Kwa ugumu wa maisha nilionao, michango inayoendelea inanifikirisha sana

Asante sana kwa faraja yako bila kashfa wala maneno ya kuudhi kama wengine ,, ubarikiwe mnoo popote ulipo mkuu

Naamini kuna siku nitaandika mrejesho hapa
Wapo wengi tu sister,ni kupambana tu,hakuna mbadala!
Kipindi bado ni mwanafunzi wa chuo,nilikuwa naishi na Anko wangu aliye kuwa ameishia Std 7,(tulikuwa tunakutana kwa kaka mkubwa chuo kikifungwa),
Anko wangu,alikuwa ananiona kama vile Mimi kusoma chuo,nimeyapatia sana maisha,akawa ananiuliza,na yeye afanyeje atoke kimaisha,kwanza alianza kuuza mitumba,baadae akaona hailipi,akaniomba nimsaidie kuandika mchanganuo wa mradi,ili autumie kuomba mtaji kwa ndugu yeyote.
Miaka ya 2000,kulikuwa na biashara sana ya vibanda vya simu,tukaandika mchanganuo,tukapitisha bakuri,ndugu na jamaa wakachangia,wengine walikuwa kwenye haya makampuni ya simu,enzi hizo buzz Gsm(tigo),wakampa vifaa,akafungua vibanda kibao vya kupiga simu,
Baada ya miaka miwili,jamaa alikuwa ana cash ya kutosha mpaka akaagiza container zima la computer ili afungue internet cafe,
Uwezi amini,by the time namaliza chuo,pocket money ya kuzungusha bahasha mjini,nilikuwa naomba kwake,
Jipange tu mdada,kutoka inawezekana,
Too bad,Anko wangu alifariki 2005,

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh! Nimekuelewa aisee
Tabia ya pesa inapenda uthamani(value) ndio maana watu smart wanakwambia jiengezee Value ndio pesa itakifata...ni rahisi kwa Maxence Mello kupata uCEO wa AirtelTZ kuliko wewe usie na value, Rahisi MilladAyo kupata mchango wamatibabu akiumwa kuliko wewe, Rahisi Diamond kupata Deals za MaBillion kuliko muuza nazi mtaani.

Value ya Mbowe huwezi ifananisha na yako na value hiyo Mbowe hakuitenheneza Overnight inaelekea kipindi ambacho ndio wazo la ku-engage kwenye politics watu walimuona hana kazi yakufanya ila leo anauwezo wakichangiwa mpaka 500M kwa value aliyoitengeneza.

So usipende Shortcut tafuta vibarua, kazi za Ali ya chini, jiajiri locally ukishapata pesa utaiyengeneza Value yako zaidi.

Portfolio | 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kudhani kuwa siasa haikuhusu ni utoto. Kaa utafakari vizuri utagundua kwa hali yoyote uliyo nayo huwezi ikwepa siasa,wanasiasa ndio wanaamua mambo yaende vipi.

Hata uwe na uwezo kiasi gani huwezi jenga shule ili wanao wasome, huwezi jenga barabara ili usafiri, huwezi jenga hospitali ili utibiwe, huwezi tunga sheria zako, huwezi kuwa na jeshi, huwezi kuwa na mfumo wako wa uwekezaji, huwezi jitungia sera zako na mengine mengi huwezi kujifanyia.

Unahitaji entities za kushughulika na hayo mambo,ndipo issue ya serikali na organ zake na siasa zinapata mashiko.

Kuna wengi walikuwa wanajifanya hawajishughulishi na siasa kwamba wana vishughuli vyao eti watapoteza muda,leo hii vimekufa kwa siasa za awamu hii ndio wanastuka kuwa kumbe siasa ni sehemu muhimu ya maisha wakati ni too late.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, upo sahihi sana kwa msimamo wako. Na hivyo ndivyo inatakiwa kuwa, wanasiasa waweke miongozo/kanuni na sera imara ili sisi watu wa chini tuneemeke, sadly though kwa nchi yangu siamini hivyo, ila sipingi wengine kuendelea kuamini kama wewe.
 
Sasa mkuu kama hii kachanga mtu mmoja tu angalia usife kwa kihoro
FB_IMG_1583944438500.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kumbuka tu, hakuna mwanasiasa nchi hii anaweza kubadilisha hali yako, pambana tu mkuu. Hizi za tusirudie makosa ni propaganda tu ili tubadilishe walaji wa mkate wetu wa taifa, kiuhalisia wewe na mimi ndio tupambane na hali zetu.
ukipata "walaji mkate" zaidi ya mmoja lazima atakuwepo mwenye unafuu kidogo kati yao.
ukiona analegalega, baada ya miaka 5 unaweka mwingine.

bora wape "walaji" wapokezane kuliko mmoja anayekula hadi anajisahau anaanza kuwaita wenziwe malofa, nyumbu, nk.
 
Mkuu, upo sahihi sana kwa msimamo wako. Na hivyo ndivyo inatakiwa kuwa, wanasiasa waweke miongozo/kanuni na sera imara ili sisi watu wa chini tuneemeke, sadly though kwa nchi yangu siamini hivyo, ila sipingi wengine kuendelea kuamini kama wewe.
Ni kweli mkuu usemacho,kwa kwetu haijawa hivyo bado. Na moja ya sababu ni ulevi wa madaraka yaani watu wanaona hata wakiboronga vipi hamna cha kuwafanya,hata mkiwakataa kwa kura wataendelea kuwepo kwa 'nguvu' na hii ni hatari sn kwa ustawi wa taifa.

Watu makini hawataweza kuishi ama kuwekeza hapa kwa kuwa risk ni kubwa sn chochote kinatokea muda wowote. Ikifika level hii madhara yanaanza kutuhusu wote.

Tazama elimu ilivo mbovu,tazama huduma za afya, tazama mfumo wa utoaji haki, rushwa, ukandamizaji wa watawala, ajira hakuna, mrundikano wa kodi, biashara zinakufa then unaambiwa uchumi unapaa. Tukifika hatua hii hakuna aliye salama.

Lakini tusimsusie fisi bucha, moja ya namna bora ya kuwaweka tumbo joto ni kuwaonesha kuwa hatuwakubali na mambo yao, hivyo tuendelee kuonesha hisia inapobidi iwe kupitia uchaguzi au matukio kama hili la kesi ya jana nk.

One day yes,monkey will go to town!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asnte kwa nielewa mkuu yani wewe umenielewa haswa nilichomaanisha
Kuna watu pesa kwao sio shida, ndio maana mtoa mada anasikitika kuwa yaani yeye mlo wa siku ni issue wakati kuna milioni 350 zimechangwa kwa siku moja tu, na watu wametoa hadi 10m, dadeq "sema sina hela..."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kwenda GoFundMe.com ukapige harambee huko.

Unaweza kushangaa kwa furaha juu ya kile kinachoweza tokea.
Watu kule Wachoyo. Mtu anachangia Dola 1. Mimi Nilizani kule wanaanza na Dola 100. Kuna mtu nilifuatilia Mchango wake huko nikashangaa utoaji wa majuu Dola 1.
 
Wewe hutaki kufanya kazi umekaa kijiweni
Hellow poleni na majukumu
Ni jioni tulivu namshukuru Mungu ninaafya tele

Tumeona hukumu ya viongozi wa chadema
Mamilioni ya mapesa
Basi ile sijakaa sawa nikaona kwenye mitandao hamasa ya michango
Namba zikatolewa za kutosha
Basi giza tororo likazidi na joto likanizidia mana hata hela ya umeme sina nikapitiwa na usingizi nikala
Asubuhi baada ya shuhuli hapa na pale naona michango imetimizwa ya mamilio ya mapesa
Kigogo kaposti na risiti tena ya kawaida si ile ya EFD tulohamasishwa tuzitumie.

Imenifikirisha mno juu ya hali ngumu niliyonayo ambayo nakosa hela kidogo ya mtaji ili niweze kujiingizia kipato
Maajabu ni kwamba kwa maelezo hela imechangishwa na wananchi

Wapendwa wanaJamii Forum wenzangu hebu naombeni tu mnipe kazi ya kufanya na mimi nipate kipato ama wa kunikopesha mtaji na mimi niweze kuanza biashara ,si mchango wa haya mamilioni hapana ni mataji tu wa laki 5 kwani nina watu nyuma wananitegemea mnoo

Natanguliza shukrani zangu za dhati ,,ila kiukweli bado nafikiria yale mamilioni yaliyochangishwa kwa haraka vile sijui wenzangu wanapataje hela na mimi nakwama wapi!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Looh, tulikuwa tunadanganywa eti hali mbaya mara vyuma vimekaza. Sasa ipo wazi hiyo hoja haina mashiko tena.

Nawaasa kwa spidi hii hii, hakikisheni kila mkoa una kiwanda, vituo vya afya na kuboresha shule za kata.
 
Back
Top Bottom