Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.

TwendeSasa

Senior Member
Joined
May 24, 2008
Posts
128
Reaction score
116
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila
 
Kusema 'kwa ukali' ni kujaribu kufanya unnecessary amplification ya jambo ambalo hata halipo, labda kutaka kuharibu mjadala tu.

Ni vigumu kuelewa kwa nini wanatumia hata uongo kuhalalisha hoja zao au matendo yao dhidi ya CHADEMA. Ni kitu kinachoshangaza sana.

But it tells a lot.
 
Dr.wa CCM huyu hana tofauti na fastjet!c ni kama wale wanafunzi wa kile chuo flan waliokuwa wanapewa degree kwa sbb tu ni wanamagamba
 
Kitila anachokisema hajui tofauti yake na wengine nini.

1. Kuweka usiri ktk jambo ambalo labda ni la kujenga. Kuyafanyia mambo gizani.

2. Mambo yapo gizani yanashirikisha wale wasio wapendea mema huku ukijua hawawapendei mema. Kuvunja utaratibu kwa makusudi. Mfano, leo uende tume ya uchaguzi na kutaka kugombea urais japo ni haki kugombea watakushangaa kutaka kufanya kilicho halali yako kwa utaratibu wako.

34. Katika utaratibu wako kukosoa ambacho ungekosoa ktk utaratibu wa wote. Watu wanajiuliza huenda una agenda wasiyoijua na huenda ukawa umetumwa. Inawezekana huna tatizo ni dharau tu kwa kuwa umesoma wenzako hawakusoma hivyo wafuate yako na si ya wengine. Suala la kusoma mnaliweka ktk picha.

Naamini wasomi si wazuri wa mabadiliko. Wasomi huwa wapo mawinguni wakati wa wengi wapo ardhini na wanataka mambo yaende ki-ardhi ardhi. Kitilya aende kuanzisha chama atakacho awaache Chadema na mapungufu yao.
 
Kitila Mkukumbo amechanganyikiwa na hoja zake, Kama ni mzalendo angeonyesha uzalendo ndani ya chama kuliko kuanza usaliti wa kukihujumu chama, hapo inadhihirisha jinsi ambavyo anatumikia waliomtuma
 
Maneno sawa kabisa kutoka kwa dr Mkumbo.
Ngurumo anamtumikia kafiri ili apate mradi wake wakati Mkumbo yuko huru, hafungwi na minyororo ya itikadi kwa sasa!.
Hivi ngrumo haoni jinsi Wabunge wa CHADEMA kama kina Lema wanavyotumia nguvu kuhalalisha posho za kijinga.
Hivi Ngurumo haoni jinsi wabunge wa CHADEMA wanavyobehave kama wabunge wa CCM pindi linapokuja suala la mijihela?
 
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.

Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.

Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.
 
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.

Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.

Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.
Acha unafki wewe
 
kitila na mwenzako ombeni mdahalo cc ndo 2toe hoja nyie mjibu coz najua hata ngurumo anaweza akaandika mengi juu ya kitila.
 
JF hii hii itakuja kuhukumu maana kila andiko litabaki hapa.

Sawa, Chadema ina mapungufu tena makubwa tu na si ya juzi, lakini kwanini kasi ya makala, kukosoa kumepamba moto sasa? Hivi leo Kitila anataka kutuambia alipokuwa anakosoa tulikuwa hatujui? Kwanini haya maneno makali makali wanazidi kuyakuza kipindi hiki?

Hivi huyu Kitila kama angekuwa anakosoa kwa kasi hii hii kabla hajafukuzwa si angejenga heshima kama mtu mwenye misimamo? Zitto aliposimama sasa ndipo alipo siku zote na tunamfahamu kwa hilo na hawezi kutushtua kwa kauli na matendo yake sasa, hata Kitila atafute justification za kiwango gani bado anazidi kutufanya tuzidi kumuweka kwenye kundi lile lile ..........

Kitila umeharibu, umekubali umeharibu, tulia tafakari hatma yako ya kisiasa ujijenge kwa namna mpya na si hii inayoonesha umejaa hasira tu za kufukuzwa na si hasira za kutaka mabadiliko.

Sorry brother....
 
Ni upuuzi kuhubiri demokrasia majukwaani halaf mnashindwa kuitekeleza ndan ya chama.Dk Kitila yupo sahihi acheni ulimbuken kwa kutetea ujinga ndan ya chama.
 
Ni upuuzi kuhubiri demokrasia majukwaani halaf mnashindwa kuitekeleza ndan ya chama.Dk Kitila yupo sahihi acheni ulimbuken kwa kutetea ujinga ndan ya chama.

Mkuu, kosa la Mkumbo ni ujinga na upuuzi wa kutengeneza waraka nje ya vikao na taratibu za chama. Kama unaona hiyo ni sahihi basi wachukue wakusaidie kwenye kujenga demokrasia kwenu
 
Bado Dakatri hujatujibu kwa ufasaha sisi wenye akili za kawaida, sijaelewa hivi HAKI hutafutwa gizani, hivi demokrasia inatafutwa gizani? yaani nje ya mfumo unaoelewaka wa kitaasisi- hivi ni kweli daktari unataka kutuaminisha kwamba kwamba utaratibu huo uliotumia kwa kuandika waraka wa SIRI ni sahihi na ULIKOSA kabisa njia nyingine ya kupenyeza mawazo yako ndani ya chama chako tena ukizingatia wewe ulikuwa mshauri wa chama kwenye haya haya mambo ya siasa, hii fursa iligoma kabisa, kabisa, kabisa hadi kuamua kujiunga na hao wengine kuratibu WARAKA huo kwenye giza totoro?

Hivi ni nini maudhui ya kitu kuandaliwa GIZANI, naamini hata kama ni kitu kizuri lakini watu lazima wakitilie shaka!! ni sawa na baba mwenye nyumba kukutwa anadokoa mboga kwenye chungu jikoni then ukasema hilo ni jambo la kawaida sababu mboga yenyewe kanunua yeye. hapa lazima kutakuwa na tatizo tena kubwa mno kati ya baba mwenye nyumba au familia yake kwa ujumla.

Sitaki kukuchocha najua wewe ni mwerevu sana, HOJA kuu kwa sisi watanzania wa elimu ya kawaida tunataka kujua ni kwa nini daktari ukaamua kufanya mambo GIZANI wakati ulikuwa na fursa ya kuyafanya hayo kwenye NURU? tena ukuwa na fursa tele ndani ya chama?
 
Kwa hakika maneno ya kitila ni ukweli kama hoja ya kukataa posho ilikuwa ni ya chama iweje mpaka mwenyekiti asiifuate na kwa maana hiyo walikuwa wanamtafuta zitto kwa kipindi kirefu.tuache siasa za upepo tuangalie maslahi yetu na vizazi vyetu."nikiambiwa nichague kati ya tanzania na chadema tanzania kwanza chadema pili.zzk
 
Hivi huyu Kitila Mkumbo ni Dr wa binaadamu, mifugo au falsafa? Hoja kuu ya ngurumo ni kwamba Hakuna records zinazoonyesha aliwahi kuwakosoa viongozi wa chama wala chama katika vikao stahiki ndani ya chama, yeye anakuja na hoja ya kuandika kwenye magazeti.

Ngurumo anasema kwa nini Kitila hakutumia fursa ya kutakiwa kujieleza kwenye kamati kuu kuelezea udhaifu na Ufisadi waliouandika kwenye waraka wao wa kishenzi kama kweli alikuwa na nia njema na chama chake, Alishindwa, ikiwa na maana kwamba ni muoga , muongo, mzandiki,pandikizi,mnafiki na msaliti.


swala la kuandika kwenye magazeti hata sisi tunaandika hapa JF.

DR Gani huyu Jamani, Hawezi kuelewa hata analalamikiwa kivipi, nadhani Ngurumo alikosea kutambua usomi wake.
 
Hivi wanajamvi, naomba tu kuuliza.

Mbona karibia watu woote wenye nafasi/vyeo na wasomi kutoka maeneo ya Singida wana MIDOMO sana? Mfano tu kwa uchache Nape, Mwigulu, Chiligati, Dr.Mkumbo etc

Hata niliosoma nao wako hivyo hivyo!!!

Tatizo liko wapi?????
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom