Kwa vijana wa CHADEMA – Chama kinamjenga mtu, si mtu kukijenga chama

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,863
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na wimbi la baadhi ya vijana waliowahi kuwa wanachama wa CHADEMA kujiondoa au kuhama chama hicho kwa madai ya kubaguliwa, kupuuzwa au kutotendewa haki. Wengine wamelalamika kuwa juhudi zao hazitambuliwi, na hivyo kuamua kusaka hifadhi sehemu nyingine. Hata hivyo, ni muhimu kwa vijana hawa na wengine wanaofikiri njia hiyo kuwa suluhisho, kutafakari kwa kina historia ya siasa za Tanzania na mafanikio halisi ya watu waliokuzwa na vyama, hasa CHADEMA.

Kwanini Ulijiunga na CHADEMA?
Vijana wengi waliivutiwa na CHADEMA si kwa sababu walikijua chama hicho tangu kianze, bali kwa sababu kilikuwa chama salama kwao. Chama kilichoonyesha dira, mwelekeo, na msimamo thabiti katika kudai haki, demokrasia, utawala bora na usawa katika taifa letu. Waliona ndoto zao na matumaini yao yakitafsiriwa kupitia mikutano, maandamano ya amani, mijadala ya hoja nzito bungeni, na sauti ya wapinzani waliokuwa imara.

Chama Kinamjenga Mtu – Mtu Hajengi Chama
Ni kweli isiyopingika kuwa mtu mmoja hawezi kulazimisha chama kubadilika kwa maslahi yake binafsi. Chama cha siasa kina misingi, itikadi, kanuni na maadili. Hata viongozi mashuhuri waliotokea ndani ya CHADEMA waliweza kung’ara kwa sababu chama kilitoa fursa, jukwaa na misingi ya kisiasa iliyowawezesha. Lakini wengi walipohama, waliishia kusahaulika au kupotea kabisa kwenye ramani ya siasa.

Mifano Hai ya Waliojiondoa CHADEMA na Kupotea

  1. Dkt. Wilbrod Slaa – Alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na mgombea urais aliyewapa matumaini makubwa Watanzania mwaka 2010. Alipohama chama hicho, alitoweka kwenye duru za siasa. Alipojaribu kurudi, nguvu ile ya mwanzo haikuwepo tena.
  2. Joshua Nassari – Kijana aliyeaminiwa na taifa. Alipohama, alitoweka kisiasa.
  3. Peter Lijualikali – Shujaa wa Bunge, sauti ya watu wa Kilombero. Alipotoka CHADEMA, akawa kimya.
  4. Vicent Mashinji – Katibu Mkuu wa chama. Heshima yake ilitokana na nafasi aliyokuwa nayo CHADEMA. Leo hii, jina lake halizungumzwi tena katika siasa za nchi.
  5. Peter Msigwa – Mmoja wa wapiganaji wa siku nyingi, lakini hata yeye nguvu yake ilianza kufifia alipoingia kwenye mivutano ya ndani.
  6. David Kafulila na Zitto Kabwe – Wana historia inayofanana. Walikuwa vijana wa matumaini waliokuzwa na vyama vya upinzani, lakini walipopoteza mwelekeo na kusahau asili yao, ushawishi wao ulianza kupungua.

Ujumbe kwa Vijana Walioko CHADEMA Leo
Msikubali mihemko ya muda mfupi kuharibu misingi yenu ya kisiasa. Siasa ni safari ndefu, yenye majaribu na mapito mengi. Hata katika familia kuna changamoto, lakini huwezi kuhama familia kwa sababu hukuridhika na maamuzi ya baba au mama. Badala ya kukimbia, kaeni ndani ya chama, pitieni mifumo rasmi ya kutoa maoni, pigeni kura kwenye vikao, jipeni muda – kwa sababu vyama havitengenezwi kwa msingi wa kuwaridhisha watu binafsi, bali kuhudumia jamii.

Hitimisho
Vijana mna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ndani ya CHADEMA na ndani ya taifa. Msiwe sehemu ya historia ya waliopotea kwa sababu ya tamaa ya haraka au kutokujua thamani ya jukwaa walilopewa. Jiulize, leo hii ungekuwa na jina na heshima hii bila CHADEMA? Kama jibu ni hapana, basi heshimu chama chako, kiandae kwa kizazi kingine, na jenge historia ya uaminifu, si ya kusaliti.
 
kijana ukiwa CDM unaonekana na kusikika

Ukienda CCM sasa

Anayeonakena na kusikika ni WASSIRA
 
Back
Top Bottom