LIKE
JF-Expert Member
- Dec 17, 2013
- 4,744
- 9,841
Aisee.. Huu uzi!
Kwanza mie nikienda kwa mtu yani mpaka naondoka naona kama kuna vitu nmeboronga kwa muda nlikuwa hapo.
Mpaka sasa hivi sijui kucheza mchezo wowote wa kijamii kama draft, bao, karata, pull table, yani mie hata baiskeli tu sijui kuendesha. Yote hii sababu ya kupenda kukaa peke angu.
Aisee hakuna mtihani mgumu kama kutembelewa na mgeni unaemuheshimu. Mimi hata mtu akiniita kunipa au kuniambia kitu flani huwa napata shida sana.
Hakuna kitu naumiaga kama nmeishiwa sasa nmfuate au nimpigie mtu anipige tafu!
Mungu mwema, sehemu ninayoishi nilichaguliwa mzee wa kanisa tena katika ujana wangu huu, hii imenisaidia angalau kidogo maana mara moja moja lazima usimame mbele ya watu kuongea. Na penyewe kabla ya kwenda kuongea unapata tabu sana tena unafika alafu baadhi ya point zinapotea.
Mke wangu ni muongeaji na huwa ana nisaidia sana hata tukiwa kwenye event flani flani linapokuja suala la mimi kutake place hasa kwenye maombi yeye ndio hufanya kwa Niaba yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app
huyo ni Mimi sasaaa
Sent using Jamii Forums mobile app