Kwa walioappeal vyeti feki na majina bado hawatoi

Trayvess Daniel

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
637
1,222
Huu ni ukosefu wa umakini kwa chombo husika, kuna makosa ya kibinadamu na makosa ya kimtandao kwa vyombo vyote viwili baraza la mitihani na TAMISEMI. Kwanini hawataki kuchukua jukumu la kubeba hayo makosa? Kwanini watu waappeal na kuonekana wameonewa lakini bado mshahara umesimamishwa? Hii si haki. Ndugu zangu mlioappeal na kuonekana safi, kukaa kimya kwenu ndio kuonewa kwenu. Huu mwaka utaisha huku mnajiangalia..... Muungane kwa pamoja kupigania kilicho chenu. Msiache huu mwezi ukapita bure, kwa uchache wenu (3% ya majina yaliyotuhumiwa) mnaweza kufanya kitu.
Wanasheria saidieni muongozo katika hili
 
Kwanini hawataki kuchukua jukumu la kubeba hayo makosa? Kwanini watu waappeal na kuonekana wameonewa lakini bado mshahara umesimamishwa? Hii si haki. Ndugu zangu mlioappeal na kuonekana safi, kukaa kimya kwenu ndio kuonewa kwenu.


Kuna mtu alisema hapa serikali haina fedha kwahiyo inatumia UP kama kisingizio
 
Back
Top Bottom