Harakati za Mawinga wa kariakoo na ghadhabu wa wateja

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,020
5,439
Habari zenu.

Nilifika kariakoo kwa lengo la kutafuta spea za pikipiki yangu aina ya tvs na baadhi ya vifaa vya electronics.

Lililonifedhehesha ni hili, nilikuwa na shida na ''Tv Guard'', nikaanzia mtaa wa congo kuulizia bei.

Huku nikiwa nafahamu bei yake, nami bajeti yangu ilikuwa bei yake isizidi elfu 10.

Duka la kwanza, akanambia elf 20 mwisho akaishia elf 15, nikamwambia nina elf 7, akagoma nikasepa zangu.

Duka la pili, akanambia elf 25 mwisho akaishia elf 22, nikampa bei yangu elf 7 malengo yangu ni elf 10, akakataa nikaachana naye nikaondoka zangu.

Duka la tatu, akanambia elf 30 mwisho elf 25, akaniuliza kwani una bei gani?, nikamwambia nina elf 7 akasema haimlipi,Nikaondoka.

Duka la nne, akanambia elf 35 mwisho elf 30, akaniuliza una bei gani?, nikampa bei yangu ileile ya elf 7 tu , ila malengo yakiwa ni kuishia elf 10, akagoma nikaenda zangu.

Kitu ambacho nilikuwa nikijiuliza, kwanini kila ninapoenda bei inapanda!!

Nikaelekea mtaa wa Narung'ombe;

Duka la kwanza, akanambia elf 20 mwisho elf 15, nikampa elf 7 yangu tu ileile, akakataa nikaondoka.

Duka la pili, akanambia elf 15, nikajua hapa nitanunua hata kwa ten, yumbana naye, akapunguza buku tu, nikamwambia nina elf 7, akagoma nikaongezea hadi ikafika elf 10, akagoma akanambia bei ya mwisho ni elf 13 kama huna badi. Nikafikiria na kwa namna nilivyozunguka, nikaona isiwe tabu nikampa elf 15 akanirudishia chenji yangu. Nikachukua tv guard yangu, nikaondoka.

Ila hata hivo roho iliniuma sana kutoa hiyo elf 13.

Ushauri; wakuu tujifunze kufanya window shopping kabla ya kufanya maamuzi ya kununua kitu chochote. Au unaenda duka moja unatajiwa bei unaamua kununua hapohapo. Tunaliwa parefu wakuu.

Hawa mawinga wanapandisha sana bei za bidhaa, hawafai hata kidogo. Ukiwaona wakimbie kama ukoma.
 
Sasa hivi ni wengi , hapa nina marafiki kibao mawinga..Sasa hivi status zao unakuta bidhaa ile ile na picha ile ile ila kila mtu na bei yake ...Hamna bidhaa mpya kabisa bei ni tofauti.

Naona watu wawe wabunifu angalia la sivyo soko kwao litakuwa gumu sana.
 
Ndiyo nachofanyaga, hasa vitu vya electronics.... Huwa na google bei kabisa kabla sijaenda kununua.....

Nikija kwako kununua nakuwa na idea na bei ya bidhaa husika, najumlishia na VAT kabisa...
 
Back
Top Bottom