Kwa waliofika Lubumbashi na Kinshasa

kuhusu nafasi za biashara kama unaweza kusafirisha hata gunia la ndizi basi nenda nalo...mara ya mwisho kwenda pande hizo walikua wana import mpaka mikate...chakula kinalipa sana huko tatizo kukifikisha..


DRC/RDC mpaka leo bado barabara zao ni shida yaani tunawapita hata sie watanzania kwa ubora. Kwa sasa chakula ni kingi tu ila bado fursa ipo kwani kuna wafanya biashara wengi wa kule wanapenda sana kuingiza biashara hata kama hazina faida kwao na hazilipi ili mradi tu ana duka.
 

mkuu mji gani huo
 
Nilikuwa lubumbash almost two months wala hakuna lolote la maana labda kidogo ningekushaur uende kenya japo cjui kama utaweza gharama za maisha
 
Kaka vipi biashara ya dhahabu un aweza nipa mchanganuo yani bei upatikanaji wake nk
 

mkuu epuka sana wanawake wa kasumbalesa.mchana watu usiku majini.take care.lubumbash ni jiji so hayo usemayo ya anasa utapata.ila watu si wakarimu.km bongo.kukuzunguka ni mchezo mdogo sana hasa km umeenda kibiashara.
 

Watafute Samatta na Ulimwengu watakusaidia....
 
AMada nzuri sana hii kwa mtu mwenye interests za biashara.
Nimesoma thread nzima na ukiacha mizaha naona kuna oppurtunities kwa mtu aliyedhamiria biashara.
Ila sijapata feedback ya mtu anayetaka kunzisha biashara, vibali au leseni vinapatikana kirahisi?

Mfano, chakula ni shida, waweza fungua duka kubwa, inabidi ukodishe duka na upeleke semi treka ya bidhaa za chakula.
Vibali vya usafirishaji vinapatikana kirahisi?
Na leseni ya duka je?

mleta mada kaleta kitu skili ichangamke!
 
Hawa watu ni wavivu kumbe
 
Nasikia huko ni kawaida kumkuta mtu anadrive hammer halafu nyumba anayoishi ni ya matope ama mabox
 
mkuu epuka sana wanawake wa kasumbalesa.mchana watu usiku majini.take care.lubumbash ni jiji so hayo usemayo ya anasa utapata.ila watu si wakarimu.km bongo.kukuzunguka ni mchezo mdogo sana hasa km umeenda kibiashara.
Nimesoma Uzi vizuri na umenipa mwanga ila hapa pameniogopesha,sasa ilikukabiliana na hili mliokuwa huko mnatumia mbinu gani kukwepa tabia hii yao ya utapeli na usaliti kwa sisi wafanyabiashara tunaoitaji kwenda huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…