Kuna tofauti Kubwa katika Tv hizi za Flat,kuna za LED,LCD,Plasma na OLED. Nitaelezea tofauti ya LED na LCD.
Kwa Kawaida asilimia 95% ya maduka yanayouza TV hizi wengi wa wauzaji hawafahamu tofauti ya hizi tv huishia kusema hii iko clear na ile iko clear ile mbaya. ama maduka mengi baadhi ya Tv huzimwa na kuwashwa baadhi na huishia Kusema umeme ukweli ni kwamba Pindi zitapowashwa zote Mteja mwerevu na mwenye ushirikiano na macho yake ataweza kugundua tofauti ya Tv hizo,kutokana na hilo watu wengi wamekua wakiuziwa tv za LCD kwa thamani ya LED. na huamini TV ile ndio bora zaidi,Acha kujidanganya hata Tv ya Kichogo (CRT TV (cathod RAy Tube)) nayo ni Clear hata kukaribia LED.
LED TV - ni aina ya LCD tv inayotumia
light-emitting diodes (LED) kama backlight,
LCD Tv - in aina ya tv zinazotumia
cold cathode fluorescent lights (CCFLs).
TV za LCD ni rahisi kupasuka Kioo chake
Tv za LCD ukitaka ijua Bonyeza Kioo utaona kama ukungu waKijivu,ukiexpand toka ulipo bonyeza.
tv za LED hutumia (diode)ndogo sana. tv hiz sio rahis kupasuka Kioo chake hasa za makampuni kama Makampuni makubwa kama Sony,Lg,samsung,Toshiba,Sharp,Vazio na nyingine. kwa hizi za china sinauzoefu nazo.
Tazama Picha hii hapa utaona tofauti ya LCD na LED.
Picha ya LED inakua angavu na Rangi Kamili. Kamaunavyo hapo rangi nyeusi kwa lCD imekua kama imepauka. kwa LED imekua angavu zaidi..
Pia LCD Tazama samaki wake Muonekano wake Kisha Fananisha na muonekano wa LED samski wake walivyo.
Tazama rangi ya Mchezesha samaki hao Rangi ya Blue ya LCD imekolea zaidi Kwa LED imeoneshwa Rangi Halisi
Tazama mChezesha samaki wa LCD muonekano wake ulivyo,ni mweupe zaidi(kupauka) kisha mtazame wa LED alivyo na rangi Kamili na anaonekana Sura japo kidogo unaweza kusimulia sura yake.
Kwa hayo machache yatakusaidi kutafuta TV nzuri. ningekua Dar ningekukaribisha dukani kwetu ila sie tupo Moshi.