soma hapa!

Kama hujikubali hakuna atakayekukubali?
Kwani kama jamaa anampenda na anajua ana watoto wawili, yeye tatizo kaliona wapi hadi kuuliza haya??

Huoni kuna ka "inferiority" fulani hivi?

Maana huyo jamaa kaona wasichana wangapi lakini bado kaenda kwake???

Nadhani haumtendei haki nivea...
 
BAK mkuu nimekupata vizuri na nimejifunza kitu kikubwa.

Umejifunza kitu gani? Say umeachana na huyo mume wako vizuri tu, na labda anaprovide kwa hao watoto, waweza kata mawasiliano kweli? au utawazuia wanao wasiwasiliane na baba yao/zao? Na hili swali BAK linakuhusu pia.
 
Last edited by a moderator:
Kama hujikubali hakuna atakayekukubali?
Kwani kama jamaa anampenda na anajua ana watoto wawili, yeye tatizo kaliona wapi hadi kuuliza haya??

Huoni kuna ka "inferiority" fulani hivi?

Maana huyo jamaa kaona wasichana wangapi lakini bado kaenda kwake???

Sio kila mwanaume anapoenda kwa mwanamke anaenda na ukweli. Na ukimwamini kila mwanaume anayekuambia anakupenda, unaweza kuwa jamvi la wageni. Nivea anajua kabisa kuwa na mtoto/watoto kabla ya kuolewa inapunguza 'points' za kuwa wife material (najua hilo hulikubali, but ndo ukweli)
 
Umempenda mwanamke mpende kama alivyo watoto ni matokeo ya upendo wenu,labda nikuulize swali unapofunga ndoa unafunga na watoto? pili kama mwanamke ni kigoli hana watoto mnapofunga ndoa si kwa matumaini kuwa mtazaa watoto?asipopatikana mtoto unafukuza mke?we endelea tu na mipango yako watoto ni zawadi toka kwa mungu yawezekana hao ndiyo wakawa wako jumla zawadi yako toka kwa mungu wala haisumbui.
Anachopaswa kufahamu muuliza swali ni kuwa kupenda hakuna fomula. Waswahili wanasemaukipenda boga penda na ua lake, lakini kuna mifani mingi ya kuonyesha jinsi hilo linavyoshindikana.
Kupenda ni suala linalohusiana na feelings, hivyo ni vigumu sana kujua iwapo mtu utawapenda watoto au la kwa sababu nayo inategemea pia na hulka na tabia za watoto hao.
 
Kwa wanaume wengi hili si tatizo ali mradi tu huyo Baba wa watoto asiwepo kwenye picha, mara nyingi kama bado kuna mawasiliano naye basi varangati huweza kutokea na kuharibu amani katika mahusiano.



BAK my dear, mawasiliano yepi unategemea yasiwepo?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Aisee kwa wanaume walio wengi (at least from my experience) akikubali ujue anategemea zaidi ya love, yaani pengine anaona mambo yako ni mazuri hivyo utamtunza yeye pamoja na mtoto/watoto wake. Hapa ninamaanisha awe single au na yeye awe na mtoto/watoto motivation in maslahi/maisha mazuri kwanza. Usishangae baada ya kufunga ndoa akadai mbadilishe jina la mmiliki wa gari, sijui nyumba, biashara n.k So be careful my sister, si rahisi kihivyo!

Hivi hujawahi kuona au kusikia wajane wakitapeliwa mali walizoachiwa na wanaume zao kisa amepata mwanaume wa kumuoa na kuishi naye na watoto wake hata kama anao 4? Kuna mama mmoja Dodoma alifiwa na mumewe, akamwacha na watoto 3 na mali lukuki. Basi wanaume kibao walikuwa wanataka kumuoa. Akaja akaingia mkenge akaolewa na mmojawapo. Kilichotokea ni majuto hadi leo......

Sasa je kama huyo mwanamke ni hohehahe/kajamba nani, utaongeleaje kuhusu hilo???huyo mwanaume atakua kafata nini???
 
Kwa wanaume wengi imekuwa nadra sana kutokea hivyo nadhani kwasababu ya kuhofia zaidi "nini watu wanaonizunguka watasema" lakini ikitokea wanaume hawana shida sana juu ya hilo. Mimi binafsi kwangu haina shida pia kama ingetokea.
 
Kama kuna mapenzi ya kweli, kuoa mke mwenye watoto wawili inawezekana. Kumbuka kuwa ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili. Lakini ni ukweli usiopingika kuwa Kuna changamoto nyingi sana zitajitokeza pale ambapo muunganiko wenu wa ndoa hautasababishwa na upendo baina yenu, bali vitu fulani fulani.

Kuna hatari ya dharau na hali ya kutokuheshimiana kujitokeza kwa mke/mume na watoto wa mke/na hao mtakao zaa huko baadaye kama wana ndoa nyie mtashindwa kuelewana na kupanga mipango yenu vizuri. Pia ndg wanaweza kuleta vikwazo sana ktk mahusiano yenu. Kumbuka pia hao watoto watahitaji kwenda kwa baba yao/zao. Ni muhimu kuliweka hilo vzr mapema na kutafuta njia sahihi ya hao watoto na wewe mama mtu kuwasiliana na huyo mzazi mwenzio wa zamani vinginevyo unaweza kuonekeana unakumbushia enzi na kuhatarisha usalama wa ndoa mpya!

Lakini ukweli ni kuwa wapo waliofanya hivyo na kufanikiwa ingawa si wengi sana ila mwisho wa siku, hatma ya maisha yenu ya ndoa ipo mikononi mwa nyie wanandoa wenyewe.

HorsePower :A S thumbs_up: :A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
Last edited by a moderator:
Lakini jamaa si kataka kukuoa pamoja na watoto wake?

Kwani wanaoumizwa kwa kudangyanywa na wanamme kuwa wanawapenda na baadae kuwaacha wote wana watoto??

Sio kila mwanaume anapoenda kwa mwanamke anaenda na ukweli. Na ukimwamini kila mwanaume anayekuambia anakupenda, unaweza kuwa jamvi la wageni. Nivea anajua kabisa kuwa na mtoto/watoto kabla ya kuolewa inapunguza 'points' za kuwa wife material (najua hilo hulikubali, but ndo ukweli)
 
Mie nashangaa tu, eti baba wa mtoto asiwepo kwenye picha, how??
Yaani uwakosanishe baba wa mtoto na mwanae kisa ndoa mpya?

Hapa nahitaji mtu wa kuelewesha
Umejifunza kitu gani? Say umeachana na huyo mume wako vizuri tu, na labda anaprovide kwa hao watoto, waweza kata mawasiliano kweli? au utawazuia wanao wasiwasiliane na baba yao/zao? Na hili swali BAK linakuhusu pia.
 
Kupenda ni kuchagua, kama huyo mwanamke nimempenda kiukweli haina shida yoyote kumuoa lakini hao watoto si wanababa yao? itabidi tu awalee.
 
bwana mzee mm nakushauri somba mali zako weka ndani usiulize mtu uliza moyo wako kaka jadiliana na bibiye kuhusu baba za hao watoto wekeni misingi imara ya mahusiano yenu asiwaingilie mtu kwenye hilo hivi kama una ulemavu wa uzazi ukaasili mtoto kisheria utakuwa umefanya kosa?
 
ndio maana siamini kwenye ndoa baada ya kuvunjika ya kwanza ni mtazamo wangu tu.

Chauro hata mimi huwa naamini zaidi hivyo, ingawa inawezatokea mmeachana mkiwa bado hamjazaa, hivyo ukaenda kuanza upya kwa mwingine.

Lakini mkiwa na watoto tayari ni risk kwa wote, siyo kwa mwanamke tu. Hata mwanaume unawezajikuta watoto wako wanateseka ile mbaya, kisa umeamua kuacha mama yao na kuoa mwanamke mwingine.
 
Sasa je kama huyo mwanamke ni hohehahe/kajamba nani, utaongeleaje kuhusu hilo???huyo mwanaume atakua kafata nini???

Unachosema Yummy ni kweli, wewe jaribu tu kuwachunguza kiundani wenzi wa jinsi hiyo utajua ninachomaanisha. Hapo nilitoa mfano mmoja tu wa mali za mjane. Lakini kama ulivyosema kuna wakati inatokea mwanaume ndo anawatoto lukuki, halafu anahitaji mama kwa aili ya kumlelea wanae. Kwa mfano tumeshuhudia harusi mwanaume ana watoto 3 na yuko safi tu kimaisha, halafu anaoa mwanamke ana mtoto 1 (huyo unayesema hohehahe) akiamini kuwa atatulia ndani kwa kuwa alishazalishwa bila kuolewa, pia atakuwa mlezi mzuri kwa wanae kuwa ana mtoto tayari.
 
Jmos iliyopita nilikuwa kwenye harusi ya dada mmoja anaolewa na ana watoto wanne
Mwanaume ni kijana kabisa nadhani 30-35 years na yeye hana mtoto.
Maswali milioni yalikuwa yanatembea kichwani kwangu...

Situation kama hiyo FirstLady1 si bure, hapo huyo kijana lazima ana zaidi ya love kichwani mwake. Hebu tujuze kidogo kuhusu profile zao financially, mali, elimu n.k
 
kama ni watoto wadogo under 7yrs naweza nikamuoa mamayao na kusetle nae.ila kuna restrictions flan flan hivi(sitaki kuwaona baba yao kwangu)
upande wa pili wa sh ni wanandugu wa mwanaume sizani kama wanaweza wakawa comfotable na huyo mwanamke.
 
Situation kama hiyo FirstLady1 si bure, hapo huyo kijana lazima ana zaidi ya love kichwani mwake. Hebu tujuze kidogo kuhusu profile zao financially, mali, elimu n.k

Nikiangalia wote wako vizuri kabisa ..mdada ni mjasiriamali na Kijana ni msomi na ana kazi yake nzuri tu..
Labda hapo kuna true love..?
 
Nikiangalia wote wako vizuri kabisa ..mdada ni mjasiriamali na Kijana ni msomi na ana kazi yake nzuri tu..
Labda hapo kuna true love..?

Mmh haya bana, may be that one is exceptional!! Let us wait and see...., but I'm very skeptical!
 
Back
Top Bottom