Tatizo la Hanang' ni pale ofisi za Halmashauri, DED mama Gody Pamba na wasaidizi wake hawana uzalendo na ile wilaya kwani hata OC zinapoingia fedha nyingi hungia kwenye matumizi hewa na hata Nagu anapoambiwa kwa kuwa amemleta kutokana na urafiki wao humkingia kifua. Gody Pamba ameletwa Hanang' na Mary Nagu baada ya Chadema kushinda kata ya Katesh katika uchaguzi mkuu 2005 na DED aliyekuwepo ambaye alikuwa mchapakazi mwenye uwezo wa kuziba mianya ya ufisadi akahamishia halmashauri ya Kishapu, sababu ikiwa ni Chadema kushinda Kata ya Katesh, kukataa kumpa Nagu pesa za kampeni tofauti na taratibu na Majungu toka kwa wakuu wa idara pia yalitumika kumtoa huyu ndg E.L. Shimwela, kwani kwa muda mfupi aliokuwepo Hanang' ufanisi ulionekana na matumizi hewa yalidhibitiwa.