Kwa walevi: Hali ipi hukutokea ukishalewa?

Kwa walevi: Hali ipi hukutokea ukishalewa?

Nanoli

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
3,739
Reaction score
5,979
Mimi sio mnywaji wala mlevi wa pombe, hii ni kutokana na kuiona kero pombe kila ninapoonja huniletea matatizo, kama vile kichwa kuuma, kutapika na pombe kuchelewa kutoka mpaka siku inayofuata na kunifanya nione kero sana.

Hivyo naichukia. Sasa najiuliza, kitu gani kwa wenzangu kinawavutia kula ulabu huku kukiwa na hasara nyingi na faida chache? Kwa kawaida pombe inapoanza kukolea kwa mlevi, humletea mabadiliko yanayomfanya awe tofauti.

Wapo wengine wanajiona wenye nguvu ya kuwa wababe, wengine huwa waongeaji sana, wengine hupendelea kushika shika makalio ya wahudumu na mengine, sasa hii ndio burudani yenyewe?

Wewe mdau pombe inaposhika kasi ni furaha gani hukujia ambayo ndio burudani inayosababisha uipende pombe?
 
unakunywa pombe gani mkuu?????Inategemea na pombe...unakunywa Valuu?mfano mimi nakunywa pombe ambazo nikiamka asubuhi nakunywa hata chai ya rangi...yaani inakatika yote...( eg.pombe kali ambazo ni clear white kama vile pure grain vodka)...jaribu hiyo mkuu...ila usichanganye na kitu chenye sukari
 
Basi, sihitaji tena kujaribu mkuu..
 
Sijui kama nitakuja kuuaacha hii kitu.. I love i love it.................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom