Kwa wana Hanang' iliyoongozwa na Mh Sumaye na sasa Mh Mary Nagu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wana Hanang' iliyoongozwa na Mh Sumaye na sasa Mh Mary Nagu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jqnakei, Apr 13, 2012.

 1. J

  Jqnakei Senior Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika tz wilaya ambaye huduma muhimu za jamii ni duni sana, nasema tena sana si kidogo ni Hanang mojawapo ambako mpaka sasa imeongozwa na mawaziri wawili (sumaye na sasa Nagu) lkn wilaya hii huduma muhimu kama vile maji, matibabu na elimu ni duni sn ktk baadhi ya maeneo mfano kata ya Gehandu na B/lalu ambako watu huchota maji kwa masaa 12 ktk baadhi ya maeneo na maji haya mara pengine si salama kwa afya ya binadamu kutokana na meneo yakochotwa haya maji, si jambo la kushangaa kuwakuta watoto weng tu hawajaenda shule wakichunga kutokana na shule kuwa mbali sn ktk baadhi ya maeneo nimewahi ona mwanafunz wa primary akitembea masaa 2 njiani afike shule, huduma za afya kama matibu zipo mbali sn ktk baadhi ya maeneo ambako watu hulazimika kutembea masaa 6-8 mara pengine. je hawa viongozi wetu hawaoni hilo tatizo? kuwa hizi huduma muhimu za jamii ziwepo karibu kwa ajili ya maendeleo ya jamii?. Kweli kwa hili tutafikia tz vision 2025 au ni ndoto?.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,114
  Likes Received: 2,219
  Trophy Points: 280
  Jimbo lingine la CDM hili,usiwe na wasiwasi si umeona nassari?
   
 3. U

  Upatu Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo jimbo linachukuliwa na Rose Kamili ambaye hivi sasa ni mbunge wa viti maalum wa CDM katika wilaya hiyo. Kikubwa walichofanya hayo magamba ni kuweka barabara ya lami ambayo inaunganisha Singida na Minjingu. Lakini hakuna kitu kingine chochote, kila kitu ni shida. Hilo Jimbo tayari ni mali ya CDM
   
 4. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,642
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo barabara wameanza kuweka lami lini na imekamilika?lami yenyewe bado haijaunganisha singida na manyara
   
 5. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Jimbo la CDM hilo ni muda tu tunasubiri ufike ROSE KAMILI awe NASSARI wa hilo JIMBO tulieni watu wa HANANG.
   
 6. s

  slufay JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,360
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo kaka huwa hawakai HANANG wanakaa masaki na Kiluvya hiyo sehemu ya kuombea kura tu, halafu elimu ndogo, wafugaji wengi sana hawaenda shule ukienda na t-shirt unapata kura zote
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,956
  Likes Received: 367
  Trophy Points: 180
  Binafsi naifahamu vizuri jimbo la Hanang, na tokea nianze kupiga kura sijawahi kuichagua ccm kutokana na jinsi walivyotutelekeza sisi wananchi wa Hanang.
  Jimbo la Hanang limebarikiwa kuwa na mlima ambao una vyanzo vingi vya maji, mfano maeneo ya Nangwa mlimani, Jarodom, Gendabi.
  Maji yalitolewa Gendabi na serikali yakapelekwa mashamba ya NAFCO, huku wanakijiji wanateseka kupata huduma ya maji. Vijiji vya Mogitu, Gehandu, Balangdalalu just to mention few vimekuwa vikipata shida ya maji kwa muda mrefu.
  Kwa mfano watu gehandu kupata maji nilazima wasafiri zaidi wa kilomita 15 mpaka 20 kupata maji.
  Jimbo la Hanang linahitaji kiongozi mwenye ujasiri, ambaye anaweza kuthubutu kwa namna yoyote ile.
  Jimbo la Hanang lilipata bahati ya kuwa na waziri mkuu kwa muda wa miaka kumi, lakini hakuna alichosaidia kimaendeleo.
  Sumaye kuwa waziri mkuu ndiyo chanzo cha kudorora kwa maendeleo ya wilaya, kutokana na kuyaua mashamba ya NAFCO kwa makusudi. Nakumbuka baada ya kushinda ubunge 1995 na kuteuliwa kuwa waziri Mkuu ziara yake ya kwanza ilikuwa CMSC, akaahidi kuyauza mashamba ya nafco yote hata kwa shilingi kisa hawakumpigia kura, baba yangu alimchallenge sana na kumjibu vibaya, kitendo kilichogharimu ajira yake.
  Hanang kwa sasa ina madiwani 25, ambapo 12 wanatoka CCM na 12 wa CDM 1 wa CUF.
  Ni imani yangu kuwa 2015 wananchi wa Hanang hawatafanya makosa.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,572
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ..inaelekea Sumaye na Nagu wameweka utaifa mbele, ndiyo maana majimbo yao yamedorora kimaendeleo.

  ..hivi mlitaka wawe kama Msuya, Mramba,Magufuli,Kikwete, kupendelea majimbo yao??
   
 9. s

  slufay JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,360
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Utaifa gani hata visima vya maji visiwepo wakati kuna mlima HANANG' daima utakumbukwa kwa lipi; Je sifa ya kuwa na utaifa ni lipi hasa?
   
 10. U

  Upatu Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vibaraka tu hao, hakuna cha utaifa, mbona Sumaye kajilimbikizia mali kama alikuwa anajali utaifa, Wanafiki tu hao, wanajifanya kujipendekeza kwa maraisi wao lakini hakuna kitu majimboni mwao
   
 11. J

  Jqnakei Senior Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUNACHOMAISHA ULISHIRIKIANA VP NA WANANCHI WALIOKUPA DHAMANA LA UONGOZ KTK KUILETEA JIMBO MAENDELEO. Utaifa gani unauzungumzia kama umeshindwa kusimamia maendeleo ya jimbo lako?. Hamasisha na simamia maendeleo ya jimbo lako pia tuuone na huo utaifa ktk kusimami rasima za wananchi inatumika kwa maendeleo yao.
   
 12. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,487
  Likes Received: 1,850
  Trophy Points: 280
  hanang ilipaswa kuwa wilaya inayoongoza kwa kipato cha kilimo ngano,shayiri wateja wa uhakika bakhresa na breweries
   
 13. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nagu badala ya kuwasaidia wana hanang alikwenda kuwaada wanaarumeru kuwa eti wakimachagua sioi watajenga EPZA maeneo ya makiba!
  wiki mbili zilizopita ametoa msaada wa matreta kwa kifupi amekalia kuti kavu.
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 6,857
  Likes Received: 3,989
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha ha! Mkuu usitake kuniambia magamba "wameazimishwa" kwa muda!
   
 15. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nashukuru kama mmeona huo uozo wa Hanang' maana wanafahamu kule hakuna atakayeona huo uozo wao. Hayo yaliyosemwa ni ya kweli lakini pia ukiingia Halmashauri ya Hanang' ufisadi uliopo hauna huruma na wakazi wa Hanang', ipo mishahara hewa, posho hewa ndiyo usiseme, fedha za likizo, matibabu na mapunjo mishahara watumishi wamekosa matumaini. Msemaji wa wilaya hiyo hasa pale Halmashauri ni afisa mmoja mwenye cheo cha chini maarufu kwa jina la mzee wa matusi. Huyu ndiye DED na ndiye afisa elimu wa wilaya na huwa anawatukana walimu kama watoto. Wilaya hii inapaswa kuangaliwa kwa macho mawili kweli hali si shwari, Madeni ya walimu ambayo serikali iliahidi kulipa kabla ya mwezi febr. Mwaka huu, Hanang' walimu hata leo hawana matumaini. Tatizo la Hanang' linaanzia kwa wanasiasa hadi Halmashauri.
   
 16. c

  chamgema12 Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka hebu ishilikishe akili japo kidogo!
   
 17. L

  Laban Boaz Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tiba ya jimbo hilo ni kulirudisha cdm ili liwe na uhuru halisi na kamili. Imenisikitisha kusikia jimbo lenye utajiri mwingi kama hilo linakuwa na maisha magumu namna hiyo. Poleni sana wana hanang' ila "freedom is coming tomorrow"
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,159
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu;
  Kweli wewe kamanda ni mzalendo na unaifahamu vizuri Hanang. Umenihabarisha vema. Lakini hayo majina ndio yalivyo au umeteleza kidogo....LOL!
   
 19. J

  Jqnakei Senior Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chakushangaz anawaambia Arumeru wakichagua upinzani serikali haitapeleka maendeleo, hakuona jimbo lake lilivyo na halimbaya ambayo ipochini ya chama tawala. Naamini HANANG' hawatafanya makosa 2015.
   
 20. M

  MOSSAD JACOB Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Charity starts at home.we kama kwenu umeshindwa kuweka hata kisima cha maji kijiji chetu utaweka.jamani uongozi ni kileo .kunawanao kunywa sana na kuona hakuna kesho na wapo wa kiasi wanawaza kesho itakuwaje?
   
Loading...