Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Alichosema chasha ni sahihi kabisa,mashine zinazotengenezwa hapa nchini ni usanii tupu,watengenezaji hawako serious na kazi.Kuzinunua ni kutupa pesa tu pasi na sababu yoyote ya maana.Hata hizi zinazotumia umeme bado ufanisi wake ni mdogo sana kiasi kwamba haziwezi kukupa faida.Kama uko serious na kazi pata machine kutoka nje ya nchi,mfano China au Italy huko utapata za uhakika.Kisha nunua generator kwa ajili ya emergence hapo utatengeze pesa,haitakiwi kufanya biashara kwa kubahatisha.

Asante kwa ushauri Kichwa mbovu, nitaufanyia kazi.
 
Mkuu tunashukuru kwa elimu unayotupatia.mimi niliweka vifaranga wa malawi na katika siku ya kwanza hadi ya tano niliwapatia mchanganyiko huu glucose, otc plus na trimazin.je natakiwa kurudia tena mchanganyiko huu kwenye hiyo siku ya 16?

Pia vifo vilikua vingi na baadhi ya dalili ulizozitaja kama kushusha mabawa,kusinzia niliziona nikawapatia ctc20% je ilikuwa sahihi? Na kama kuna nyongeza juu ya hili nitashukuru zaidi.

Asante
 
Chasha asante sana kwa ushauri wako, ukiwakuta hao watengenezaji wa kibongo jinsi wanavyozifagilia nane nane utasema nimepata.

Mkuu ni kweli kabisa na Tatizo ni kutafuta Utajiri wa Harakaharaka, Niliwahi kuhudhuria maonyesho ya Nanenae Arusha, nikakutana na Mvumbuzi wa Incubators nilipo muuliza ana muda gani tangu agundue hii mashine aliniambia ni kama miezi miwili, na hapo alikuwa nauza na si kuonyesha,

Nilazima wavumbuzi wa Tanzania waache tamaa ya pesa na kuwekeza zaidi kwenye utafiti kabla ya kuja na product inayo weza kushindana kokote
 
Wadau naombeni leo mniwie radhi nimeshinda nikifinya kazi za field huko msata toka asubuhi. Nilikuwa na zoezi la kuwapa chanjo ng'ombe. Ndio maana leo sijapatikana hewani.Endeleeni tu kutuma maswali yenu na kesho mungu akipenda nitayatolea ufafanuzi.
 
Mkuu tunashukuru kwa elimu unayotupatia.mimi niliweka vifaranga wa malawi na katika siku ya kwanza hadi ya tano niliwapatia mchanganyiko huu glucose,otc plus na trimazin.je natakiwa kurudia tena mchanganyiko huu kwenye hiyo siku ya 16? Pia, vifo vilikua vingi na baadhi ya dalili ulizozitaja kama kushusha mabawa,kusinzia niliziona nikawapatia ctc20% je ilikuwa sahihi? Na kama kuna nyongeza juu ya hili nitashukuru zaidi.

Asante

Hapo ilitakiwa utumie Vitalyte ikichanganywa na hiyo trimazin 30% na ni lazima urudie siku ya 16-20. OTC plus inatakiwa ijitegemee kwani ina Antiobiotics na vitamin.Inapendekezwa OTC Plus itumike siku ya 24-27 ili kuwakinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na kuwafanya wawe na afya njema. Kwenye ctc 20% hukuwa sahihi,dawa hii inawafaa zaidi kuku wakubwa.
 
Mkuu Kichwa vipi kuhusu Chakula cha Kuku hao Chotara na wakienyeji na lazima kiwe Pure na cha hawa kuku wa kisasa? na kwenye kutamisha mayai ukitumia ile njia ya Kuchagua sex ya mayai unaweza fanikiwa kutotoresha Majogoo tupu au Majike tupu?

Kimsingi chakula ambacho kuku wa kisasa anakula hata kuku wa kienyeji anakula,hakina shida 'isipokuwa kuku wa kienyeji ana uwezo mkubwa zaidi wa kujitafutia chakula chake mwenyewe ukilinganisha na kuku wa kisasa na hivyo kwake chakula maalum ni kama supliment.

Ingawa inapendekezwa kama unahitaji ufanisi uwe mzuri kwenye ukuaji ni muhimu kuku wa kienyeji/chotara wakafugwa kisasa na wakapewa chakula maalum ambacho kuku wa kisasa waapewaPia ni muhimu kuzingatia chanjo na tiba kwani magonjwa ambayo kuku wa kisasa anapata pia na kuku wa kienyeji au chatara hupata.

Kuhusu kuzalisha vifaranga kwa kufanya sexing kwa kutumia mayai inawezekana lakini haiko accurate ndio maana watu wanaojaribu kufanya hivyo hushindwa na kuamua kuzalisha kawaida na mwaisho hufanya sexing kwenye vifaranga waliozaliwa.
 
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajiriwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

Mkuu, tumekusoma sana! Pia umeni tamanisha, tatizo hukuweka wazi ni jinsigani naweza kuku pata kani hata namba huku weka!
 
Mkuu Kichwa Mbovu

Ni vifaranga wa mayai toka Kampuni gani una recommend mtu kufuga? Vifaranga ambao hawafi sana na wanataga vizuri
 
Mkuu Kichwa mbovu asante sana kwa hii elimu unayotupa, ingawa jina yako humu JF haiendani na nondo hizi.

Mimi nafuga kuku wa mayai (kisasa) 550, wiki ya 12 sasa, pia nafuga kuku wa kienyeji sio chotara, kwa nje. Huwa nawatreat wote (layers na wa kienyeji) na wanarespond vizuri na sijapata scare ya magonjwa. Kuku wa kienyeji wamerespond vizuri as nilianza nao 10 tu ila wanatagiana na kuangua vifaranga sana ninao sasa kama vifaranga 40, wa saizi tofauti wengine wakubwa na wadogo, nimewaacha na mama zao maana nilijaribu kuwafungia wenyewe na kuwalisha , hawa vifaranga, hawakurespond vizuri. Nawafungia na mama yao kwa muda (kunguru nouma) alafu nawaachisha mama zao wakatage tena. Nafugia kwenye compaund yangu eneo la 30 by 60 enclosed walls.

Swali: Nafikiria kuleta majogoo ya chotara, ili wapande hawa kienyeji nipate kuku bora kwa ajili ya kuuza nyama, yaani niachane kiasi na pure kienyeji. Nia yangu mayai yakitagwa yatamiwe na hawa wa kienyeji ili nitoe vifaranga vikue niuze kuku wa nyama, kwani wa kienyeji maumbo madogo kama usemavyo. Sasa kwa baadhi majibu uliyokuwa unatoa kwenye hii mada nimepata ujumbe kuwa lazima nipate parent stock kutoka nje? au sikukupata vizuri? kwamba haya mayai mpaka yawe treated lasivyo vifaranga havitakuwa na afya? lakini ni wa kienyeji ndio wanataga sio hawa chotara....bado sijafikia hatua ya kutotolesha na mashine...Natanguliza shukrani, Mola akubarik zaid,
 
Hapo ilitakiwa utumie Vitalyte ikichanganywa na hiyo trimazin 30% na ni lazima urudie siku ya 16-20. OTC plus inatakiwa ijitegemee kwani ina Antiobiotics na vitamin.Inapendekezwa OTC Plus itumike siku ya 24-27 ili kuwakinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na kuwafanya wawe na afya njema.Kwenye ctc 20% hukuwa sahihi,dawa hii inawafaa zaidi kuku wakubwa.

Nashukuru sana mkuu.pia kuna baadhi ya vifaranga kama watatu wa umri wa wiki 5 wamkua wakivimba jicho je hii ni dalili ya upungufu wa vitamin au ugonjwa mwingine?? na nawezaje kuzuia hiyo hali??je ni sahihi kutumia vitastress badala ya vitalyte?asante
 
Mkuu hivi kuna Kampuni zinazo uza Incubatos za kutoka Nje unazo zifahamu? Make naona mauza uza tu,
 
Mkuu hivi kuna Kampuni zinazo uza Incubatos za kutoka Nje unazo zifahamu? Make naona mauza uza tu,

Ndio mheshimiwa Chasha nina mawasiliano na makampuni kama matatu hivi yanayotengeneza kuuza Incubator,moja kutoka Uingereza,nyingine kutoka Italy na ya tatu kutoka China.Wengi niliowafanyia mpango na kuagiza hizo Incubators waliagiza kutoka china.Italy na Uingereza mashine zao ni ghali sana.
 
Vipi hayo makampuni yako Tanzania? ya za kutoka Italy na Uingereza ni ghali sana hata kutoka South Africa ni ghali mno, kuna moja ya China nina mawasiliano nayo, ila ishu iko Bandarini make kuna jamaa amenipigia ghalama za Babdalini ni kubwa kuliko bei ya Mashine yenyewe tena mara tatu, ila sijajua kama Incubators ziko kwenye orodha ya msamaha wa Kodi, na kuna jamaa wa china walikuwa wamenitumia proformal invoice kabisa ila ghalama za Bandalini ndo kisiki
 
Nashukuru sana mkuu.pia kuna baadhi ya vifaranga kama watatu wa umri wa wiki 5 wamkua wakivimba jicho je hii ni dalili ya upungufu wa vitamin au ugonjwa mwingine?? na nawezaje kuzuia hiyo hali??je ni sahihi kutumia vitastress badala ya vitalyte?asante

Nakushukuru ndugu Dafo kwa swali lako.Kifupi dalili ya vifaranga kuvimba macho inaweza ikawa ni magonjwa mawili ambayo yote yanakuwa na hizi dalili.Ugonjwa wa kwanza ni upungufu wa Vitamin A.Kifaranga mwenye ugonjwa huu huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowana.Kuku wenye huu ugonjwa mara nyingi huwa hawaponi,wanakufa.
Ugonjwa huu kwa kawaida hujitokeza baada ya kpindi kirefu cha kiangazi.Kinga ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara.Pia kuku wote wapewe dawa ya vitamin mfano vitalyte,antistress,amin'total,multivitamin,supervit etc.ili kuzuia kujitokeza kwa ugonjwa.

Ugonjwa mwingine unaonyesha dalili za kuvumba macho ni ugonjwa wa mafua ambayo ni haya kawaida sio yale mafua makali ya ndege.Dalili za mafua (Infectious coryza) ni pamoja kuvimba macho,kuziba macho,huanza jicho moja na badae jicho la pili.Pia kama utapata nafasi ya kuwasikiliza vizuri hasa wakati wa usiku utasikia wanakoroma.Pia kutokwa kamasi puani na kupiga chafya.Ugonjwa huu unatibiwa na dawa moja inaitwa Coridix au tylosine 75%

Kuhusu antistress unaruhusiwa kutumia madala ya vitalyte kweni nayo ipo kwenye kundi la dawa za vitamin.
 
Mkuu Kichwa mbovu asante sana kwa hii elimu unayotupa, ingawa jina yako humu JF haiendani na nondo hizi.

Mimi nafuga kuku wa mayai (kisasa) 550, wiki ya 12 sasa, pia nafuga kuku wa kienyeji sio chotara, kwa nje. Huwa nawatreat wote (layers na wa kienyeji) na wanarespond vizuri na sijapata scare ya magonjwa. Kuku wa kienyeji wamerespond vizuri as nilianza nao 10 tu ila wanatagiana na kuangua vifaranga sana ninao sasa kama vifaranga 40, wa saizi tofauti wengine wakubwa na wadogo, nimewaacha na mama zao maana nilijaribu kuwafungia wenyewe na kuwalisha , hawa vifaranga, hawakurespond vizuri. Nawafungia na mama yao kwa muda (kunguru nouma) alafu nawaachisha mama zao wakatage tena. Nafugia kwenye compaund yangu eneo la 30 by 60 enclosed walls.

Swali: Nafikiria kuleta majogoo ya chotara, ili wapande hawa kienyeji nipate kuku bora kwa ajili ya kuuza nyama, yaani niachane kiasi na pure kienyeji. Nia yangu mayai yakitagwa yatamiwe na hawa wa kienyeji ili nitoe vifaranga vikue niuze kuku wa nyama, kwani wa kienyeji maumbo madogo kama usemavyo. Sasa kwa baadhi majibu uliyokuwa unatoa kwenye hii mada nimepata ujumbe kuwa lazima nipate parent stock kutoka nje? au sikukupata vizuri? kwamba haya mayai mpaka yawe treated lasivyo vifaranga havitakuwa na afya? lakini ni wa kienyeji ndio wanataga sio hawa chotara....bado sijafikia hatua ya kutotolesha na mashine...Natanguliza shukrani, Mola akubarik zaid,

Hongera mheshimiwa Madago kwa kuendesha huo mradi wa kuku wa mayai na wa kienyeji.
Kuhusu majogoo ,ni vyema ukapata ya kisasa kabisa yani pure mfano majogoo wekundu Rhode Island red au wale Barred polmouth rock au hybrid yake hawa majogoo ambao ni kaka wa hao kuku wa mayai.Ikikosacross inakusaidia kuboresha ile kosaafu yako na kukuwezesha ufuge kibiashara na kupata faida.

Kwa huo mradi wako wa kuku wa kienyeji huna haja ya kuwa na parest stock wala kutreat mayai kwani project yako ni nndogo.Dawa za kutibia mayai ni ghali kidogo inahitaji wale wenye miradi mikubwa ya utotoreshaji.Utibuji wa mayai huongeza kiwango cha utotoreshaji wa idadi ya mayai,pia huzuia magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa mama kwenda kwa vifaranga.Na pia huwafanya vifaranaga wanaozaliwa kuwa wenye afya wakubwa na wenye afya njema.

Wale vifaranga ilitakiwa uwawekeechanzo cha joto pia uwape zile dawa za kuzuia magonjwa ya vifaranga mfano Ugonjwa wa pullorum na coccidiosis Na pia wangepatiwa chonjo ya mdondo pamoja na Gumboro.
 
Hongera mheshimiwa Madago kwa kuendesha huo mradi wa kuku wa mayai na wa kienyeji.
Kuhusu majogoo ,ni vyema ukapata ya kisasa kabisa yani pure mfano majogoo wekundu Rhode Ireland red au wale Barred polmouth rock au hybrid yake hawa majogoo ambao ni kaka wa hao kuku wa mayai.Ikikosacross inakusaidia kuboresha ile kosaafu yako na kukuwezesha ufuge kibiashara na kupata faida.

Kwa huo mradi wako wa kuku wa kienyeji huna haja ya kuwa na parest stock wala kutreat mayai kwani project yako ni nndogo.Dawa za kutibia mayai ni ghali kidogo inahitaji wale wenye miradi mikubwa ya utotoreshaji.Utibuji wa mayai huongeza kiwango cha utotoreshaji wa idadi ya mayai,pia huzuia magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa mama kwenda kwa vifaranga.Na pia huwafanya vifaranaga wanaozaliwa kuwa wenye afya wakubwa na wenye afya njema.

Wale vifaranga ilitakiwa uwawekeechanzo cha joto pia uwape zile dawa za kuzuia magonjwa ya vifaranga mfano Ugonjwa wa pullorum na coccidiosis Na pia wangepatiwa chonjo ya mdondo pamoja na Gumboro.

Mkuu hapo kwenye Red, kwani nilazima kuwe na Mradi mkubwa ndo Utibu Mayai? nikiwa natotoresha mayai 1000 sihitaji kutibu hayo mayai?
 
Kwahiyo KM kama nimekuelewa vema, nikishawapata hao Rhode Island kwa mfano, waka-cross na hawa wa kienyeji nliokuwa nao, mayai yatakayokua yanatoka hayana shida kuku hawa wa kienyeji wakilalia ili watotoe? Nauliza hivi kwa sababu nimeshawahi kuuziwa mayai kutoka kwa mtu mwenye hawa machotara nikawawekea hawa wangu wa kienyeji walalie lakini outcome yao nimeshindwa kufaidika nayo. Namimi naomba uni pm namba yako tafadhali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom