Kwa wajuzi/wazoefu wa computer za Apple

Prince Luanda

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
1,925
2,197
Kuna siku hapa Chuo (DIT) nilimuona mdau mmoja akipiga msuli laptop aliyokuwa akiitumia ni Macbook nilimfuata jamaa ili nimuulize machache kuhusu Macbook laptops kwa sababu na mimi nilitamani kumiliki siku moja.

Nilimuuliza hivi unatumiaje Macbook kwenye mambo yako hapa chuo kwa sababu kwenye somo la computer mara zote tunatumia software za Windows OS (Microsoft) halafu kwa sisi wanafunzi wa Civil Engineering kuna software kama vile ArchCAD, AutoCAD etc alizitumiaje kwenye PC yake?

Akanijibu kuwa ile laptop yake anaitumia bila shida so alichofanya aliizima na kuiwasha tena screen ikaleta interface ambayo inakutaka uchague kwenye process ya booting uswitch kwenda Windows OS au Mac OS, akachagua Window akanionyesha software za Window na kila kitu akafanya hivyo hivyo kwa kuchagua Mac OS.

Nilishangaa sana nikamuuliza kumbe ndivyo zilivyo. Then akaniambia kama nahitaji nimcheki. Sasa wadau naomba kuwauliza wajuzi wa humu hii kitu ndivyo ilivyo kwa Macbook zote au baadhi?

Naombeni mnijuze je inaweza kuwa fake?

Asanteni.
 
Sawa mkuu lakini uswitch kwenye Mac os inafanya kazi kama macbook kwanini?
hata ukiwa na laptop ya kawaida unaweza kuweka osx.

concept hapa ni kwamba mac na pc zote zinatumia architechture moja ya x86 hivyo unaweza kuweka operating system ya x86, sio windows tu unaweza weka distro za linux kama ubuntu hata ukaweka android x86.
 
Back
Top Bottom