Kwa wafanyabiashara wa vifaa vya electronics nisaidieni tafadhali

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Natumai mu wazima wote naombeni kufahamishwa bei ya vitu hivi kwa wanaovifahamu bei zake.Tv ya LCD inch 42 na 52 aina ya Sony na, Tv ya LCD inch 42 na 52 aina ya Samsung.tafadhalini nisaidieni ninahitaji kununua ikiwezekana na duka linalouza vifaa hivyo original kwa kariakoo
 
Natumai mu wazima wote naombeni kufahamishwa bei ya vitu hivi kwa wanaovifahamu bei zake.Tv ya LCD inch 42 na 52 aina ya Sony na, Tv ya LCD inch 42 na 52 aina ya Samsung.tafadhalini nisaidieni ninahitaji kununua ikiwezekana na duka linalouza vifaa hivyo original kwa kariakoo
Ndugu yangu jaribu pale mlimani city utapata hizo tv unazotaka akini bei ni shughuli Mimi nilinunua tv samsung 40 inch 3D toleo namba saba maana hawa samsung wanatoa kwa matoleo kama tamdhilia vile. hiyo tv nilinunua Euro 800 kama madafu 1.824.000 hapo mlimani nimeiona wanauza milioni nne tena hupewi hata miwani ya 3D
 
Miwani inakufanya kuhisi kuwa upo eneo la tukio, maana utaona engo tatu mbele, kati na nyuma kama vile unavyotazama live sehemu kwa macho yako sio picha.<br />
Miwani ya 3D ina kazi gani? Na nini maana ya TV ya 3D
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;
 
utadawazi bwana...mimi naendelea na nchi 15 yangu...hitachi
 
Mkuu Mlimani City wala usithubutu kwenda. Nilijaribu kufanya window shopping mwezi Disemba mwaka jana nikakuta kuwa bei ya Mlimani city ni kubwa mno kulinganisha na mjini. e.g LCD full HD ya Samsung ya inchi 32 Karikaoo kwa wakala wa Samsung ambaye anakupa waranti ya miaka 2 ilikuwa around laki nane wakati mlimani city ilikuwa 1.3 mil. Sikumbuki vizuri bei ya inchi 42 ila tembea mtaa wote wa Uhuru ukiliganisha bei tena angalia kwa wale ambao ni mawakala wa hiyo brand. Baada ya mtaa huo nenda JM Mall kuna duka kubwa sana pale ila bei zao ziko juu kidogo. Kwa Sony original nenda pale Samora kwa wakala wa Sony japo pia bei zao ziko juu kidogo ila nafuu ukilinganisha na Mlimani City.
 
Kuna tofauti Kubwa katika Tv hizi za Flat,kuna za LED,LCD,Plasma na OLED. Nitaelezea tofauti ya LED na LCD.

Kwa Kawaida asilimia 95% ya maduka yanayouza TV hizi wengi wa wauzaji hawafahamu tofauti ya hizi tv huishia kusema hii iko clear na ile iko clear ile mbaya. ama maduka mengi baadhi ya Tv huzimwa na kuwashwa baadhi na huishia Kusema umeme ukweli ni kwamba Pindi zitapowashwa zote Mteja mwerevu na mwenye ushirikiano na macho yake ataweza kugundua tofauti ya Tv hizo,kutokana na hilo watu wengi wamekua wakiuziwa tv za LCD kwa thamani ya LED. na huamini TV ile ndio bora zaidi,Acha kujidanganya hata Tv ya Kichogo (CRT TV (cathod RAy Tube)) nayo ni Clear hata kukaribia LED.


LED TV - ni aina ya LCD tv inayotumia light-emitting diodes (LED) kama backlight,
LCD Tv - in aina ya tv zinazotumia cold cathode fluorescent lights (CCFLs).
TV za LCD ni rahisi kupasuka Kioo chake
Tv za LCD ukitaka ijua Bonyeza Kioo utaona kama ukungu waKijivu,ukiexpand toka ulipo bonyeza.

tv za LED hutumia (diode)ndogo sana. tv hiz sio rahis kupasuka Kioo chake hasa za makampuni kama Makampuni makubwa kama Sony,Lg,samsung,Toshiba,Sharp,Vazio na nyingine. kwa hizi za china sinauzoefu nazo.


Tazama Picha hii hapa utaona tofauti ya LCD na LED.
Dolphin_sharp_and_blur.jpg

Picha ya LED inakua angavu na Rangi Kamili. Kamaunavyo hapo rangi nyeusi kwa lCD imekua kama imepauka. kwa LED imekua angavu zaidi..
Pia LCD Tazama samaki wake Muonekano wake Kisha Fananisha na muonekano wa LED samski wake walivyo.
Tazama rangi ya Mchezesha samaki hao Rangi ya Blue ya LCD imekolea zaidi Kwa LED imeoneshwa Rangi Halisi
Tazama mChezesha samaki wa LCD muonekano wake ulivyo,ni mweupe zaidi(kupauka) kisha mtazame wa LED alivyo na rangi Kamili na anaonekana Sura japo kidogo unaweza kusimulia sura yake.



Kwa hayo machache yatakusaidi kutafuta TV nzuri. ningekua Dar ningekukaribisha dukani kwetu ila sie tupo Moshi.
 
Back
Top Bottom