Kwa viongozi wa zanzibar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa viongozi wa zanzibar.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JAMVI, Jun 7, 2012.

 1. J

  JAMVI New Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu

  Rais wa Zanzibar; DR. MOHAMMED ALI SHENI .
  Makamo wa Kwanza wa Rais; Maalim SEIF SHARIF HAMAD.

  Kumbukeni Allah S.w amekuteuni kuwa ni viongozi wa kuu, wa Taifa letu la Zanzibar,chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.Serikali isiyotawaliwa na Ushabiki wa vyama vya Kisiasa ambao uliwagawa wa Zanzibar kwa misingi hiyo.Kwa hilo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kuunganisha nyoyo zetu Wazanzibari.Nifika kuna miongoni mwetu hawalipendi hilo.

  Ndugu zangu viongozi wapenzi,Kumbukeni ahadi mlizotoa za kuwatumikia wananchi,kutetea maslahi yao,kusimamia umoja, mshikamano ,amani, utulivu , kwa maslaha ya Taifa letu. Tulikuchagueni baada ya kuwa na imani kwenu na bado hatujaondosha imani hiyo. Ndugu zangu, Fahamuni kwamba mlikubali kuwa ni viongozi na wakilishi wa wananchi na sio watawala kwa hivyo hiyo ni amana na kila mmoja ataulizwa kwa amana yake. Kumbukeni kwamba wale ambao mliwaita na wakaitika kwa kampeni, rai, ushawishi,nasaha,kuwasikitikia,na kwa gharama zote wawe pamoja nanyi jua , mvua,njaa,usiku mchana,wengine kupata majeraha,kufariki kwa ajali katika kipindi cha kampeni, mlifurahi kwa wingi wao na mapenzi yao kwenu walishikamana nanyi bega kwa bega kwasababu ni letu sote. SASA ndio WALEWALE, kwa IMANI waliokuwa nayo KWENU kama ni VIONGOZI na WAWAKILISHI wao,katika JAMBO KUBWA la mustakbali wa NCHI yao, na baada ya kuona kwamba mmelipuuzia hilo, wameamua KUPAZA SAUTI zao ,Kina BABA, VIJANA,MAMA ZETU, DADA ZETU ili mlipigie mbio mmekua wa guumu Jee pana nini hapa? Jee mmerubuniwa? Jee mmegeuka na kuvaa ngozi ya chui? .Mlipowajia mliwaita kwa sauti za kiduumu ,daima, haki, sawa,wazanzibar oyeee !!! na wakaitikia. LEO wamekuja kwenu wapaza sauti zao, na kuingia barabarani kwa amani ili muwaone na muwasikie katika jambo ambalo mlistahiki nyie ndio muwe mbele na wao wawe nyuma au bega kwa bega nanyi. Baada ya kuuona mmelifumbia macho wameona wanyanyue sauti zao kukumbusheni wajibu wenu na wasingefanya hivyo isipokua kwa kujua kuwa mtajali na kuthamini madai ya nchi yetu kwa pamoja ZANZIBAR. Lakini busara na jazaa yenu ,malipo yenu kwao ,ni kuwapiga , kuwatesa , kuwatia vilema, kuwatia ndani na kuwatafutia magari na mabomu ya pilipil mkawarushia !!!!! Nakuwafungulia kesi mahakamani,kwa ushawishi tu wawatu fulani wasioitakia kheri Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, wanafurahi wanapoona twasokotana kila siku.

  Ndugu Raisi, Ndugu Makamo wa Rais ,wawakilishi na wabunge, mmehisi kuwa hayo ndio malipo yao na hongera yenu kwao ya kuweko madarakani? Msitusaliti,tumekupeni madaraka, tumekupeni nguvu ,tumieni nguvu tulizokupeni kutetea maslahi yetu na ya nchi yetu Zanzibar, nasio kutudhoofisha.Tunakuaminini jiaminini,mtajenga heshima yetu na ya nchi yetu.Mmeshindwa udereva tupeni wenyetu msitutie msingini kwa kuwaridhisha waliochapia njiani.Ondoeni Muhali,Muhali wa wazee wetu kwa Julius Nyerere umekwisha,na maradhi haya ndo yalotufikisha hapa,Umakamo wa Uraisi haupo,ati mgombea mweza! ni sawa na mpambe wa Bw Harusi huishia mlangoni tu hana lake jambo katika maamuzi ,Rais wa Zanzibar hana chake,Raslimali zetu ziwe zao na zao zao!.Mwisho wamesubutu kusema sisi hatuna nchi na ukweli ndio huo! SASA wazanzibar wataka nchi yao,hakuna ndoa isio natalaka! Mzee karume alisema “Muungano mwisho Chumbe” akiimanisha kila nchi na mipaka yake.”Muungano ni sawa na koti “ akiimanisha joto likizidi unalivua. Sasa halina joto tuu,limezalisha kunguni tele wametuzonga mpaka masikioni.Mzee karume alifahamu hivyo na nnawasiwasi ufahamu huo ndio ulo pelekea kifo chake Mungu amrahamu . Sasa Muungano ni nyavu, nyavu ya samaki kwa wazanzibari,wakitaka kujizongoa ndio inawazonga zaidi. Kauli ya viongozi kuimarisha Muungano ,sijengine wala sikutatua kero zake ,bali ni kuendelea kuibana Zanzibar ili ipoteze mamlaka yake, raslimali zake, ifikie kuwa ni kijiji au kata tu katika Tanganyika, uzoefu unaonyesha hivyo,bali ndio sera ya C.C.M, toka Serikali mbili kwenda moja.Muungano aina hii dunia nzima hakuna, matokeo yake imekua ni muumano badala ya Muungano sisi twaaumia nyinyi viongozi kama hamna uchungu nayo kwa sababu ya muhali na maslahi ya muda mfupi mnayoyapata nyinyi na familia zenu, sisi tunaangalia mustakbali na vizazi vijavyo. Muungano wa SERIKALI MOJA NA MBILI HATUUTAKI NA USHAPITIWA NA WAKATI.

  Mheshimiwa Rais ,Makamo mawaziri,Wawakilishi,wabunge :Na jua ninayoyazungumza miongoni mwetu yanawakera kweli kweli, hawa siwazanzibari khalisi, na wala hawaitakii mema Zanzibar, sitaki kutumia neon WAZANZIBARA kwani katika hao wanaitakia kheri Zanzibar kama sisi tunavyoitakia kheri Tanganyika lakini hao ni wanafiki wa Taifa letu, utawaona ni wenzetu lakini maadui zetu,tuhadhari nao. Eee Mungu Allah tufichulie tuwajue,na hawa ndio sababu ya fitna zote Zanzibar.NDUGU ZANGU, kuweni viongozi na msiwe watawala mtaangamia, wakowapi kina Firauni dhil autaad, Thamoud ,Aadi na Naamrudh ?Na wengine wengi mnawajua katika karne zenu hizi wako wapi? Walijifanya watawala, wakatakabari kwa Allah Mwenyezi Mungu Muumba, na wakatakabari kwa watu wao , raia wao, Allah akawaangamiza,akawapokonya madaraka, na akawapa wanyonge wasiokua na guvu.
  Kwani” Allah anampa ufalme anaemtaka na humpokonya anaemtaka, na humpa nguvu anaemtaka na humuondoshea anaemtaka”….(Al-quran)
  Ndugu viongozi, Shikamaneni na wananchi pamoja ,sikilizeni malalamiko yao na sauti zao,zifanyieni kazi wala MSIWASALITI na KUONYESHA TAKABURI kwani nyinyi tegemeo lao.
  ALLAH ,Eeh Mwenyezi Mungu, ibariki Zanzibar , watu wake na raslimali zeke , wabariki viongozi wetu wote , Rais na Makamo zake,na wananchi wote.Tuungane katika kuitetea Zanzibar,Yaarabi tupe nguvu tuitetee nchi yetu na Jamhuri yetu .Eee Allah tujaalie tuishi vizuri na majirani zetu na ndugu zetu wa Tanganyika hatunachuki na ndugu zetu watanganyika . Tulinde na maadui zetu wasioitakia mema Zanzibar, na tufichulie wanafiki miongoni mwetu. Aamin.
  Eee Allah shuhudia kuwa nimewafkishia .

  Mimi ni Mzanzibari.
   
 2. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu binadamu hajui thamani ya kitu alichonacho mpaka akipoteze.
   
 3. S

  Simbaarobaini7 Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamvi you are great and I liked your talk. Kama wanainchi wa kawaida wa Zanzibar wanaona hivyo basi madai ya Wazanzibari jamani yasikilizwe. Ingawa mimi ni muumini wa Muungano maneno yako Jamvi yameni-touch sana. CCM na Viongozi wanang'ang'ania Muungano kwa maslahi yao binafsi ndio maana hawataki ujadiliwe kwenye Tume ya Katiba. Its high time kuwasililiza Wazanzibari kama wanataka kujitenga let it be! Wapeni refererundum ya Muungano watakaoshinda na iwe hivyo. Mbona kule Canada jimbo la Quebbec lilitaka kura ya maoni ya kujitenga ilipopigwa wengi walikataa na leo Quebbec ni sehemu ya Canada. Do the same to Zanzibar and upheld thei opinion badala ya kutumia nguvu za Dola kulinda Muungano usiotakiwa upande mwingine wa huo Muungano. Bravo JAMVI, ALUTA CONTINUA!
   
 4. Z

  ZIGZAG Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana endelea kuwaelimisha viongozi wetu wa znz hawa ndio zaid wakiamua hata kesho suala la muungano litawezekana kama ilivyowezekana serikal ya mseto. kwa upande wa tanganyika wala hakuna tatizo ni shwar tu.
   
Loading...