Hivi Marais wa Afrika wakikutana makao makuu ya AU Addis Ababa huwa wanajadili umoja upi ikiwa nchi zimefungiana mipaka kwa visa vikwazo mipakani?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,107
49,809

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1717567065975054762?t=7EzYVKNQv0ied1s1baqUdQ&s=19
Kila Mwaka wanakusanyika kama watu wasiojielewa ambao huenda kupiga picha na kula starehe Kwa Kodi za Watu wao.

Nchi za Africa Zimefungiana Mipaka Kwa vikwazo vya visa,vikwazo Mipakani,mizozo isiyoisha na upuuzi mwingine kama huo ambao unazidi kudidimiza Watu wa Bara hili huko hao Viongozi mbumbumbu wakilaumu Wazungu.

Tafiti zinaonesha intra Africa trade ni just 15% (Aibu ya Karne) huku gharama za biashara na usafiri baina ya Nchi za Kiafrika ni kubwa Sana kuliko kufanya biashara na Nchi za Nje.

Unaambiwa kutoa mzigo Tanzania Hadi Lubumbashi hapo DRC ni bei kubwa kuliko kutoa mzigo Dar Hadi India.

Hivyo hivyo kusafiri na ndege kutoka Dar Hadi Lagos ni sawa na kutoka Nairobi hadi Marekani nk.

Nilimsikia Wode Maya anasikitoka jinsi alivyoshmbuka kupata visa ya Angola kutoka Ghana,urasimu na gharama zake ni kubwa sana mpaka akasema isingekuwa passion ya kazi yake angeacha.

Sasa hivi wamekuja na Azimio la Eneo huru la Biashara Afrika lakini utekelezwaji wake ni Kila Nchi ikijiskia.

Kiukweli inanisikitisha sana.Nazipongeza Baadhi ya Nchi ambazo zimeamua kufuta visa Kwa Waafrika kama Benin,Gambia, Seychelles,Ghana na Kenya na zingine ambazo Zimepiga hatua.Tujifunze Kwa hao je wamepata hasara Kwa kufuta visa?

View: https://twitter.com/TheCitizenTz/status/1719282631789998444?t=bXZS4-j_O0ZMqow9JlXviA&s=19

Nchi kama Tanzania na ujamaa wake ni shida tupu,ukianza kufuatilia visa ni kama vile unafuatilia kesi,hovyo kabisa imegeuzwa chanzo Cha mapato badala ya Huduma.

Maswali
1.Sababu zinazozuia Nchi za Afrika kuwa na Umoja wa mdomoni badala ya ushirikiano wa ukweli ni nini hasa?

2.Mbona ripoti zinaonesha wazi kwamba biashara baina ya Nchi za Kiafrika Iko chini mno na expensive yet Marais wa Afrika hakuna Juhudi za maana wanafanya wakati wanajua kwamba intra Africa trade inakuza uchumi kuliko biashara na Wazungu ambayo inasomba Mali kutoka Afrika?

3.Kwani hawajui kwamba matatizo ya kiusalama yanasababishwa na umaskini ulioletwa sababu ya kutokuwa na free movements of goods and people? Kujifungia ndani bila kujifunza na Kushirikiana na mwingine utawezaje kutatua shida zako?

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1720253510896308558?t=ps7Eq-zZ5JfRg4jHFkTFjw&s=19
 
Wakati umefika Waafrika gubadilike kifikra na kimtizamo,kuendelea na kufungiana mipaka inamnufaisha mkoloni kuliko sisi.

Njia ya haraka ya kuondoa umaskini ni ku trade wenyewe Kwa wenyewe,kujenga miundombinu ya kutuunganisha Kwa pamoja na soko kubwa la pamoja.

Mfano Tzn tunahangaika kuimalisha Bandari na barabara yet ikifika mpakani mwa Zambia tabu Iko pale pale hakuna ukichofanya.

South Leo imeingia kwenye crisis ya umeme ila tungekuwa na grid connectivity ilikuwa ni swala la kununua Umeme kutoka Ethiopia wakati inajipanga bila kuathiri biashara na maisha ya watu,likewise Kwa Tanzania.
 
Hongera Rwanda Kwa kufuta visa Kwa Waafrika
Screenshot_20231103-064703.jpg
 
Back
Top Bottom