Kwa ujenzi huu wa Uwanja wa ndege Chato, Rais Magufuli anatukatisha tamaa "watu wake"

Mkuu barafu,

Mbona unafanya kama hii habari ni ngeni kwako? Hivyo vipimo tulivijadili sana wakati ule na kuhitimisha kwamba kinachojengwa Chato ni International Airport!!! Kwa kuzingatia runway yake; kama ulivyosema haujaachana sana na JK Nyerere International Airport! Tukajaribu kuhalalisha kwamba, okay, fine... je, hakutakuwa na economic impact kwa huo uwanja... watetezi wa kila kitu wakadai utachochea utalii... nikaombe nitajiwe vivutio vya kitalii vilivyopo Chato! Hadi mjadala ule unafungwa; sikutajiwa hata kimoja!!

Tukajaribu kumwangalia Mkapa ambae haku-opt kujenga uwanja wa Masasi... tukafanya comparison ya umbali kati ya Mtwara to Masasi na Chato to Geita! Tukakuta umbali wa Mtwara to Masasi ni karibu mara mbili ya umbali wa Geita to Chato! Hapa tukahoji, ikiwa Mkapa aliweza kutumia uwanja ulio karibu mara mbili zaidi hadi kwao compared to JPM, nini Mheshimiwa kinamfanya ashindwe!

Hatukupata jibu na hadi kesho sina jibu... angalau kwa jibu la kuweka mbele ya kadamnasi! Si dhambi kuepusha bawa katika ulimwengu wa Cybercrime Act...

Itoshe tu kusema kwamba, huwezi hata kidogo kulinganisha Heliport na Uwanja wa ndege!!! Kwa Rais kuwa na Heliport, hasa ukizingatia direction ya nyumbani kwa JK; kwa hakika angalau inasameheka! Kwamba, ili asiwe anatengeneza disaster barabarani kwa sababu tu anakwenda kwake; basi ni heri atumie chopper! Na kama atumie chopper, chopper ya Rais haiwezi kutua popote as if ni chopper ya askari... heliport hapo inahusu!

Aidha, huwezi pia kulinganisha daraja la Mkapa na Uwanja wa ndege! Daraja la Mkapa linamsaidia hata mshona viatu na mpasua matumbo ya samaki pale Ferry... lakini sio Uwanja wa Ndege!

Daraja la Mkapa ni daraja la wananchi... daraja ambalo lingeweza kujengwa na Rais yeyote hata kama si wa Kusini... kama JK na Malagarasi yake!

Huwezi hata chembe kulinganisha bandari (ya Bagamoyo) na EPZ huko Bagamoyo na uwanja wa ndege, kwa sababu; hivyo ni vitega uchumi vitakavyomnufaisha kila mmoja!! Kama ambavyo huwezi kuthubutu kusema Bandari ya Dar es salaam ipo kwa ajili ya Wazaramo na Wandengereko!

Kinyume chake, Uwanja wa Chato zaidi ya kumnufaisha Mheshimiwa na team yake hakuna kingine cha ziada!

Nachelea kusema kwamba, ulevi wa aina hii wenzake huwa wanaufanya wakiwa wameshakaa sana madarakani kiasi cha kujisahau na kudhani wanaongoza kampuni zao binafsi! Lakini jambo kama hilo linapokuja kutokea within 1 year of administration; inatosha kabisa kuwa RED FLAG ya kuwafanya watu wahoji... "what next?" BoT; UChato (cf UDOM), Central Railway Station (Western Zone), Zonal Investment Center, kuwa mkoa... anyway, karibu tumalizie ujana!!!
 
Mpango wa ujenzi wa uwanja haukuanza kipindi cha urais wa JPM....mkoa mpya wa Geita upo ukanda wa mkuu wa madini ya dhahabu...unastahili kuwa na uwanja wa ndege
LUSOMYA
Inaonekana hujaelewa kitu hapa.
Kwanini Uwanja ujengwe kijijini Chato na sio Geita mjini? Chato kuna ni nini?
Kuna haja gani kuwa na uwanja mkubwa, wakisasa na wa gharama hivyo katika kijiji cha Chato?
Upi uhusiano wa Dhahabu na uwanja mkubwa wa ndege?

Mererani kuna Tanzanite, Mwadui kuna Almasi, Nzega kuna Dhahabu, Bulyakuru kuna Dhahabu, Singida Vijijini kuna dhahabu nk. Kote huko hakuna viwanja vya ndege vilivyojengwa na Serikali.
 
Kwani chato sio Tanzania?
Kuhusu chato kung'olewa kagera ni kwa sababu ya kuanzisha mikoa ya Geita na Simiyu ili kupeleka huduma karibu zaidi kea wananchi,wilaya nyingi zilimegwa na nyingine mpya kuanzishwa.Magufuli alikuwa hajawa Rais,wala hakuwa Tamisemi
Ndio hakuwa mfalume lakin alikuwa na alikuanainfuluence ya kufanya hivyo.
 
Mpango wa ujenzi wa uwanja haukuanza kipindi cha urais wa JPM....mkoa mpya wa Geita upo ukanda wa mkuu wa madini ya dhahabu...unastahili kuwa na uwanja wa ndege
Kwanini uwanja usijengwe Geita? Unajua umbali wa kutoka Geita to chato?
Kama lengo kusaidia wafanyabiashara angejenga Buselesele/Katoro maana hapo Ndio kuna wafanyabiashara, chato mji wenye gari zisizofika 60 kuna traffic light? Halafu kuhoji marufuku,

Kwahili endeleeni tu kumuombea mimi nilishajitoa kwenye maombi
 
Mkuu chige heshima kwako
Nimefurahia sana mchango wako...Umeelezea ya JK na Chinga kwa uzuri sana.Nimeelewa vizuri.Hii ndio raha ya mjadala,na hasa kwenye jukwaa kama hili....Umenielimisha vya kutosha.ASANTE.

Nimeufufua mjadala ili kuufungia mwaka...nia haikuwa nyingine,bali kumaliza mwaka kwa mjadala huu.Lkn zaidi,juzi nilikuwa maeneo ya Geita na Chato...Nimeona jinsi uwanja huo ukijengwa kwa kasi ya ajabu.Hapo neio nikaona,kweli jambo hili ni "serious" kabisa.

Asante kwa hoja zako zilizoshiba.
 
Hata wa picha
793db49951c78502fa950578a4288da0.jpg
 
Tukiacha Airport kuna barabara nyingi sana zinajengwa kwa kiwango cha lami na kuna mradi mkubwa wa maji umeelekezwa chato. To be honest Chato inapendelewa sana ila ni mji mdogo sana tena sana. Yaani in bora hata Katoro/Buselesele aisee
 
Mkuu barafu,

Mbona unafanya kama hii habari ni ngeni kwako? Hivyo vipimo tulivijadili sana wakati ule na kuhitimisha kwamba kinachojengwa Chato ni International Airport!!! Kwa kuzingatia runway yake; kama ulivyosema haujaachana sana na JK Nyerere International Airport! Tukajaribu kuhalalisha kwamba, okay, fine... je, hakutakuwa na economic impact kwa huo uwanja... watetezi wa kila kitu wakadai utachochea utalii... nikaombe nitajiwe vivutio vya kitalii vilivyopo Chato! Hadi mjadala ule unafungwa; sikutajiwa hata kimoja !

Tukajaribu kumwangalia Mkapa ambae haku-opt kujenga uwanja wa Masasi... tukafanya comparison ya umbali kati ya Mtwara to Masasi na Chato to Geita! Tukakuta umbali wa Mtwara to Masasi ni karibu mara mbili ya umbali wa Geita to Chato! Hapa tukahoji, ikiwa Mkapa aliweza kutumia uwanja ulio karibu mara mbili zaidi hadi kwao compared to JPM, nini Mheshimiwa kinamfanya ashindwe!

Itoshe tu kusema kwamba, huwezi hata kidogo kulinganisha Heliport na Uwanja wa ndege!!! Kwa Rais kuwa na Heliport, hasa ukizingatia direction ya nyumbani kwa JK; kwa hakika angalau inasameheka! Kwamba, ili asiwe anatengeneza disaster barabarani kwa sababu tu anakwenda kwake; basi ni heri atumie chopper! Na kama atumie chopper, chopper ya Rais haiwezi kutua popote as if ni chopper ya askari!

Aidha, huwezi pia kulinganisha daraja la Mkapa na Uwanja wa ndege! Daraja la Mkapa linamsaidia hata mshona viatu na mpasua matumbo ya samaki pale Ferry... lakini sio Uwanja wa Ndege! Daraja la Mkapa ni daraja la wananchi... daraja ambalo lingeweza kujengwa na Rais yeyote hata kama si wa Kusini... kama JK na Malagalasy yake! Huwezi hata chembe kulinganisha bandari (ya Bagamoyo) na EPZ huko Bagamoyo na uwanja wa ndege, kwa sababu; hivyo ni vitega uchumi vitakavyomnufaisha kila mmoja!! Kama ambavyo huwezi kuthubutu kusema Bandari ya Dar es salaam imejaa Wazaramo na Wandengereko! Kinyume chake, Uwanja wa Chato zaidi ya kumnufaisha Mheshimiwa na team yake hakuna kingine cha ziada!

Nachelea kusema kwamba, ulevi wa aina hii wenzake huwa wanaufanya wakiwa wameshakaa sana madarakani kiasi cha kujisahau na kudhani wanaongoza kampuni zao binafsi! Kinyume chake jambo kama hilo linapokuja kutokea within 1 years of administration; inatosha kabisa kuwa RED FLAG ya kuwafanya watu wahoji... "what next?" BoT; UChato (cf UDOM), Central Railway Station (Western Zone), Zonal Investment Center... anyway, karibu tumalizie ujana!!!
Good analysis
 
Mleta mada nakupongeza sana kwa kusema ukweli.

Nilisikitika sana wakati uwanja wa ndege wa Mpanda unaanza kujengwa.Nilijitahidi kuwauliza baadhi ya viongozi , kwanini uwanja na si kuboresha Huduma za afya katika hospitali yetu ya wilaya ambazo ni duni ?

Jibu la utetezi nililopewa ni kuwa eti "UNHCR wametoa fedha bilioni kadhaa kwa ajili ya shukrani kwa kuwatunza wakimbizi wa Rwanda na Burundi kwa miaka mingi.Hivyo tuchague hizo pesa tufanyie mradi gani wa maendeleo na serikali yetu imeamua kutuongezea pesa zaidi tujenge uwanja wa ndege wa kisasa".

Tatizo kubwa la nchi hii ni kutotambua vipaumbele.Auric Air ilikuwa inapiga trip za Dar -Mpanda kwa zaidi ya Tsh.500,000/- one way.Jiulize ni wakazi wangapi wa Mpanda wanamudu kulipa nauli hiyo.Kama watakuwa wengi hawazidi watano kwa kila tripu.Kwanini mabilioni yote hayo uyawekeze kwa watu wachache na si mahitaji ya walio wengi kama Huduma za afya na elimu.

Pinda kaondoka Mpanda katuachia Uwanja wa ndege ambao hautamfanya akumbukwe wala kuheshimika .Hata kama ilikuwa ni mipango ya kuacha alama basi pale alifeli mara mia angejenga Chuo kikuu angeheshimika na angesaidia sana watanzania wa kutoka pande zote za nchi hii.
 
252 Reactions
Reply
Back
Top Bottom