Kwa wale wanaohitaji ku root smartphone zao

ericjames574

Member
Aug 30, 2015
44
125
Watu wengi kwa Sasa wanapendelea ku root smartphone zao nikiwa kama mmojawapo aliyefanikisha ku root nipo tayari kuwasaidia watakaohitaji

ericjames574

Member
Aug 30, 2015
44
125
Kuuliza si ujinga, Ku-root smartphone ndio kufanya nini na nini faida yake?
Wengi tumekuwa tukijiuliza maswali kuhusu ku ROOT simu
Hapa kuna maelezo machache yanayoweza kukufungua,
Ili kufahamu fungua link hapa chini

Nini maana ya ‘Kuroot’ simu yako? #Android #Rooting

Kuroot ni nini? Kuroot simu ya Android ni jambo linalofungua geti kuu la programu endeshaji hiyo na hivyo kukuruhusu kufanya mambo mengi zaidi katika programu endeshaji hiyo kuliko ilivyo kawaida.
Tushaulizwa mara kadhaa juu ya jambo hili na ata baadhi kuuliza jinsi ya kuroot simu zao. Haya ni yote ya kufahamu kuhusu ‘rooting’.

root-android.png

Kwa kiurahisi
Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta ya Windows basi utakuwa unafahamu ya kwamba pale kompyuta ikiwashwa inakupa chaguo la kuingia kama mtumiaji mkuu yaani Administrator – ambapo ukiingia kama Administrator unaweza fanya mengi zaidi katika upakiaji wa programu na ata katika masuala ya mafaili.

Pia kuna uwezo wa kuingia kama Mtumiaji Mgeni – yaani Guest. Ambapo hapa hautaweza fanya mabadiliko mengi katika kompyuta hiyo, utabanwa katika mambo mengi yanayohusu uwekaji programu na ata kufanya mabadiliko ya mipangilio (settings) ya kompyuta hiyo.

Toleo la Android katika simu yako – iwe Samsung, Huawei, Tecno n.k linavyokuja linakuwa linakupa uwezo wa kufanya mabadiliko ya kama mtumiaji mgeni (Guest) katika simu hiyo.

Tendo la kuroot ndilo litakalokupa uwezo wa mtumiaji mkuu, yaani Administrator katika simu hiyo na hivyo utaweza fanya mengi ata yale yanayoweza haribu kabisa programu endeshaji hiyo.

Je utaweza fanya yapi kutokana na kuroot simu yako?

android-root-1.png

Ukiroot programu endeshaji ya Android ya simu yako utaweza kufanya mambo kama vile

* Kuweka apps ambazo kwa hali ya kawaida isingewezekana kabisa kuwekwa kwenye simu
* Kufuta (delete) apps na programu zilizokuja na simu husika ambazo kwa kawaida huwa huwezi zifuta. Apps hizi zinaitwaga Bloatware
* Kusasisha au kubadilisha kabisa toleo lako la Android. Ata kama mtengenezaji simu husika, iwe Samsung n.k bado hajakupa sasisho rasmi kwa ajili ya simu yako kuweza kupata toleo la kisasa zaidi la Android, kwa kuroot unaweza fanikiwa kupakia toleo la kisasa au ata kubadili kabisa
* Kufanya mabadiliko mengine mbalimbali kulingana na utakacho katika muonekano na utendaji kazi wa simu yako

Njia za Kuroot
Kuna njia nyingi sana kwa sababu suala la kuroot simu linategemea mambo mengi sana, mara nyingi njia ya kuroot simu flani haifanani na ya kuroot simu nyingine. Tofauti zinakuwa kwa kampuni kwa kampuni ya simu na ata saa nyingine tofauti zinakuwa kwa aina ya simu ata kama zinatoka kampuni moja.

Katika kuroot kwenyewe bila kujalisha app au programu au hatua utakazotumia, njia kuu ni mbili;

* Ya kutumia makosa ya programu endeshaji – Kupitia kufahamu makosa, yaani ‘exploits’ basi watengenezaji apps au programu wanaweza fanya programu/app iingie ndani kabisa ya Android ya simu yako na kukupa uwezo wa Admin, yaani simu ikawa ‘rooted’
* Kwa kuweka ‘Custom Recovery’ – Hii ni njia isiyo salama zaidi kwa kifaa chako ila pia ndiyo moja ya njia inayokuwa mara nyingi tofauti tofauti kwa kila kifaa.

Muhimu kufahamu

* Makampuni yenyewe ya simu sio yanayotoa njia za kuroot na kwa kiasi kikubwa huwa hawashauri ufanye jambo hili. Kama simu ina warranty basi kitendo cha kuroot kitaondoa sifa ya warranty hiyo.
* Ukikosea njia au ata kama umefanya kila kitu sahihi kama mambo yasipoenda vizuri basi Android inaweza nasa katika hali inayoifanya simu yako isiweze tumika. Hali hii inaitwa ‘Brick’ – yaani jiwe. Mara nyingi hii inamaanisha itakubidi uanze upya.

Tutakuletea njia mbalimbali maarufu za kuroot simu lakini kama unajiamini na unataka fanya mwenyewe basi mtandao wa XDA ni moja ya sehemu muhimu ya kuanzia. Kitu muhimu sana ni kuhakikisha unafuata maelekezo na kutumia mafaili husika kama maelezo ya jinsi ya kuroot simu hiyo husika. Njia hazifanani.

Je ushawahi kuroot simu yeyote? Waambie wengine ilikuwa ni simu gani na ulitumia njia gani?

starj4

Senior Member
Jul 2, 2016
143
195
Nadhan kila chenye faida huwa hakikos hasara, tuambie madhara yake n yap kwakuwa umetupa tu faida

pleo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,882
2,000
kuna ukweli wowote niki root nitaweza kutumia app za kulipia bila kufanya malipo Google play kama ni sahihi kwa kiasi gani?

NYANYADO

JF-Expert Member
Jan 8, 2013
3,439

Asante kwa maelezo mazuri, tafadhali weka maelezo ya jinsi ya ku root simu toka jukwaa la xda, au kingroot ili tuendelee vizuri na somo, pia anza kuaandaa ROM

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
7,985
2,000
kama hizo root hazinisaidii ku_patch adroid app basi haina umuhimu sana.
Kuna baadhi ya app zinazohitaji simu kuwa rooted ndio zitumike kwenye simu yako. Kwanza kuroot simu naona ni kuruhusu virus waingie kwenye simu kupitia app zinazotoka kwenye vyanzo visivyotambulika.

ericjames574

Member
Aug 30, 2015
44
125
Asante kwa maelezo mazuri, tafadhali weka maelezo ya jinsi ya ku root simu toka jukwaa la xda, au kingroot ili tuendelee vizuri na somo, pia anza kuaandaa ROM
Steps za kufuata ktk ku root
1. Tambua version ya cm yako Android 4.1,4.2,4.3,4.4,5.1 nk
2.kama version yako ni 4.1 au chini ya hapo tumia root master apk, kama ni 4.2 na kuendelea tumia kingo root apk
3.install hizo app nilizotaja hapo juu kisha fuata maelezo kwenye app

ericjames574

Member
Aug 30, 2015
44
125
Steps za kufuata ktk ku root
1. Tambua version ya cm yako Android 4.1,4.2,4.3,4.4,5.1 nk
2.kama version yako ni 4.1 au chini ya hapo tumia root master apk, kama ni 4.2 na kuendelea tumia kingo root apk
3.install hizo app nilizotaja hapo juu kisha fuata maelezo kwenye app
Faida na hasara
Faida
1.unaweza ku block ads ambazo hutumika kuleta vírus au kuiba taarifa zako
2 . kufuta mafaili yaliyokuja na cm hivyo kufanya cm kuwa nyepesi
3. Kuzuia mtu asifute app zako
4. Kurudisha picha au vídeos zilizofutwa

Hasara
1.kupoteza warantii

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom