Kwa umakini huu CHADEMA itafika mbali sana

Kwa umakini huu CHADEMA itafika mbali sana

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
CHADEMA wanafahamika kwa mipango madhubuti na makini. Viongozi wa JUU KABISA ndani ya chama wana sifa ya usiri na umoja. Mara nyingi pale wanapotoka hadharani kuiweka mipango yao huonekana kama maamuzi ya ghafla.

Lakini huwa na mafanikio makubwa kama yalivyopangwa kutokea na hutokea kama walivyopanga yatokee. Kiufupi hakuna ughafla. Kwa wapinzani wao mafanikio haya huleta madhara makubwa sana na huwafika ghafla bila kutarajia.

Hata ndumila kuwili ndani ya CHADEMA hupigwa na bumbuwazi jinsi mipango hii inavyofikia hatua za kutekelezwa bila wao kushiriki au kufahamu uwepo wa michakato yake. Moja ya bao la karne na mfano mzuri wa mikakati hii ni uteuzi wa Dr. Slaa kuwania Uraisi wa mwaka 2010.

Jina lilifahamika siku iliyopangwa lifahamike hadharani na kuwaacha waasi wa ndani na wapinzani wa chama midomo wazi! Yaliyofuata ni historia ambayo wewe msomaji pia unaijua.


Kwa anayefanya tafakari vizuri atagundua kuwa wapinzani wa CHADEMA wanafamu fika kwamba hiki chama hakiwezi kumlengesha mapema mgombea wao ajaye au kuruhusu kwa namna yeyote ile akae pahala atakapolengwa na mashambulizi ya mara kwa mara kirahisi.

Na yeyote anayeonekana kwa sasa wamemtengeneza tu ili wapinzani wa CHADEMA wapoteze risasi kwa kulenga wrong target. Watajichosha na kupoteza rasilimali zao wakidhani wanamdhoofisha mgombea ajaye kumbe wasijue wanajichosha wao wenyewe! Hii ni sababu ya kwanza.


Sababu ya pili, ni kanuni ya kawaida kwamba ukitaka kulitawanya kwa urahisi kundi ambalo uimara wake na umoja wake unachangiwa kwa kiasi kikubwa na umahiri wa uongozi wa mchungaji wake, basi piga mchungaji wao na wengine wote watatawanyika! CHADEMA inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama.

Hakuna dalili zilizowazi zinazoonesha taswira ya safu ya Uongozi ujao. Katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika ndani ya CHADEMA kwenye ngazi yoyote ya juu zinadhihirisha kuwa ni vigumu kupenyeza mamluki au kuwavuruga kwa kutumia mamluki.

Hii ni historia njema na inaweza kutumika kutuaminisha kuwa hata zamu hii watavuka salama. Kwa hiyo nafasi pekee kwa wapinzani wa CHADEMA kuleta mtikisiko ni kumuondoa Mchungaji wa kundi kabla ya muda wa ratiba ya kuondoka kwake.


Siamini kama kweli Freeman Mbowe amekuwa Mlengwa No. 1 wa dola ya CCM kwa pigo moja la ghafla na la bahati mbaya. Jipe muda kidogo kutafakari utaona jinsi pigo lilivyokuwa limepangwa kitambo na lilivyotakiwa kuwa moja tu lenye kufikia malengo makubwa kwa mkupuo bila kutikisa sana wala kuhamasisha hasira ya umma. Dondoo hizi zikusaidie:

Bomu maalumu na la teknolojia mpya kabisa kutoka kiwandani-China likaingia nchini na kulipuliwa ulinganishe na nguvu/jitihada inayowekwa na yombo vya usalama kujua liliingiaje nchini

Walenga shabaha (snipers) waliotayari kumalizia kazi iwapo bomu halikuleta madhara yaliyopangwa

Wapiga risasi wenye bunduki za kivita na zenye risasi za kutosha kuhakikisha blusters wanaondoka salama kwenye eneo la tukio
Mawasiliano kutokuwepo katika eneo la tukio nusu saa kabla na nusu saa baada ya tukio

Bado tunasubiri ushahidi wa video toka kwenye DVR hapo ndipo wabaya wote watafyata midomo kama ilivyokuwa kwa Daudi Mwangosi ambaye tulishaanza kuaminishwa kuwa alipigwa na kitu kizito toka kwa waandamanaji akikimbilia kwa polisi kumbe kitu kizito kilitoka kwa polisi wenyewe.

Halafu wengine wanasema eti walijilipua wenyewe kutafuta huruma ya wananchi kweli!? Tusemeje sasa na hayo ndio matokeo ya akili ndogo kuongoza akili kubwa.!
 
I wonder how much CHADEMA has paid you to come up with this analysis.
 
PISTO LERO,

Ili kuwaepushia watu vifungo (ban) humu ndani ambavyo vinaweza kutokea kwa kuhamasishwa kuvunja sheria ya "Name Calling" au kwa sababu za Kitaaluma kujilinda na mashambulizi dhidi ya Plagiarism ni vema ungemtambua (acknowledge) Mwandishi wa makala uliyoihamisha kutoka Jukwaa la Great Thinkers na kuileta Jukwaa la Siasa.

Makala halisi na Mwandishi wake inapatikana hapa: Kwanini Freeman Mbowe ghafla amekuwa mlengwa No. 1 wa Dola/CCM?
 
I wonder how much Chadema has paid you to come up with this analysis.

Kila mtu anahogwa sio....hivi kwa nini vijana wa ccm manaonaga sisi vijana wengine wa upinzani ni tuna njaa sana?...kwa vile wakati mwingine hatujuani tu...wengine tunafanya kazi zetu na kulipa kodi bana ...vipi nyinyi..?!!!
 
Hii haihitaji wewe kuandika ndio wananchi waelewe. Una-force credit ambayo haipo. Wewe utakuwa mpuuzi. Acha ujinga fanya kazi na ongea freemind, usishabikie mikate ya watu. Ooohoo!!
 
Hii haihitaji wewe kuandika ndio wananchi waelewe. Una-force credit ambayo haipo. Wewe utakuwa mpuuzi. Acha ujinga fanya kazi na ongea freemind, usishabikie mikate ya watu. Ooohoo!!
asante mpuuzi mwenzangu kwa kuchangia topic ya kipuuzi ungekuwa unatumia akili wala usinge changia kwa maana ni ya kupuuzi.
 
Hii haihitaji wewe kuandika ndio wananchi waelewe. Una-force credit ambayo haipo. Wewe utakuwa mpuuzi. Acha ujinga fanya kazi na ongea freemind, usishabikie mikate ya watu. Ooohoo!!

Vip povu lote hili la FOMA au OMO....
T2015CDM inakaribia kusajiliwa.
 
Kila mtu anahogwa sio....hivi kwa nini vijana wa ccm manaonaga sisi vijana wengine wa upinzani ni tuna njaa sana?...kwa vile wakati mwingine hatujuani tu...wengine tunafanya kazi zetu na kulipa kodi bana ...vipi nyinyi..?!!!

Ukizisoma kwa makini post za hawa Buku7 utagundua kuwa ni watu ambao upeo wao uko chini sana na sio wa kuweza kupewa nafasi ya ajira popote zaidi ya pale Lumumba ambapo ajira inaangaliwa surname yako ni nani. Sasa wao wanafikiri kila mwenye kutetea mabadiliko ni mchovu,hawajui kuwa hao wanaowabeza wengine ni senior officers katika serikali hii hii na ndio ambao kila upuuzi wanaopanga wanaufikisha kwa wapinzani kiasi kwamba hakuna siri inayofichika siku hizi.
 
I wonder how much CHADEMA has paid you to come up with this analysis.
If u would have brain, u would have wondered why people should be paid in voluntary manners!
Many of CHADEMA supporters are working for the party out of pay!
They are proud of that bcz tym cant be paid....
Working at pay is for MAGAMBAZ like u!?
Nheee!
How much my dear?
 
Ukizisoma kwa makini post za hawa Buku7 utagundua kuwa ni watu ambao upeo wao uko chini sana na sio wa kuweza kupewa nafasi ya ajira popote zaidi ya pale Lumumba ambapo ajira inaangaliwa surname yako ni nani. .

Ndugu CHAKAZA, mbona unawasingizia wenzio bwana!
Si kwamba wana upeo mdogo aiseee...
Ni kwamba hawana kabisa...
Sample toka kwa mzee wa PIGA TU ambaye anasemekana ni MWANASHERIA!
 
I wonder when r u gon start using ur mind to think...amka Dada..nyakati za ukombozi ndo hizi...nitajie jambo moja tu ambalo u r proud of ur government..tell me..what???

NOTHING but....
On her behalf!

 
Kila mtu anahogwa sio....hivi kwa nini vijana wa ccm manaonaga sisi vijana wengine wa upinzani ni tuna njaa sana?...kwa vile wakati mwingine hatujuani tu...wengine tunafanya kazi zetu na kulipa kodi bana ...vipi nyinyi..?!!!
Nheee DR. MO
Nimepata habari kwamba vijana wengi wahitimu wa vyuo vikuu waliojiunga CCM akiwemo SHONZA na MWAMPAMBA, waliahidiwa kufutiwa deni la BODI ya MIKOPO YA ELIMU YA JUU na ikishindikana kufutika watalipiwa!
Kwa hiyo wengi hawaajiriwi na hawaajiriki...
Ukitaka kujua kwa nini, angalia reply na post zao...
GENTLEMEN DEGREES...!
 
Back
Top Bottom