Mkuu
barafu,
Mbona unafanya kama hii habari ni ngeni kwako? Hivyo vipimo tulivijadili sana wakati ule na kuhitimisha kwamba kinachojengwa Chato ni International Airport!!! Kwa kuzingatia runway yake; kama ulivyosema haujaachana sana na JK Nyerere International Airport! Tukajaribu kuhalalisha kwamba, okay, fine... je, hakutakuwa na economic impact kwa huo uwanja... watetezi wa kila kitu wakadai utachochea utalii... nikaombe nitajiwe vivutio vya kitalii vilivyopo Chato! Hadi mjadala ule unafungwa; sikutajiwa hata kimoja !
Tukajaribu kumwangalia Mkapa ambae haku-opt kujenga uwanja wa Masasi... tukafanya comparison ya umbali kati ya Mtwara to Masasi na Chato to Geita! Tukakuta umbali wa Mtwara to Masasi ni karibu mara mbili ya umbali wa Geita to Chato! Hapa tukahoji, ikiwa Mkapa aliweza kutumia uwanja ulio karibu mara mbili zaidi hadi kwao compared to JPM, nini Mheshimiwa kinamfanya ashindwe!
Itoshe tu kusema kwamba, huwezi hata kidogo kulinganisha Heliport na Uwanja wa ndege!!! Kwa Rais kuwa na Heliport, hasa ukizingatia direction ya nyumbani kwa JK; kwa hakika angalau inasameheka! Kwamba, ili asiwe anatengeneza disaster barabarani kwa sababu tu anakwenda kwake; basi ni heri atumie chopper! Na kama atumie chopper, chopper ya Rais haiwezi kutua popote as if ni chopper ya askari!
Aidha, huwezi pia kulinganisha daraja la Mkapa na Uwanja wa ndege! Daraja la Mkapa linamsaidia hata mshona viatu na mpasua matumbo ya samaki pale Ferry... lakini sio Uwanja wa Ndege! Daraja la Mkapa ni daraja la wananchi... daraja ambalo lingeweza kujengwa na Rais yeyote hata kama si wa Kusini... kama JK na Malagalasy yake! Huwezi hata chembe kulinganisha bandari (ya Bagamoyo) na EPZ huko Bagamoyo na uwanja wa ndege, kwa sababu; hivyo ni vitega uchumi vitakavyomnufaisha kila mmoja!! Kama ambavyo huwezi kuthubutu kusema Bandari ya Dar es salaam imejaa Wazaramo na Wandengereko! Kinyume chake, Uwanja wa Chato zaidi ya kumnufaisha Mheshimiwa na team yake hakuna kingine cha ziada!
Nachelea kusema kwamba, ulevi wa aina hii wenzake huwa wanaufanya wakiwa wameshakaa sana madarakani kiasi cha kujisahau na kudhani wanaongoza kampuni zao binafsi! Kinyume chake jambo kama hilo linapokuja kutokea within 1 years of administration; inatosha kabisa kuwa RED FLAG ya kuwafanya watu wahoji... "what next?" BoT; UChato (cf UDOM), Central Railway Station (Western Zone), Zonal Investment Center... anyway, karibu tumalizie ujana!!!