Kwa ujenzi huu wa Uwanja wa ndege Chato, Rais Magufuli anatukatisha tamaa "watu wake"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Mwanzoni niliposikia ujenzi wa Uwanja wa ndege Chato, basi nilidhani wameamua kumtengenezea mzee walau "Airstrip" tu ili iwe rahisi kwake kufika mpaka kijijini kwake kwa njia ya anga, kuepusha safari ndefu ya Dsm-Chato au Mwanza-Chato. Na kwa sasa uwanja huo unaendelea kujengwa kwa kasi kubwa.

Lakini kumbe si "Airstrip" tena,bali ni "Airport",maana huwezi kuwa na Airstrip yenye runway 3000M(urefu) na 45M (Upana)... huu ni uwanja kabisa,na ndio maana hata tangazo la Tender limesema "New Airport"....So this is another coming Airport in lake Zone.

IMG_2072.JPG


Soma pia > Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato: Serikali yatangaza tenda

Kuwa na Runway ya urefu wa mita 3,000 si kitoto, maanake hii ni eneo la mruko lenye urefu wa km 3 na upana wa mita 45.....Waoooooh!!! Another "International Airport" to come.

Uwanja wa ndege wa Dsm una runway mbili moja kubwa nafikiri ni km 3 (3,000M) kwa urefu plus mita kadhaa za threshold na upana ni mita 46, wakati ile ya hapo Dsm ndogo inayotumika mchana tu na kwa ndege ndogo ni km 1 (1000M) urefu na upana wa mita 30...

Sasa utaona Runway ya Chato kwa urefu inalingana na hii ya uwanja wa Dar na upana wa Dsm umezidi kwa mita moja ule wa Chato.

Hapo inapaswa tujuwe "Pavement Identification number", tufahamu "strength of runway" ya Chato itakuwa na uwezo wa kuchukuwa ndege za uzito gani, lakini kwa urefu huu tu,maanake sasa Chato inaenda kupokea ndege zenye ukubwa wa Boeing 738, B733, B737 na Airbus 320 na A319 ambazo toka Uhuru hazijawahi kutuwa Iringa, Songea, Kigoma, Tabora, Musoma na Tanga; ambayo ndio miji mikubwa ktk nchi yetu

Niliwahi kutuwa kwenye Uwanja wa Geita pale Mchauru(?), huu una hata Location Indicator ya ICAO na unafahamika kama HTRU,hawa wana hata "Control Tower", kutoka Geita pale Mgodini hadi Chato ni kama km 100 na ushee. Sijajuwa kwanini wanapeleka uwanja mkubwa hivi Chato, sidhani baada ya mkuu JPM kutoka madarakani uwanja huu utatumika kibiashara.

Hili lilitokea kwa Mizengo Pinda,alijenga Mpanda uwanja mzuri sana na wenye Tarmac nzuri sana...Lkn baada ya kutoka yeye umebaki malisho ya ng'ombe na mbuzi wa Mpanda.Na kwa sasa una hadhi ya "Airstrip" sababu hauna hata Control Tower, hakuna ndege za kibiashara zinazokwenda huko. Kampuni ya Auric Air ilikuwa na safari zake Mpanda,lakini sasa wamesitisha karibu mwaka na ushee. Ulijengwa kwa bilions of money.This was one of the "White Elephant" projects of our time.

Ukiutazama uwanja ule wa Mpanda, unajisemea tu kuwa viwanja hivi vingekuwa vinabebeka, basi ule kwa uzuri wa Runway yake na Apron, na aina ile ya lami, basi tungeubeba na kuupeleka eneo lenye movements nyingi ya ndege za kibiashara na kuutoa kule palipodorora.

Bagamoyo alitengeneza "HELIPORT" na akawa anaitumia kila mwisho wa week akienda nyumbani kupumzika, aliitengeneza pale Msoga kijijini kwake. Naona kila mtu anatazama nyumbani kila akipata madaraka. Wanasema "Charity begins at home".... Mkapa aliwapa Daraja, JK kawapelekea EPZ,bandari na heliport. Pinda aliwapelekea uwanja wa ndege ambao hautumiki. Kwa hiyo si ajabu kwa JPM kupeleka uwanja nyumbani.

Kabla ya JK kulikuwa hakuna "HELIPORT" Msoga....Lkn yeye amepeleka na hata siku anaaga Ikulu,alipelekwa Kijijini Msoga na chopa ya kukodishwa ya kampuni ya Everrest ya Kenya inayofanya kazi Tanzania.Mtu kwao, mkataa kwao mtumwa...

Naogopa pia uwanja wa Chato usijekuwa malisho ya mbuzi, ingetosha huko Mkuu tungemtengenezea tu HELIPORT ili awe anapelekwa na Chopa,maana jeshi letu lina chopa mpya, Uwanja unajengwa CHATO unakuwa na Runway (3,000m to 45m).... Hii sawa na KIA na Julius Nyerere International Airport. Huku ni kujipendekeza au nini?

Ni ukweli Rais anahitaji usafiri wa anga aendapo likizo au mapumziko nyumbani, lkn si kwa kujenga Airport Chato. Hivi kweli Chato unajenga Runway yenye "Bitumen Standards".

Kuna viwanja tunapaswa kuviboresha maana vina movements nyingi za ndege, Uwanja kama Songea umechakaa na kila siku kuna ndege moja ya abiria inakwenda, Uwanja wa Iringa huu ni km2.1 na una movements karibu mbili kwa siku, uwanja wa Kigoma ambao hata ndege za wakimbizi na UN hutuwa,japo wao kwa kusaidiana na UNHCR wamejenga uwanja Kasuru.

Safari ya kwanza ya Mandela kuja Tanzania kuonana na Mwalimu alitua uwanja wa ndege wa Mbeya. Mbeya ilikuwa katika Ramani kubwa kwa ajili ya kusaidia harakati za Kusini mwa Afrika na ilitumika pia wakati wa vita ya kwanza na ya pili ya dunia. Siku CEO wa Air Zimbabwe anazindua route mpya ya -Harare-Dsm-Harare, alisikika akisema kwa mara ya kwanza Air Zimbabwe kuja Tanganyika ilikuwa mwaka 1946(Wakati huo wa Southern Rhodesia), viwanja ilivyokuwa inatuwa ni Mbeya na Tabora.

Hivyo uwanja kama wa Mbeya(Songwe) ndege hazitui usiku eti hauna taa za sehemu ya kutua na kurukia ndege, uwanja huo ulitakiwa kujengwa miaka mingi,ulitakiwa kutumika kama "Refueling Point" kwa ndege zinazosafiri toka Kaskazini kwenda Kusini mwa Afrika/dunia au kinyume chake. Siasa za Tanzania na vipaumbele vinavyobadilikabadilika ndio vikatufikisha hapa.

Hii ya Airport ya Chato, inaweza kuwa na "watetezi" wake, lakini haiondoi haki ya wengine kuhoji umuhimu wa kiwanja kikubwa kiasi hiki kwenye eneo ambalo baada ya mtu kutoka madarakani,haiwezi kuwa na "umuhimu" wa matumizi kama ilivyo sasa. Hii inawapa "wakosoaji" wakati mzuri na "watetezi" wa Rais wakati mgumu. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Kuhoji kwetu, si hujuma na shutuma kwa aliye na mamlaka, bali ni tabia ya binadamu kuuliza kile anachoona kinampa utata.
 

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
4,078
2,000
Hivi kuna watakaokataa nikisema huyu JPM ni mbinafsi/mroho wa madaraka asiyejali utaifa?

Haya yalitegemewa hasa baada ya kuchepusha barabara iliyokuwa ipite biharamulo ili ipite chato!?? miaka hiyo ya uwaziri!! Kwa waliopita njia hiyo tafuteni kwenye GPS njia ipo biharamulo. Nani ambaye hajaona mataa ya barabarani ambayo hayatumiki chato?? Zile tuhuma za kuwapa ndugu na michepuko nyumba za serikali?

Huu ni UFISADI mbaya wa aina yake watz mmembumbaa tu!!
Sasa amekuwa Rais Chato itakuwa na international airport na ikibidi bandari hata kama hakuna bahari.

Tutaendelea kusikiliza maneno ya juu kwa mtu anayepambana kulipiza kisasi na kuzimisha hoja mbadala!! Zinduka!!!!!!!!!!!!!!
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,540
2,000
Ndio maana nguvu nyingi inatumika kuminya uhuru wa habari ili watu wasihoji.

Watumishi maslahi yao yamewekwa kushoto, wanafunzi wanakosa mikopo,vijana hawana ajira alafu unasikia Airpot inajengwa Chato na bado unasikia kuna watu wanataka waombewe!Kwa lipi?Never ever!

Alafu utasikia wengine wanaambiwa wanatumia hela vibaya!Hapa sijui tofauti iko wapi!!

Kiongozi aliekuwa na uchungu na watanzania nchu hii alikuwa ni Nyerere tu aliestaafu bila kuwa tajiri wala kupendelea alikozaliwa licha ya kukaa Ikuku kwa miaka 23.

Mwenyezi Mungu mrehemu huyu mzee maana kweli alikuwa kiongozi mzalendo ambae amekosa wa kumrithi kwa vitendo mpaka sasa
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
10,610
2,000
Bad, bad ever ...!,kwa nini asingeuimarisha UWANJA wa mwanza kwa 100%, au kabisa kuufanya wa kimataifa... ukahudumia na Serengeti.../ madege makubwa ya kitalii yakaweza kutua mwanza.

Kwa akili zangu ndogo sana atakapomaliza mda wake na
ndio utakuwa mwisho wa uhai UWANJA huo.

HIVI HAKUNA WASHAURI WA MAMBO YA AINA HII ILI KUTUOKOA NA HASARA ZISIZO ZA LAZIMA?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom