TAKUKURU kurekebisha makosa kwa kupunguza majina yaliyojirudia bado haijanishawishi kuja oral

Program Manager

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
2,511
3,432
Takukuru ni Moja ya Taasisi nyeti sana na ambayo inapaswa isimame katika misingi ya haki kwani hata majukumu yake yamejikita katika kutenda na kutetea haki.

Hivi karibuni mmetoa orodha ya majina ya vijana mliowaita kwenye usaili wa ana kwa ana oral interview, orodha ambayo imeacha maswali mengi sana kutokana na makosa mbalimbali ya kiufundi na kiuwasilishaji nitaainisha baadhi.

1 Usaili wa awali wa kupima ufahamu (aptitude test) haukuhitaji msailiwa aandike jina kwenye karatasi ya kujibia badala yake mlitaka namba pekee ambapo tuliamini mkifanya mchujo then tuone matokeo katika namba na si kuturudisha kwenye majina tena.
Yaani umeshanipa candidate number tayari kwanini usinipe majibu katika hiyohiyo namba? Kulikuwa na haja gani kutumia energy kubwa kubadili namba kuwa jina? Hapa Hakuna majibu mliyotoa watu hawajawaelewa.

2 Jina la mtu mmoja kujirudia zaidi ya mara moja. Japo mmekiri hili kosa na mmerekebisha lakini bado inaleta walakini na inatoa taswira tofauti kulingana na kila mmoja atavyoamua kufikiri.

3 Kuna malalamiko kwamba kuna majina yametoka ya watu ambao hawakuwepo kwenye usaili wa kwanza wameitwa waje kufanya Oral. Hii kama ni kweli basi ni dhihaka kubwa sana mliyotufanyia kwani inaashiria kwamba mchakato haukuwa fair bali mchakato wa mchongo.

4 matokeo hayana marks kila mtu alizopata. Kwanini nguvu iliyotumika kuweka majina isingetumika kuweka uwazi tuone performance ya kila mmoja? Mmesahihisha kweli ile mitihani?

MAKOSA NI MENGI SANA NA YALIANZA KUONEKANA HATA KWENYE USAILI WA AWALI
Binafsi nimeitwa kuja kwenye huo usaili wa ana kwa ana ila niseme tu SITOKUJA na ningehisi mazingira haya NISINGEKUJA hata kwenye aptitude test kwani nina maswali mengi yanayonivunja moyo na kukatisha tamaa.

Je, mtaonesha fairness iliyokosekana mwanzo?

Mchakato wa kupata watu mnaohitaji utakuwa na uwazi kiasi gani?

Mtatoa matokeo katika namba na siyo majina yenu mnayoyajua wenyewe?

Nikija nitaamini vipi kwamba sisindikizi watu ambao wengine hata kwenye usaili wa awamu zote hawakuwepo?

Nitaamini vipi nimefaulu usaili wa awali ikiwa kulikuwa na makosa mengi, je jina langu halipo kwenye pdf kwa makosa pia?

Kwa haya machache niseme tu kwamba SITOCHOMA NAULI kuja dodoma kwenye usaili wenu ni bora hii pesa ndogo niliyojichanga niitumie bar nikavunje bucket za budweiser na k vant Kuliko kucheza kamari na wachezeshaji wasio fair
 
Jamaa wametuvunja moyo kwakweli hakukuwa na haja ya kutuita watu wote wale tena kwenda kufanyia kwenye mkoa mmoja ambapo wengine tulitoka mikoa ya pembeni sana mwishowe matokeo yanakuwa ya namna ile.
 
Jamaa wametuvunja moyo kwakweli hakukuwa na haja ya kutuita watu wote wale tena kwenda kufanyia kwenye mkoa mmoja ambapo wengine tulitoka mikoa ya pembeni sana mwishowe matokeo yanakuwa ya namna ile.
Ni uhuni uliopitiliza umefanyika hakuna atakayewaamini kwa lililotokea
 
Msipoteze nauli zenu kwenda mtakuja kujuta nafasi zilishabookiwa mapema hizo ndio maana majina ya ambayo hawakuwepo yapo,majina yanajirudia bado ambao majina yao yalikuwepo na wamunganishiwa hukohuko.Nauli yako bora ukafanye jambo la muhimu
 
Nishaipangia matumizi mengine siwezi kwenda kwenye oral wala siwezi kununua haki kwa pesa ambayo ni mtaji tosha kuanzisha biashara
No money no fu.k.ng job
 
mnalalamikaaaaaaaa...wakati mishahara yenyewe nimefatilia ni laki6 afisa mchunguzi na laki4 kwa wasaidizi
Wakati wewe unawaza mishahara wengine wanawaza kulitumikia taifa lao na kukomesha vitendo vya rushwa.
Ndivyo mlivyo watanzania mkiambiwa suala la kuhusu kazi mnawaza kuchumia tumbo
 
Kama wewe siyo baba kantuma tafuta kazi za kufanya hizo nafasi zinawenyewe wewe unajulikana na Nani Hadi upewe hiyo kazi watu wamegharamia hizo nafasi
 
wenzako wanasema pesa kwanza uzalendo upo
Mimi niliomba nafasi ili nilitumikie taifa langu katika taasisi hiyo, nilikuwa tayari kuacha kazi kwenye NGO ambayo inanilipa pesa nzuri tu kila wiki kuliko hata hao takukuru, napenda kufanya kazi za uchunguzi tangu nikiwa mdogo ila trend yao imenivunja moyo na nimehisi hata nikiingia huko sitotimiza vizuri majukumu yangu
 
basi utakuwa wa kipekee
 
Back
Top Bottom