Kwa wageni wote

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
772
Habari wana JF hususan wageni wanaoendelea kujiunga na waliojiunga. JF ni forum ya kuheshimika na hata Serikali inataitambua vyema.

Ni vyema tukakitumia chombo hiki kama kilivyokusudiwa na isiwe sababu ya kuonekana ni chombo cha upotoshaji jamii na uchonganishi baina ya Serikali na wananchi, sababu kuna watu wachache wana uelewa finyu kuhusu JF.

Tafadhali kitumie chombo hiki ipaswavyo na isiwe sababu ya kukipelekea kiwe katika mtazamo hasi, ikiwa mada huielewi wewe pita acha na usitoe maelezo usioyafahamu wala taarifa ambazo huna uhakika nazo zikasababisha upotoshaji,watu wa humu wote ni wale wenye fikra yakinifu na imezoeleka kujibizana na kubisha kwa hoja basi tusikurupuke.

Tafadhali kabla ya kuingia kwenye midahalo soma sheria na kanuni zinazoongoza JF ndio ujichanganye kwenye libeneke. Asanteni na Karibuni.
 
Siku hizi mtu akisema ukweli ama akitetea haki yake,ataitwa mchochezi ama mpotoshaji kwa jamii‍♂️
 
Back
Top Bottom