mbiza
JF-Expert Member
- Feb 8, 2014
- 539
- 147
habarini wanammu,nimelazimika kuandika hii kitu kutokana na video iliyosambaa mtandaoni ambayo inamuonyesha mfanyakazi akimpiga mtoto mdogo mpaka kumuua,kiukweli kitendo hiki kimeniuma na kunikera mno kama binadamu.na kutokana na hayo ningependa kuwashauri wanafamilia hasa baba na mama kuwa wawe wangalifu na hawa wafanyakazi wa ndani kabla na baada ya kuwaajiri kwa sababu dunia ya sasa imebadilika na watu wamekuwa zaidi ya wanyama huwezi jua huyo mtu alipotoka alikuwaje tabia yake ikoje,mwisho wa siku majanga kama haya yanatokea na kuleta simanzi na huzuni kubwa sana katika familia hivyo kuleta dosari ya maisha kwa wanafamilia.kama inawezekana muendapo makazini hata muwe mnarudi manyumbani kuangalia hali ikoje,wengi wenu muda mwingi mpo ofisini na mnawaacha majumbani watoto na hawa wafanyakazi na hamjui huwa nini kinaendelea manyumbani,hii video ni mfano tu wa yale yatokeayo tu hatujui mengine yanayofanyika humo majumbani.sio wafanyakazi wote ni wabaya ila tuwe makini tu.