Nimeiona ila nikakudondokea wewe....
Husninyo siku hizi hanisalimii vizuri aisee....lol!!
Ndoa yenye mtoto aliyezaliwa kabla ni changamoto sana na watu wasipokuwa waangalifu wanabwaga manyanga!
Kuna jamaa yangu alilazimika kuzuiwa kwenda kwa mzazi mwenzake na kumleta mtoto nyumbani kwa sababu walikuwa wanatumia hiyo nafasi kumsalimia mtoto na mama wa mtoto....(wazazi wengine wanakuwa mabazazi)!!
Mimi ni mwanaume nilibahatika kupata mtoto wa kiume nje ya ndoa.
Sasa miaka 10 baadae nimeoa na nimemchukua huyu mtoto wangu naishi naye.
Sasa mke wangu ameniwekea masharti ambayo nafikiri ni magumu kutekelezeka. Naamini kuwa mwanamke niliye zaa naye ana haki ya kumuoma mtoto wake kila anapohitaji kufanya hivyo.
Sasa mke wangu hataki huyu mama mtoto afike nyumbani kumuona. Hataki mtoto aende kwa mama yake. Anataka mama mtoto akitaka mtoto tumtume housegirl ampeleke mtoto hoteli foleni halafu wakimaliza kuongea arudi naye.
Hali hii imeniingiza kwenye migogoro maana mama mtoto anaona namnyanyasa na upande mwingine mke wangu anaona pia namnyanyasa.
Hebu niambieni what is the beat way ku deal na hii situation?
Aisee babu mimi nashindwa kabisa kumuelewa mwanamke ambae anakubali ndoa inayomfanya mtoto wake aonekane mchungu. Sijui kama ni utoto ama lack of experience ila nashidwa kabisa. Hao ndo wale wanaosaidia waume zao kuwakandamiza watoto wao wenyewe ili mradi tu ndoa izidi kuwepo.Hii itawezakana endapo huyo mama wa mtoto hayuko kwenye ndoa. Endapo yuko kwenye ndoa hali inaweza kuwa tofauti.
Mshikaji wangu alimchukua mtoto baada ya ugomvi na mkewe, ila baadaye walishindwa na kumrudisha mtoto kwa mama. Huyo mama naye aliolewa na ikabidi mtoto abaki na bibi.
Kwa ufupi ni maisha ambayo yana changamoto nyingi sana. Hakuna njia rahisi au ya mkato.
Sindo hapo sasa. Unakuta mwanamke mwenyewe anaeng'ang'ania mtoto achukuliwe hafanyi kwa mapenzi yake kwa mtoto ila kwa insecurities zake binafsi. Mtoto anaishia kuishi maisha ya shida wakati haikuwa lazima.Over my deadbody mama yangu hawezi kulea mtoto wangu jukumu lake alishamaliza.
Kama mtoto yuko under age abaki na mama yake na hata akiwa over age ruksa pia historia inaonesha kwenye situationa kama hii tena mtoto wenyewe utakuta ni mmoja aachwe amfariji mama yake, Baba unaclear bill tu. Umeoa mwanamke mwingine zaeni wa kwenu kama unadhani mpaka kuitwa Baba au mama au fulani ni mchezo.
Kweli kila mtu ana akili na roho ya kipekee.
Kwahiyo wewe kwa akili yako una uhakika kwamba huyo mkeo ndo atakuwa na positive effect+influence na mtoto kuliko mama yake mzazi. Nyie ndo huangalia watoto wakinyanyaswa kwenye himaya zenu day in day out kisa ulimbukeni wa mapenzi.
Unajuwa hizi kesi hazifanani kama mwanamke uliyezaa naye hajaolewa na mwanaume mwingine na angalau anayamudu maisha yake mpe mtoto akae naye wewe utatoa matunzo, ni uselfish uliopitiliza mtoto kukosa mapenzi ya wazazi wake, inabidi ni lazima mmoja wenu akae na mtoto, binafsi siwezi kukubali mama yangu kulea watoto wangu, alishanizaa nimekuwa kazi yake imekwisha kama ng wajukuu watamtembelea weekend na kuspend naye likizo inatosha na yeye wale good time na mume wake siku zao zilizobaki.
Hilo la kuhakikisha mtoto hanyanyaswi ni jema, ni vizuri una uhakikisha hilo. Lakini bado hutumii busara wala haki kusema mtoto asiende kwa mama yake kamwe. Kama ulijua ulozaa nae sio mwema kwanini ulizaa nae on the first place. Ungesubiri ukazaa na ambae ni mke wako ili kusiwe na mtafaruku wa aina yoyote ile.Mke ninaye ishi naye nyumba moja hawezi kumtesa mwanangu huku mimi nikiwepo.
Nimeshuhudia mengi ndugu yangu kuhusu hili Swala Kwahiyo mpaka nimesema hivyo basi ujue ni kwamba nimeyaona na kuyaishi. Mwanamke uliyezaa naye kwa asilimia kubwa sana akiona umeshaoa atamtumia mtoto kuvunja ndoa yako.
Kwahiyo usinihukumu bila kujua Sababu zangu za kufanya hivyo. I know it all na kwa niliyopita na kuyaona there is no way nikawa blinded na mke wangu juu ya malezi ya mtoto.
nikaribishe babu, mjukuu wako kakumiss sana ujue.
Unataka kukaribishwa mara ngapi Husninyo?
Tulikuwa na wajukuu kibao wakati wa siku kuu ya Xmass na mwaka mpya....
Unakaribishwa wakati wowote ila siku kubwa nyingine itakuwa Feb 14!!
Babu DC!!
Mkuu sijasema mtoto aishi na babu na bibi yake. Nilichosema ni kwamba huyo mama wa mtoto akitaka kumuona mtoto wakaonane nyumbani kwa wazazi wa baba. Wakishaonana na kuspend time then mtoto anarudi kwa baba yake. Kwa babu yake panakuwa ni meeting point.
Kama ulijua ulozaa nae sio mwema kwanini ulizaa nae on the first place. Ungesubiri ukazaa na ambae ni mke wako ili kusiwe na mtafaruku wa aina yoyote ile.
Kama mmekubaliana na kuridhia huo utaratibu basi ni sawa. Ila kama anavyosema Lizzy, wakati mwingine mmoja wenu anaweza kuwa anatumia mabavu na hilo siyo sawa.
Hata hivyo, lazima kuwepo na jitihada kubwa kulinda ndoa, na pia kuangalia ustawi wa mtoto!
Siyo lazima kuchangia kila thread, grow up.
Mama ana Haki ya kumuona mtoto wake,tena binafsi ningependa mtoto aishi na mama yeke kuliko Kuishi na mimi. Lakini kuna wanawake wengine wanafanya makusudi kulazimisha mtoto aishi kwa baba ili apate fursa ya kuvuruga ndoa yako. Yani usije kuomba kukutana na mwanamke wa aina hiyo,huyu mkuu Lizzy anaongea tu kirahisi,unafikia kipindi inabidi kufanya maamuzi magumu ambayo mtu wa kawaida atakuona una Roho mbaya Lakini kiuhalisia ni kwasababu una jitahidi kuhakikisha things don't fall apart lkn Mzazi Mwenzio Yupo busy kukupa stress kwa kumtumia mtoto
Mimi ni mwanaume nilibahatika kupata mtoto wa kiume nje ya ndoa.
Sasa miaka 10 baadae nimeoa na nimemchukua huyu mtoto wangu naishi naye.
Sasa mke wangu ameniwekea masharti ambayo nafikiri ni magumu kutekelezeka. Naamini kuwa mwanamke niliye zaa naye ana haki ya kumuoma mtoto wake kila anapohitaji kufanya hivyo.
Sasa mke wangu hataki huyu mama mtoto afike nyumbani kumuona. Hataki mtoto aende kwa mama yake. Anataka mama mtoto akitaka mtoto tumtume housegirl ampeleke mtoto hoteli foleni halafu wakimaliza kuongea arudi naye.
Hali hii imeniingiza kwenye migogoro maana mama mtoto anaona namnyanyasa na upande mwingine mke wangu anaona pia namnyanyasa.
Hebu niambieni what is the beat way ku deal na hii situation?
Well ukisema hivyo napata point yako na taratibu naanza kukuelewa.Lakini kuna wanawake wengine wanafanya makusudi kulazimisha mtoto aishi kwa baba ili apate fursa ya kuvuruga ndoa yako. Yani usije kuomba kukutana na mwanamke wa aina hiyo,huyu mkuu
xfactor pamoja na yote hayo bado humtendei haki mzazi mwenzio. Besides, unadhani kwa kumkataza mtoto kwenda kwake ndo hatajaribu kukuharibia ndoa yako kama lengo lake ni hilo?! Be fair, kama unavyopenda wewe kukaa na mwanao ndo na yeye anapenda vile vile, mpe uhuru nae. Pia usidhani mtoto atakuja kukushukuru kwa hilo. Maana hapo ulipo unafikiria "ndoa yangu, ndoa yangu" na wala sio mtoto. Don't be like that aisee. Binafsi nisingefurahia kama mtu nlonae angekuwa kama wewe iwapo angekuwa amezaa kabla ya kukutana na mimi. Besides, Sio kila ubaya unaokusudiwa humfika mtu, mengine hupita tu kwahiyo usiishi kwa hofu ya kufanyiwa ubaya kupitia mtoto. Pia kumbuka kwamba huyo mtoto anakua na atakuja kufanya maamuzi yake mwenyewe linapokuja swala la kuonana/kuwa na mama yake mzazi. How will you control him/her then?! Kama ujinga si atajazwa tu?!
Muhimu ni wewe kutumia nafasi yako kama baba,mume na mzazi mwenza vizuri. Usikandamize sana upande mmoja ukapendelea kwingine na mwisho ukaishia kuharibu badala ya kujenga kama ulivyokusudia.
I prefer mtoto aishi na mama yake kuliko kuishi na mimi.